Wanaodhania CHADEMA itapoteza umaarufu kama NCCR-MAGEUZI wanajidanganya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaodhania CHADEMA itapoteza umaarufu kama NCCR-MAGEUZI wanajidanganya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nitonye, Sep 25, 2012.

 1. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Kumekuwepo na kila aina ya makala zinazoongelea maisha ya chama cha democrasia na maendeleo( CHADEMA) kuelekea kupoteza umaarufu wake. Sababu zinazoelezwa ni vurugu zinazotokea kwenye maandamano na kwenye mikutano ya hadhara kama kule Iringa, Morogoro na kule Arusha.

  Ikumbwe kuwa kipindi NCCR-MAGEUZI iko juu hakukuwepo na mwamuko hasa kwa vijana kulingana na matukio ya ufisadi kwenye serikali. Kwa sasa hakuna cha kuinyamazisha Chadema kwa maana umaskini umezidi kuitesa jamii na jamii imeshachoka hivyo inataka mabadiliko.
   
 2. commited

  commited JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  mkuu Mungu ni mwema, na hakuna hakimu mzuri kama muda/ wakati.. kwa hiyo tuombe uzima, na Mungu Hatawaacha watu wake waendelee kuteseka miaka 50 na zaidi na hawa wezi na wahuni wasio na huruma kwa wananchi wao.. kuna jambo ataenda tu.
   
 3. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Vurugu za mwanza zina mkono wa magamba
   
 4. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Lengo lao ni kutaka kuichafua CDM lakini hawatafanikiwa
   
 5. Rohombaya

  Rohombaya JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 8,255
  Likes Received: 3,087
  Trophy Points: 280
  Kwani kiliichoisarambatisha NCCR nini? Ni ukosefu wa demokrasia ya ndani pamoja kuwa na mapandikizi ya ccm. Mwenyekiti alikuwa ndiyo chama. Hili lichukuliwe kama tahadhari kwa CDM pia kama kuna mapandikizi yang'olewe kabla ya mvua kuanza kwani yakikomaa haitakuwa kazi rahisi kuyang'oa.
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Siyo maandamano na migomo pekee, mvutano ndani ya chama kama vile ambavyo tunasikia kule Mwanza, mvutano baina ya ZITTO na M/kiti na Katibu mkuu, bila kusahau udikteta ambao SHIBUDA anauelezea kuwemo ndani ya CDM siyo kwmba ni tishio kwa uhai CDM bali ni hatari kwa Taifa zima kwa vile watanzania watajifunza tabia ambazo hazina maslahi kwa Taifa.
   
 7. t

  thatha JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mtaishia kusema hivyo 2. CCM yenyewe inachapa mwendo. Kamateni huyo gamba mmchape aache kuwavuruga. Kweli mbaazi ikikosa maua husingizia jua.
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  CDM watatafuta mchawi sana lakini mwisho wa siku, mchawi ni mfumo wa kimafya ndani ya chama hicho. Na hili litawagharimu sana kwa vile ni vigumu sana viongozi kulikubali hili.
   
 9. t

  thatha JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kama kweli kuna tatizo katika serikali ya sasa, basi mabadiliko hawezi kuletwa na CDM, hiki chama hakiwezi kufanya vizuri zaidi ya CCM hata siku moja hasa ukizingatia kuwa viongozi wake wengi hasa wa ngazi za juu ni makapi kutoka CCM.
   
 10. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wasemaji wa chadema nwengi!
   
 11. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Unamaanisha CHADEMA itadumu milele au?
   
 12. tanira1

  tanira1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  chadema sio nssr moja wala sio ccm mbili kuchujuka chadema ilo ni ndoto nani ajasikia leo kuwa kikwete kakili chaguzi za ccm watu wamemwaga ngawila? mtanzania gani mwnye akili achague mmwaga ngawila kwenye chama chake huyo ukimpa nchi si atatumaliza watanzania wameona na wamesikia safari hii hawadanganyiki tena hawakubali kuambiwa vierehere vyao vya kuwachagua wamwaga ngawila ndio vimewaponza
   
 13. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  propaganda hizi pia zinatumiwa na maadui wa CDM kuharibu sura ya chama mbele ya watanzania
   
 14. b

  blueray JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Usiwe na shaka hasa na baadhi ya watu waliotumwa na magamba kuivuruga CDM kama kina Shibuda. CDM ni taasisi, watu Kama hawa hawakosekani kwenye chama. Wanafahamika, hawana uwezo wa kuendelea kuhadaa wananchi na Siku zao ndani ya CDM zinahesabika! Mwisho wa siku mamluki wote wataenguliwa Kama pumba na mchele.hakuna mtu mwenye uwezo wa kuhadaa nguvu ya umma.
   
