Wanaodai Zitto Hakushiriki Opereshen za Chama ni fitna tu:Tumaini Makene Alishajibu hilo.

Status
Not open for further replies.

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,428
Wadau,

Kuna watu kwa muda mrefu wanakazana sana Kumchafua Kijana Zitto kwa sababu wanazozijua wao.Miongoni mwa hoja wanazotumia ni kwamba ati hakuwa akishirikiana na wenzake katika shughuli za Chama.Hebu turejee taarifa ya Tumaini makene ambaye ndie msemaji wa chama ya tarehe 18 August 2013.
USAHIHI: Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na kujitenga na ziara ya viongozi wakuu


Kwa mukhtasari, katika Taarifa hiyo, Msemaji wa Chama Tumaini Makene aliitanabahisha jamii na kuionya kuwa makini na watu wanaodai kuwa Zitto hashirikiani na wenzake katika operesheni za chama , kwani wanaozua maneno hayo lengo lao ni kupoteza focus ya watu kwenye masuala ya msingi ya kitaifa hasa katiba.

"Wana CHADEMA wawe makini na upotoshaji au hila za kuwaondoa kwenye focus ya suala la Katiba Mpya, hasa ambapo kwa sasa chama kinakusanya maoni ya wanachama na wapenzi wake juu ya Rasimu ya Katiba Mpya"
Ilisema sehemu hiyo ya Ripoti ya Msemaji wa Chama ndugu Tumaini Makene.Katika ripoti hiyo, Makene aliambatanisha na maelezo ya Zitto, kuonesha kuwa maelezo hayo yalikuwa ni sahihi kabisa kama yanavyoonekana hapo chini:
"Moja, sijajitenga na ziara ya chopa. Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, kamati hii inasimamia mahesabu ya Serikali. Ziara inafanyika kipindi cha kamati za Bunge na hivyo sikuweza kushiriki kwani ni hatari mno kuacha PAC chini ya wabunge wa CCM peke yake. Leo kamati inahoji Wizara ya Elimu yenye madudu kibao, Hazina yenye kukusanya mapato yote ya Serikali na ratiba nzima nitawasilisha hapa. Haya yote uongozi wa chama unajua. Ni mgawanyo tu wa majukumu. Hata hivyo nimeshiriki kuandaa mikutano katika mkoa wa Kigoma na gharama zote za maandalizi nimetoa mimi. Hata gari anayotumia mwenyekiti huko Kigoma ni gari yangu. Kusema nimesusa ni uzushi sana wenye lengo la kuleta mgogoro kwenye chama.

Pili, mimi ni mbunge kutoka Kanda ya Magharibi. Kila kanda imepewa wajibu wa kujiimarisha kichama. Nimekuwa nilifanya hivi toka kanda zimeundwa. Kuanzia mkutano wa mwanzo nimekuwa nikitimiza wajibu wangu wa kuhakikisha kwamba kanda ya magharibi inakuwa imara kichama. Nimefanya ziara kadhaa mkoa wa Kigoma na mkoa wa Tabora. Hivi sasa kanda zote zinapaswa kufanya uchaguzi wa ndani ya chama. Nimeamua kuanzi tarehe 20 Septemba (mara baada ya Bunge mkutano wa 12 kumalizika) kuanza ziara ya kanda ya magharibi kuchochea ujenzi wa chama kuanzia matawi ili tuweze kuendana na ratiba ya uchaguzi. Ziara hii itafuata taratibu zote za chama na sijaamua naifanya na nani maana maafisa wa chama wanapingiwa na katibu Mkuu.

Ninasikitika sana kwamba kumekuwa na tabia za kuchonganisha viongozi wa chama bila sababu kwenye mitandao ya intaneti. Kwa mtu anayeipenda chadema hawezi kufurahi mambo haya.

Mimi kama Zitto siwezi kufanya jambo lolote la kuathiri chama changu ambacho nimeshiriki kukijenga kwa kadiri ya uwezo wangu. Ninaomba pia watu wengine watumie muda zaidi kuunganisha viongozi badala ya kuwagwa. Tunahitaji sana umoja na mshikamano wa dhati "


Sasa kusema ukweli inashangaza kidogo kwa hawa watu ambao leo hii wanadai Zitto hakuwa akishirikiana na wenzake kwenye operesheni za chama sijui chanzo chao cha habari ni nini. Zitto anasema amekuwa akishiriki kwa kadiri alivyokuwa amepangiwa, Msemaji wa chama anasema alikuwa anafanya kile alichopangiwa, halafu mimi na wewe tuko mitaani tunapiga kelele kwamba hakuwa anashiriki.Hii ni fitna na mwisho wa ubaya aibu
.Ni bora wale tunaofanya hiyo kitu tukaacha kwani si vizuri.

CC Eberhard
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom