Wanaodai Rais Magufuli kuongezewa muda ni wahalifu

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Uhalifu ni kufanya kinyume na katiba na sheria za nchi. Katiba ya nchi yetu imetoa vipindi viwili vya miaka 5 kila kipindi cha mtu kuwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, kwa hiyo kufanya kinyume na hilo ni uhalifu na kuvunja katiba na sheria za nchi.

Sioni kama kuna sababu ya vyombo vya dola kunyamaza na kushindwa kuwachukulia hatua wale wote wanaojitokeza hadharani kutamka wazi kwamba Rais Magufuli aongezewe muda baada ya kipindi chake kwisha. Watu hawa wanahatarisha amani ya nchi kwani nchi nyingi za Afrika zimeingia ktika vita ya wao kwa wao kwa sababu ya marais kujiongezea muda kinyume na matakwa ya nchi, hivyo kupuuzia kauli hizi ni kutengeneza bomu katika taifa.

Inawezekana watu hawa wametumwa au wanafanya hivyo kwa makusudi ili kupima upepo.
Niwaambie wazi hata wanaccm wengi hawaipendi hii kauli maana wapo vijana waliokuwa kuwa wamejikeza kwa wingi 2015 kutaka kugombea kupitia ccm ila JPM akateuliwa na chama chake, kwa akili nyepesi wanaosema lugha hizi wanadhani ni wapinzani tu ndio wanaweza kuzipinga la hasha hata wana ccm wengi hawataki hizi kauli.

Mbaya zaidi kama kauli hizi zitaendelea bila kuchukuliwa hatua, muda simrefu watajitokeza watu barabarani au mtu mmoja mmoja watakao dai kuwa JPM apunguziwe muda asiongoze hadi 2020 polisi mtawakamata na kuwaita wachochezi je hawa nao hawachochei?
 
Bahati mbaya hata yule uliekuwa unaota ama kutamani awe rais hataweza tena huenda asubiri baads ya miaka 40.
sabbu vyovyote iwavyo katiba ya CHADEMA na maendeleo iliyojipatia kwa kutobadirisha uongozi wa juu ni mfano bora sana wa kuigwa na Taifa hili.
 
Akili zako ndio zimeshadumaa kaka yangu, maana chadema siyo nchi wala hakuna Rais wa nchi aliyetoka chadema. be careful when you comment, usikurupuke tunaongelea Rais wa nchi wala hatuongelee mwenye kiti wa chama.
 
..watu au mtu mmoja mmoja watakao dai kuwa JPM apunguziwe muda asiongoze hadi 2020 polisi mtawakamata na kuwaita wachochezi?

Ikitokea hii kitu, DC wa wilaya husika ataagiza police wamkamate haraka mtu huyo na kumtia ndani kwa masaa yasiyopungua 72 kwa kumdhihaki Rais na kutishia amani ya Nchi
 
hao watu hawana tofauti na wale uamsho waliokuwa kizuizini.... kumweka rais madarakani kinyume na katiba ni uhaini...
 
Mimi sio mtabili Ila kwa anayo fanya mzee Kipara kwasasa ya visasi n chuki itamgharimu sana baada ya Utawala wake kuisha
 
Kwa mtazamo huu tunakoelekea naona katiba inaenda kusiginwa kwa urafi na tamaa ya madaraka kwa kisingizio cha muda hautoshi.

This is africa chini ya jangwa la Sahara
 
Hapo ndio utajua hatuna tofauti na DRC wala Burundi au Uganda we are Black

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
Ccm bana,,,kila wakiangalia hawaoni wa kumsimamisha 2025,sasa jitiada zinaanza mapema za umilele
 
Msukuma najua elimu yako ni ndogo sana Baba Wa Taifa alituachia katiba na ukomo wa Uraisi alisema hata watanzania wakikupenda vipi ni ni vipindi 2 Kama kweli tunamwenzi Baba Wa Taifa na Katiba ni vipindi viwili tu.Huo mfano wako Wa kocha hauna tija Nchi hii iko Chini ya Katiba

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Kuwa makini usije kuitwa mchochezi ila hiyo ni hali halisi kabisa

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 
Nyie endeleeni kumdanganya huyo jamaa ajiongezee mda ndo atajua kile kisemwacho jeshini " what makes grass to grow blood blood blood."
 
Kuna kila dalili kuwa hayo matamko yanayotolewa nchi nzima hivi sasa kwa wananchi wanaotaka Magu awe Life President, eti kwa kile wanachoita kuridhishwa na utendaji wake yana all blessings ya Presidaa wetu!

Kwa kuwa tubavyomjua Mkulu wetu jinsi ambavyo huwa hana 'kifua' cha kutunza jambo linalomkereketa, angekuwa tayari keshalitolea tamko la kuwaonya hao watu.

Kwa kimya chake tunachiokishuhudia hivi sasa kwa suala hili ni dalili tosha kuwa zina baraka zote za Mkulu!
 
Back
Top Bottom