 15. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Umeandika "kama kweli" ina maana huamini kuwa kuna matatizo. Unaishi nchi gani?
   
 16. m

  muchetz JF-Expert Member

  #16
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 496
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Nina wasi wasi na unachotaka kutumaminisha (Pengine wewe ni wale wanachama wa ... unataka kujenga mgongano(confusion)), Unaposema demokrasia ndani ya chama una maana gani???? CDM wamefanya chaguzi zao zote kwa wakati na kwa uwazi(inawezekana kuna glitches ndogo hapa na pale, lakini ndiyo siasa). Nitajie chama kingine(including CCM) ambacho kimefanya hayo kwa kipindi cha takriban miaka 10 ilopita!!!

  CCM hivi sasa wako kwenye chaguzi zao za ndani lakini tayari mpaka bastola zimesha enda hewani!!! Na bado huoni bado huo ni ukosefu mkubwa wa demokrasia!!!!! Inashangaza. Hivi kuna wanavijiji wangapi wa huko Tabora(tukio lilitokea huko) wana uwezo wa kununua bastola(kwa kufuata taratibu tulizojiwekea)????? Kumbuka Tabora kama sehemu nyingine nyingi za Tanzania asilimia zaidi ya 80 wako vijijini. Huoni uongozi ndani ya hicho chama ni malirithi (Inheritance)?

  Unachotaka kutuaminisha (behind the scenses) ni kuwa (eti) CCM wana demokrasia ya ndani!!!!! Pathetic!!!!!

  "So while your point your finger someone else is judging you" ... Bob Marley.
   
 17. Rohombaya

  Rohombaya JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 8,255
  Likes Received: 3,087
  Trophy Points: 280
  Mheshimiwa muchetz,
  Ninasikitika kwamba haukunielewa post yangu na sitachelea kusema kuwa hii imesababishwa na ushabiki mkubwa ulionao kwa CDM ( Post yako inaprove kwa 100%). Ni mtu asiye timamu ndiyo atakaye kataa matibabu eti kwa hoja ya kwamba kaenda hospitali akakuta kuna wagonjwa wengine wanaumwa kuliko yeye kwa hiyo akajiona yeye ni afadhali na hahitaji matibabu tena. Kama CCM inafanya jambo baya kwa kiasi cha juu basi hii isiwe ruksa kwa CDM kufanya angalau kwa kiwango cha kati kwani hii haitakuwa inaitendea vyema demokrasia ya watanzania. Kama tunataka kuwa huru katika kufikiri basi tusizongwe na uCDM au uCCM katika vichwa vyetu kwani bila kufanya hivyo basi tutakuwa tunajaribu kutetea mabaya ya vya vyama vyetu yaonekane mazuri.
  Hata hivyo kwenye sikusema kwamba ndani ya CDM hakuna demokrasia ila ni wewe tu umekurupuka.

  Note: Mimi ni mpigakura huru na sio mwanachama wa chama chochote hadi sasa
   
 18. Monyiaichi

  Monyiaichi JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 1,825
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  vurugu zote zinazotokea kwenye mikutano ya cdm ina mkono wa chama tawala, wala hilo halina mjadala. Huwezi kumwona jk akifanya hizo fujo au katibu mwenezi au kiongozi yeyote, wanatumia watu wengine, especially vijana wachovu ambao wote wanajumlishwa kuwa ni wanachama wa cdm. Katika mikasa ya mauaji hutegemei kumwona yule muuaji akienda kwenye tukio-may be rarelly, anatuma watu/mtu, kwa hiyo huondoa ushahidi kuwa ninani mhusika.
  Secondly- hivi umewahi kusikia viongozi wa cdm wakimlalamikia zzk au shibuda? Kwa nini hawajawahi? Basi wanajua jambo, waachieni tu wana uwezo wa kuhandle hiyo situation.
  Na hata kama hawaelewani, kuna migogoro, ndio hiyo inayosababishwa na umamluki, mwenye akili anatambua kwa urahisi tu, msing'ang'anie sana kupigia mstari kutokuelewana au migogoro ndani ya cdm ambayo wakati mwingine pia ni lazima iwepo. People differ in thinking, in perceptions na hamna haja ya kulazimisha cdm ndio wasiwe na hiyo kasoro.
   
 19. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Hayo ndio maombi yao..ila wakiandika wanashindwa sema wzi kuwa hayo ndio maombi yao.
   
Loading...