Wanaodhani Afrika nzima haina demokrasia waje wajifunze Malawi

ikhlas

JF-Expert Member
Jun 25, 2015
550
500
KUTOKA KWA MALISA GJ
Nimetafsiri kutoka kwa dada Maria Mhandire wa Lilongwe.
____________
Wanaodhani Afrika nzima haina demokrasia waje wajifunze Malawi. Nadhani sisi ndio nchi ya kwanza kwa demokrasia Afrika na tuna mengi ambayo hata wazungu walioanzisha demokrasia wanaweza kujifunza. Kwa wale wasio wakazi wa Malawi ngoja niwaeleze hali ilivyo hapa;

Mwaka huu tutafanya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge. Rais Peter Mutharika anagombea kwa awamu ya pili kupitia chama tawala cha DPP.

Makamu wake Saulos Chilima anagombea kupitia chama cha upinzani cha UTM.

Yani Rais na Makamu wake wanagombea kupitia vyama viwili tofauti, na kampeni zinaendelea, kila mmoja akinadi sera zake.

Wakikutana kwenye matukio ya kitaifa wanakaa pamoja kama Rais na Makamu wake. Baada ya hapo wanakutana majukwaani wakipingana kwa hoja.

Mutharika na Chilima walikua chama kimoja cha DPP. Lakini mwaka jana wakatofautiana. Chilima akajiondoa na kujiunga na chama cha upinzani cha UTM.

Hakupoteza nafasi yake ya Umakamu wa Rais, maana Katiba ya Malawi inaruhusu kiongozi kuhama chama bila kupoteza nafasi yake ya uongozi.

Mgombea mwingine ni Atupele Muluzi, Waziri wa ardhi ambaye anagombea kupitia chama cha upinzani cha UDF.

Rais Mutharika hajamfukuza kazi. Kamuacha aendelee na kampeni za Urais akiwa bado Waziri wa ardhi.

Demokrasi ya hali ya juu.
Rais wa zamani Joyce Banda nae anagombea kupitia chama chake cha PP.

Licha ya tuhuma za ufisadi zinazomkabili, lakini Rais Mutharika ameruhusu agombee akisema wananchi ndio watakaoamua.

Mgombea mwingine ni Lazarus Chakwera wa MCP. Hiki ndio chama cha ukombozi cha Malawi. Ndio chama cha Rais wa kwanza Hastings Kamuzu Banda.
Kampeni zinaendelea.

Hakuna vurugu, kakuna fujo, hakuna polisi wanaopiga raia. Hakuna drama za kijinga za polisi kuvuruga mikutano ya wapinzani kwa taarifa feki za kiintelijensia.

Wanaotaka kuandamana wanaandamana, Wanaotaka mikutano ya hadhara wanafanya. Wanaotaka vikao vya ndani ewala. Ili mradi kila mmoja anatumia njia yake kushawishi achaguliwe.

Raia wa Malawi tunaendelea na maisha yetu kama kawaida, tukila Nsima (ugali) na kusikiliza sera za kila mgombea. Ni mataifa machache sana duniani yanaweza kuwa na kiwango hiki cha demokrasia. Tunajivunia nchi yetu.!
 
Richard irakunda

JF-Expert Member
Oct 23, 2018
3,512
2,000
Achana nao, tufanye ya kwetu. Kwanza ule mgogoro wa Ziwa Nyasa sijui uliishia wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
Uliisha baada ya Joyce Banda kujikuta sio raisi wa Malawi
Pia waliona mkwere kawapania kweli ikabidi wavunge tu

Ila mara madai ya kuwa ziwa lote ni lao huwa yanakuja kipindi cha uchaguzi kama hichi lkn nadhan wameamua kuwa wapole tu maana awamu hii diplomasia ni ZIRO

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,237
2,000
Hongera nyingi ziwafikie. Kwa aina hiyo ya demokrasia, hakika ni mfano wa kuigwa. Huku kwetu wakati wa kampeni, watu kugombania fito, ni jambo la kawaida.
 
