Wanaobeza hatua ya chadema ya juzi, ya kutoka nje ya bunge ni bumbum wa siasa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaobeza hatua ya chadema ya juzi, ya kutoka nje ya bunge ni bumbum wa siasa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Byendangwero, Feb 10, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna baadhi ya watu wanao ibeza CDM kwa uamuzi wake wa juzi, wa kususia hatua za mwisho za mjadala wa kufanyia marekebisho kanuni inayotoa ufafanuzi wa ni nini maana ya kambi rasmi ya upinzani. Kwangu mimi kitendo hicho cha CDM ni ushahidi mwingine unao dhihilisha namna chama hicho kilivyokomaa kisiasa; maana kama kingeliendelea kukaa ndani ya bunge mpaka suala hilo likafikia hatma yake, kusingelikuwapo uhalali wowote wa chama hicho kuendelea kulipinga suala hilo, kwa vile nacho kingelihesabiwa kuwa sehemu ya uamuzi huo. Maadam wakati uamuzi huo unachukuliwa chenyewe hakikuwepo kina kila sababu ya kuendelea kupinga hatua hiyo.
   
 2. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,981
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Hiyo ni sawa kabisa Byendangwero, ila mimi nina swali; hawa CDM kutoka bungeni wakati kikao kinaendelea walivunja kanuni yoyote ya bunge. Je wanachukuliwa hatua gani???????????????
   
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  hakuna kanuni yeyote ya bunge iliyovunjwa na hivyo no displinary action to be taken against the giant party/cdm.
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hakuna kanuni yeyote iliyovunjwa; isipokuwa CDM ilitumia haki zake za kikatiba kuwasilisha ujumbe rasmi kuwa hawezi ikawa sehemu ya maamuzi ambayo msingi wake, ni kulinda maslahi ya watu fulani fulani, kwa gharama ya maslahi mapana zaidi ya umma.
   
 5. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  heko kabisa cdm mbele kwa mbele
   
Loading...