Wanaodhani ni Tigo tu wanajidanganya, lakini hata wanaotuchungulia nao wanachunguliwa

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Asalam-aleikhum Wana-JF!

Niko kwenye mada tayari. Yule wakili wa TIGO ktk kesi ya Mbowe na wenzake jana tarehe 02/11/2021 amefunua uvundo (a can of worms) katika kampuni za simu na TCRA kwa upande mmoja na kwenye vyombo vya Dola na Serikali yenyewe kwa kiwango kinachotia wasiwasi.

Kwa bahati mbaya hizi kampuni za simu, Airtel, TIGO, Halotel na Vodacom (ukiondoa TTCL) uongozi wao au wanahisa wao wakuu ni kutoka mataifa ya kigeni. Unafikiri hawajui chochote kuhusu uingiliaji wa mawasiliano ya wateja wao hapa nchini? Na wateja wao si pamoja na Serikali yenyewe na vyombo vya Dola?

Tuamini vipi kwamba hao wageni hawana access kwa taarifa zetu binafsi na za taasisi nyeti kama wao ndio wanatuletea, wanasimamia na kuweka mbinu za kuhifadhi data na kulinda mawasiliano yetu kila mahali?

Kama hiyo haitoshi, hata benki zetu CRDB, NBC, NMB, nk. na za kimataifa kama Barclays, EXIM, nk nako siri za account zetu zinachunguliwa kiholela tu, tunaaminije baadhi ya mabenki hayo hayatoi siri zetu hata kwa adui zetu kisiasa, kiuchumi nk?

Yaani kwa hili vundo watu wenye uelewa na imani katika misingi ya demokrasia na utawala bora wangeficha sura zao kwa AIBU!

Lakini ningependa kujadili maswali kadhaa kuhusu athari za hili jambo, katika sura yetu kama taifa na mbele ya vyombo na wadau wa nchini kwa upande mmoja na kimataifa kupitia taasisi zao hapo juu kwa upande mwingine; ili tujiulize kwamba kesi hii kama imetungwa, ni kwa faida ya nani hasa?

Kama taarifa za mawasiliano yangu mimi mtu binafsi katika simu, mitandaoni, benki, hospitali na popote nilipo na wakati wote zinachunguliwa na vyombo vya Dola (polisi, takukuru, NIDA, tiss, jwtz, immigration nk. Kwa kweli hata mtu binafsi anaweza kukuingilia kupitia watu kama huyu.
Kwahiyo kwa mtindo unaojidhihirisha katika kesi ya Mbowe hakuna aliye salama!

1. Swali muhimu la kujiuliza ni kwamba je: Katika mazingira kama haya, wakubwa hao (labda sio wote) lakini inadhirika baadhi yao wako nyuma ya vitendo hivi; wenyewe wana uhakika gani kwamba wako salama na watakuwa salama mbele ya safari baada ya kuondoka kwenye nafasi walizonazo?

Mimi sipendi jambo hilo litokee, kwangu binafsi, kwako na kwa viongozi wetu.

2. Juzi juzi tu kule Dodoma katika mkutano wa Waziri Mkuu na Mawaziri wote wa Serikali; iliripotiwa kwamba Serikali inataka wasemaji wa vyombo vya Serikali wasitoke nje ya mfumo wa Serikali yenyewe ili kuepusha kuvuja kwa siri za Serikali.

Kwahiyo swali la pili muhimu la kujiuliza tena ni, je:

Walengwa wa maelekezo haya ya Waziri Mkuu; yaani wao wenyewe kila mmoja kama Waziri na akiwa yeye binafsi pamoja na hizo taarifa alizonazo za siri Serikalini na huko kwenye mabenki ya ndani na ya kimataifa; mitandaoni, NIDA, TCRA, TIGO, polisi nk; yuko salama kweli?

Viongozi wetu kama Mawaziri, RCs, DCs, Wabunge, nk. wote kila mtu labda yeye na mkewe, watoto na ndugu zao ni wamiiliki wa simu za aina zote mpaka hizo smartphones, na wanawasiliana na kila aina ya watu ndani na nje ya mipaka ya nchi. Wana account kwenye mabenki mbali mbali nk. Na baadhi yao kama Wabunge, hasa wale wenye elimu ya msingi, simu zao ziko salama kiasi gani?

Wote wana uelewa wa ku-detect uingiliwaji wa simu zao, za wake zao au za watoto na ndugu zao? Na hawa nao hawana no siri za Serikali pia?

Yaani lazima tujiulize hata hao walioko kwenye taasisi nyeti za nchi, katika hali hii, siri zao ziko salama kiasi gani huko benki, TCRA, NIDA, Polisi, TIGO nk.?

Nihitimishe kwa kusema wahenga waliposema: 'kikulacho kinguoni mwako' walikuwa na maana kubwa sana! Kwenye kesi hii ya Mbowe, tuwe tayari kujifunza, vinginevyo tutaliwa.
 
New world order.

mpango mpya wa kuitawala dunia.
Yaani Sasa hivi Wana jua Mimi nimelala wapi na wakinitaka wanipate wapi.

Itafikia hatua mtu hazaliwi mbaya dunia itoe ruhusa.
 
Asalam-aleikhum Wana-JF!

Niko kwenye mada tayari. Yule wakili wa TIGO ktk kesi ya Mbowe na wenzake jana tarehe 02/11/2021 amefunua uvundo (a can of worms) katika kampuni za simu na TCRA kwa upande mmoja na kwenye vyombo vya Dola na Serikali yenyewe kwa kiwango kinachotia wasiwasi...
Kwenye kesi inayopelelezwa na serikali kote Duniani Wahusika wanatoa taarifa zote zinazohitajika mahakamani iwe bank,simu au social media
Jipange.
 
Kweli kikulacho kinguoni mwako. Tena watu washaliwa tayari na nguo zimeanza kushambuliwa.
Kama taifa tupo mashakani maana kweli nimwendo wa kuchunguliwatu

Ila kusema ukweli kwa hili la Tigo wameonyesha ni kampuni ya hovyo sana ambayo haina chain of command na ndio maana matapeli wengi wanao ibia mawakala wanatumia tigo…..haiwezekani kampuni kubwa kama hii mtu mmoja afanye kila kitu yeye mwenyewe..

Mm sio mwanasheria lakini naamini kuna maswali mawakili wautetezi waliya acha au kusahau kama namna barua ilivyotumwa kama walitumia dispatch book na kuonyesha mpokeaji nani na pia kujua yeye kama mwanasheria anaingiaje kwenye mifumo ya kampuni wakati yeye sio It technician wa kampuni.
 
Ni kawaida ya mitandao yote hapa nchini nafikiri kabla yakupewa leseni na serikali huwa kuna mambo ukubaliane nayo maana wakati wa Makamba na Nape tunakumbuka Vodacom na walitoa siri.
 
Back
Top Bottom