Ekuweme

JF-Expert Member
May 28, 2018
1,780
2,000
Uliisha baada ya Joyce Banda kujikuta sio raisi wa Malawi
Pia waliona mkwere kawapania kweli ikabidi wavunge tu

Ila mara madai ya kuwa ziwa lote ni lao huwa yanakuja kipindi cha uchaguzi kama hichi lkn nadhan wameamua kuwa wapole tu maana awamu hii diplomasia ni ZIRO

Sent using my iPhone using jamiiforum app
Awamu hii Diplomasia ni empty

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
2,239
2,000

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,777
2,000
Huku kwetu ingekuwa kila siku watu wanafungwa, wanaumizwa, wanauawa, wanatekwa, wanafunguliwa kesi za kijinga n.k.
 
senzighe

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
1,492
2,000
KUTOKA KWA MALISA GJ
Nimetafsiri kutoka kwa dada Maria Mhandire wa Lilongwe.
____________
Wanaodhani Afrika nzima haina demokrasia waje wajifunze Malawi. Nadhani sisi ndio nchi ya kwanza kwa demokrasia Afrika na tuna mengi ambayo hata wazungu walioanzisha demokrasia wanaweza kujifunza. Kwa wale wasio wakazi wa Malawi ngoja niwaeleze hali ilivyo hapa;
Mwaka huu tutafanya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge. Rais Peter Mutharika anagombea kwa awamu ya pili kupitia chama tawala cha DPP. Makamu wake Saulos Chilima anagombea kupitia chama cha upinzani cha UTM.
Yani Rais na Makamu wake wanagombea kupitia vyama viwili tofauti, na kampeni zinaendelea, kila mmoja akinadi sera zake. Wakikutana kwenye matukio ya kitaifa wanakaa pamoja kama Rais na Makamu wake. Baada ya hapo wanakutana majukwaani wakipingana kwa hoja.
Mutharika na Chilima walikua chama kimoja cha DPP. Lakini mwaka jana wakatofautiana. Chilima akajiondoa na kujiunga na chama cha upinzani cha UTM. Hakupoteza nafasi yake ya Umakamu wa Rais, maana Katiba ya Malawi inaruhusu kiongozi kuhama chama bila kupoteza nafasi yake ya uongozi.
Mgombea mwingine ni Atupele Muluzi, Waziri wa ardhi ambaye anagombea kupitia chama cha upinzani cha UDF. Rais Mutharika hajamfukuza kazi. Kamuacha aendelee na kampeni za Urais akiwa bado Waziri wa ardhi. Demokrasi ya hali ya juu.
Rais wa zamani Joyce Banda nae anagombea kupitia chama chake cha PP. Licha ya tuhuma za ufisadi zinazomkabili, lakini Rais Mutharika ameruhusu agombee akisema wananchi ndio watakaoamua.
Mgombea mwingine ni Lazarus Chakwera wa MCP. Hiki ndio chama cha ukombozi cha Malawi. Ndio chama cha Rais wa kwanza Hastings Kamuzu Banda.
Kampeni zinaendelea. Hakuna vurugu, kakuna fujo, hakuna polisi wanaopiga raia. Hakuna drama za kijinga za polisi kuvuruga mikutano ya wapinzani kwa taarifa feki za kiintelijensia.
Wanaotaka kuandamana wanaandamana, Wanaotaka mikutano ya hadhara wanafanya. Wanaotaka vikao vya ndani ewala. Ili mradi kila mmoja anatumia njia yake kushawishi achaguliwe.
Raia wa Malawi tunaendelea na maisha yetu kama kawaida, tukila Nsima (ugali) na kusikiliza sera za kila mgombea. Ni mataifa machache sana duniani yanaweza kuwa na kiwango hiki cha demokrasia. Tunajivunia nchi yetu.!
Kila nchi ina utaratibu wake na inaonekana vyama vya upinzani nchini Malawi ni vyama vya kweli vya kisiasa.Hali kama hiyo itafikiwa kama chama chama cha CHADOMO kitageuka kuwa chama cha kisiasa na kisiwe cha uanaharakati na matukio.Hapo tutakuwa kama Malawi.Kwako G J
 
Clemence Mwandambo

JF-Expert Member
Dec 2, 2018
769
1,000
Hatuwezi kuiga ya Malawi kwa sababu nchi yetu haiwezi kuwa malawi. Hata nchi za ulaya waanzilishi wa demokrasia nazo zimetofautiana. Historia ya TAIFA lolote ndiye muumbaji wa utamaduni wa TAIFA hilo.
 
Makuku Rey

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
2,440
2,000
[QgUOTE="Mpinzire, post: 30404469, member: 120266"]Kama tungekuwa na demokrasia ya kweli ndani ya vyama vyetu leo hii toka 2005 tungekuwa na mwenyeviti 3 wamepita chama chetu cha Demokrasia yaani Mbowe, Chacha na Zitto ila kilichotokea Allah mwenyewe anajua[/QUOTE]

Jf inasajili watu wenye udumavu WA akili!hapa inazungumziwa democracy ya nchi lakn wewe unaanza kuizungumzia Chadema!!!Hivi Chadema ni chama tawala???naboreka Sana na watanzanià wenye bongo bikra!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom