Wanaobeza ushindi wa Simba sc, wajue kuwa katika mechi 5 zilizopigwa mpaka leo hakuna timu iliyoshinda kwa tofauti ya zaidi ya goli moja

Magoli mengi wala sio issue,Rivers utd walikuja hapa bongo wakawakanyaga Utopolo goli moja na kwao pia wakawakanyaga tena goli moja,kesi ikaisha.
Kwaiyo na nyie kesi itaisha kwa stahili iyo sio, kwa timu ya aina gani mliyonayo na kocha wa aina gani atakaewawezesha kuvuka kwa staili iyo? Ebu tuambie matokeo yenu ya mechi za ugenini ili tupate picha angalau ya kuwapa asilimia za kuvuka hatua inayofata
 
Kwani hao unaowaita mafunzo na mlandege ulivyokutana nao uliwafunga goli ngapi? Kipimo cha kwanza kukuonyesha timu yako ikoje ni izo timu unazozidharau wewe kwa maana uwezi kupata tiket ya kushiriki ligi ya mabingwa au kombe la shirikisho bila kufanya vizuri kwenye ligi ya ndani, Sasa Kama umeshindwa ushindani wa ligi ya ndani uko nje ndo utaweza? Mpira sio miujiza, mpira ni uwekezaji na kuwa na wachezaji bora, Kama unamtegemea mshambuliaji aina ya mugalu, au kibu denis ndo wakupe matokeo kwenye mechi kubwa unaanza kwanza kuwatathmini kuanzia ligi ya ndani wanazo goli ngapi mpaka sasa? Kama ligi ya ndani tu unayoidharau wewe wameshindwa kufunga vipi mashindano makubwa wanaweza?
Sasa kwani SIMBA SC ni failure ktk ligi ya ndani?
Kwa hatua aliyopo simba kwa sasa imepelekea nchi kupata nafasi ya kupeleka timu nne ktk mashindano ya CAF msimu ujao,
Mbili zitashiriki CAF CL na mbili zitashiriki CAF CC....

SIMBA SC inashika nafasi ya pili ktk msimamo kumaanisha kwamba anaenda direct ktk CL sasa wewe unapata nguvu wapi ya kusema kuwa ni failure hapa ndani.
Bado yupo ASCC hapa ndani
Bado yupo CAFCC kimataifa....


Pole sana kaka naona ushindi wa jana umekuuma sana ila utazoea maana huu ni mwendelezo,

SIMBA SC KLABU KUBWA KWA SASA AFRIKA

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Walichofaulu sana Waingereza sio tu uwekezaji wa ndani ya uwanja ila ni uzalendo wao kama taifa, tunaweza kusema mengi ila suala linapokuja timu ya England kwenye soka la Ulaya basi ni jambo lao wote kama nchi

Sahau kuhusu vita zamani taifa lilikuwa linasifika kisa vita (Millitary Supremacy) achana na kuhusu uchumi tayari mambo ya G8 mpaka G20 sio stori sana, sasa hivi mpira ni suala la NATIONAL PRESTIGE, kama taifa linaungana

Juzi wakati Liverpool, Manchester City, West Ham, Leicester City na Rangers wanafuzu hatua zinazofuata kwenye michuano ya Ulaya basi hashtag mitandaoni ilikuwa BREXIT BOYS RULLING EUROPE! Yes ni ufahari kwa visiwa vyote vya Uingereza

Sahau kuhusu uhasama wa Mersysides, sahau kuhusu uhasama wa Midlands au North East Rivarly, sahau kuhusu Glasgow Derby, wao suala la taifa lao ni suala lao wote! Media zao, Wachambuzi wao wanazipa nguvu timu zao

Hata Waarabu hapa Afrika wanafanikiwa kutokana na neno ARAB NATIONALISM, Yes! Ahly anapokuwa na jambo lake ile Cairo ipo kimya kupisha jambo la Mashetani, kule Morocco pia linapokuja suala lao ni wao

Yes! Mkifika Cairo kutoka huku Kusini mwa Jangwa la Sahara mnaulizwa swali “MMETOKA AFRIKA?” Yes wapo sahihi, huku kwetu tuna uswahili mwingi sana, hatumpi nafasi aliyejuu aendelee kuwa juu, tunataka wote tushuke tuchekane, hiyo ndio mentality yetu

Leo hii ukienda kusoma comments za Wasauzi kuhusu mechi ya jana kwa utafiti wangu ni 98% wote Wasauzi wapo nyuma ya Pirates, wanamaanisha utaifa wao na ufahari wao! Ndio maana halisi ya utaifa

Huku kwetu Simba wakati mwingine anapigwa vita, mpinzani anasaidiwa kupewa nguvu, lakini tunasahau hizi ni mechi za Afrika kwa ajili ya kuweka ramani, ile agenda ya VISIT TANZANIA ni kwa ajili ya hospital kule Longido, Shule kule Morogoro na madaraja kule Tukuyu

Sio suala la Simba ni suala la taifa, chuki ni mzigo mkubwa usiubebe! Please dont!

VISIT MOROGORO

Ameandika Farhanjr

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Utopolo vile wanaangalia kapombe akiwajibika
FB_IMG_16502712881933212.jpg


Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Mshabiki ambaye alitamani timu yake ifunge magoli mengi zaidi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ugenini unasemaje ni kubeza?..Watu hawabezi bali wanatamani endapo simba ingekua na mlima rahisi wakupanda ugenini.
 
Kwaiyo na nyie kesi itaisha kwa stahili iyo sio, kwa timu ya aina gani mliyonayo na kocha wa aina gani atakaewawezesha kuvuka kwa staili iyo? Ebu tuambie matokeo yenu ya mechi za ugenini ili tupate picha angalau ya kuwapa asilimia za kuvuka hatua inayofata
Pole kwa maumivu makali uliyopata.
nakushauri tumia muda wako mwingi kupumzika,hakikisha unapata hewa ya kutosha,kula kwa wakati,fanya mazoezi kiasi,,hii itakusaidia kupata nafuu ya madhara ya pumzi ya moto kutoka kwa mnyama Simba uliyovuta siku ya jana.
 
Kwaiyo na nyie kesi itaisha kwa stahili iyo sio, kwa timu ya aina gani mliyonayo na kocha wa aina gani atakaewawezesha kuvuka kwa staili iyo? Ebu tuambie matokeo yenu ya mechi za ugenini ili tupate picha angalau ya kuwapa asilimia za kuvuka hatua inayofata
As vita 0 , simba 1
Galaxy 0 , simba 2
Plateu 0 , simba 1
Swallows 0 , simba 4
Au unataka mechi zipi za ugenini?
 
Kwa wasomali alifunga mangapi? Kwa Zanaco siku yenu ya mwananchi alifunga mangapi? Au hizo mechi zote hakucheza? Kwa taarifa yako , mayele anafunga kwenye mechi ambazo mazingira yameshaandaliwa na giesiem ili ateteme kuwafurahisha misukule wa utopoloni. Mechi ambazo hazijaandaliwa mazingira , mayele huwa anageuka kuwa kibuda.
Tunazungumzia mechi za kimashindano, sio hizo mechi za kujipima nguvu.
Na hapo ulizungumzia Rivers baadae umeaumua uhamishe magoli.
Baki njia kuu, kuchepuka sio dili.
 
Mshabiki ambaye alitamani timu yake ifunge magoli mengi zaidi ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ugenini unasemaje ni kubeza?..Watu hawabezi bali wanatamani endapo simba ingekua na mlima rahisi wakupanda ugenini.
Sasa utopolo itamtakia simba heri ya kuwa na mlima rahisi wa kupanda?
Tumia akili japo kidogo,hizo ni chuki za hao mazwazwa wa nchi....

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Shida ni sisihatuwezi kucheza vizuri viwanja vya ugenini.. Ni ile timu ya gomez tu ndio tu ilipata droo na ushindi ugenini. Zile 4 kwa kaizer mpaka leo hata sielewi tulikufaje kufaje kwa wale walevi.
Ukitutoa sisi, wenzetu wana nidhamu kubwa mnoo ya ukabaji na game za away wanaweza kucheza, sisi huyu kocha hiyo game ya away ngoja akupangie kikosi hovyo, tunakufa 3 tunarudi kujipanga kwa game ijayo.


Laiti tukiweza kucheza kama mazembe jana, au tukaweza kukaba kama wao orlando basi hata huku kwenye mtoano tutakuwa tunapeta.
Binafsi matumaini ya kutoboa ni madogo mnoo, naweka 25%

Yote 9, hiyo game ya al masry bonge moja la mechi, yaani al masry kashinda 2-1 akiwa na red card 2.
Na ile draw ya juzi mashindano hayo away hujaiona..?
 
Back
Top Bottom