Wanaoandamana kuunga mkono hotuba ya kikwete wanauelewa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaoandamana kuunga mkono hotuba ya kikwete wanauelewa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaa la Moto, Aug 31, 2008.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Tangu hotuba ya JK itolewe, nimekuwa nikisikia kupitia vyombo vya habari kuwa wako watu wanashawishi watu waiunge mkono.
  Lakini mimi kwa sehemu kubwa sikubaliani na mambo mengi aliyosema kikwete maana alipokuwa akitangaza hotuba yake hiyo yenye majisifu mengi nilikuwa katika ziara ya vijijini katika wilaya ya Muleba huko Kagera.
  Nilichoona kwa kweli nilishangaa sana kama kuna sehemu zenye dhiki kiasi hiki. Kwanza sikuwahi kufikiri kwamba kuna sehemu katika nchi hii barabara kwao ni hadithi lakini watu wakiwa wamejaa umasikini usiosemekana. ahaaaaaa ni mambo ya kushanagaza kwamba Tanzania bado kuna hali kama hii huku tukijisifu saaaaaaaaaaaana.
  Bado kuna shule za msingi ambazo zimejengwa kwa nyasi na miti, na zingine hazina viwango kwani zinaweza kuwaangukia wanafunzi wakati wowote.
  Nimekuwa katika shule ambayo wanafuzi wa darasa la 5 na 6 wanakaa chini kama picha nilizounganisha zinavyoonyesha. Je hapa kuna mategemeo ya kupata wana teknolojia na wanasayansi mahili katika karne hizi kweli?
  Kama watoto wetu watasoma katika mazingira haya nakwambia hakuna lolote la kutegemea labda kama watoto wa mafisadi peke yao wataendelea kutawala na kutuibia kama baba zao.
  Baadhi ya vijiji wanatembea kilometa 40 kufuata huduma za afya wakati maji salama ni hadithi maana wananyang'anyana na mifugo kama ng'ombe.
  Sasa sijui wanaandamana kumdanganya nani?
  Tunataka kuwaangalia wote wanaoshawishi watu kuandamana hasa mijini na tunataka tuone kama si hao mafisadi na ndugu zao wanaofahidi pesa zetu za wizi alizowasamehe wasilipe.
  Tukatae upuuzi huu wa kuandamana kuunga mkono maneno yasiyokuwa na maana.
  Viongozi wa upinzani mko wapi? wakiandamana sisiemu leo nyie nanyi anzisheni ya kwenu kesho. Watu wanadanganywa kweli.
  Mungu isaidie Tanzania itoke kwenye dimbwi la viongozi waongo na walaghai. Maana wewe ushindwi na lolote.
  Shule ya Msingi.jpg
  Darasa la 5.jpg
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Picha hizi zimepigwa wiki hii hii kwa maana hii ndio hali halisi
   
 3. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Wajinga sana wanaounga mkono maandamano hayo wakati maisha yao ni duni sana. Hawana vision kwa kweli.
   
 4. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mwehu wa kukubali kila aambiwacho akiambiwa nenda kalete bakuli lililoko kwenye shimo la taka tupakulie chakula cha wote, hakatai, hukimbia mara,huku nyuma wenye akili wakila, na kumsanifu!
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Haya sasa angalia na darasa la shule hii. Kweli hapo tuna haki ya kujisifu?
  Si ni kama tumepigwa changa la macho?

  Darasa.jpg
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Sasa fikiri jinsi mbunge wao anavyojisifia kwamba serikali imeleta maendeleo makubwa sana jimboni mwake.
  Na mbunge huyu huwa hakosi kujisifu sana na kuisifu serikali.
  Na ni huyu huyu alianza kujaribu kumtetea hata EL alipopewa kashfa ya Richmond bungeni.
  Siku zote ni wa kwanza ku supoort 100 kwa 100 budget na hotuba fake zote.
  Tutafika?
   
 7. M

  MiratKad JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 294
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kutoa wito, ambao umeambatana na picha zinazoenda mbali kuelezea ufukara wa wananchi wa kawaida. Sasa wakati CCM wanaandamana ni lazima tutumie nafasi hiyohiyo pia kusambaza vijarida vyenye picha kama hizi na maelezo yake. Nakusisitiza kuwa umasikini kama huu ungeshapunguzwa endapo haya mafisadi yasingekuwa madarakani na kuiba na kujilimbikizia mali.

  Hii ni kazi rahisi tu, kila mmoja wetu myenye nia anaweza kufanya.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hawajui walitendalo, ni Tshirt za bure na Shs 2000 ni rahisi sana kupata cheap popularity Tanzania.
   
 9. D

  Darwin JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hizi picha kamwe hutaziona kwenye blog ya Michuzi
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hahahhah mzee umenena!! Mshikaji anafukuzia kuwa mpiga picha wa raisi ama wa IKULU aweke hizi amwagie kitumbua mchanga?
   
 11. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  heheh dats a true sign kuwa huko bongo maisha ni magumu wajimini..cz m sure even ukitake mmojawapo ya wanaoandamana na ukawauliza wanaandamania nini na umuulize anything abt the hotuba waweza kuta hata kuijua hawaijui kabsaa!its jus a matter ya kupewa kifuta jasho kidogo nao wanado wat they are told to do!na kufuata mkumbo tu
   
 12. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #12
  Aug 31, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280

  ...vipi ..kwani kaka michu mmemuona mtu wa kikwete sana au...mbona ana picha zipo balanced tu pamoja na kuwa mara nyingi jk humpa shavu kwenye ziara zake???
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Na hii ni ofisi ya kijiji cha nchi inayojisifia kukua uchumi na maendeleo mengi kabisa katika kila nyanja. jamani watanzania kweli tunaandamana tukijua nini kinaendelea huko vijijini? Au twataka tupete 2010 tu huku hakuna maisha bora yaliyokuwapo?:mad:
  ofisi.jpg
   
 14. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #14
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,329
  Trophy Points: 280
  MTAALAM wa sheria za jinai nchini, amesema kitendo cha washauri wa sheria wa Rais Jakaya Kikwete katika sakata la EPA, kutomshauri kuwa kitendo cha kuwaongezea muda watuhumiwa wa kashfa hiyo ili warejeshe fedha walizoiba ni batili kisheria na kimemfedhedha kwani kimemfanya Rais atumie dhana ya kisheria ambayo haipo duniani kote.

  Mtaalamu huyo, Profesa Abdallah Safari alitoa kauli hiyo Dar es Salaam juzi alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusiana na hatua ya Rais Kikwete kama zimefuata taratibu za sheria za jinai au la.

  Prof. Safari alisema amesikitishwa na kufedheheshwa sana na hatua hizo za Rais ambazo zimevunja katiba na sheria zinazoendesha mashitaka ya jina nchini na ameumia zaidi alipobaini miongoni mwa wajumbe wa Kamati iliyomshauri Rais wamo wanafunzi wake wawili.

  Profesa Safari alionesha kukerwa na wasomi wenzake hao wa sheria hasa Inspekta Jenerali wa Polisi, Bw. Said Mwema na Dkt. Hosea ambao alisema, kwa kumbukumbu zake, aliwafundisha sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pamoja na fani nyingine, Profesa Safari hufundisha sheria za jinai, ushahidi na mwenendo wa makosa ya jinai.

  "Hawa wote (Hosea na Mwema) walikuwa wanafunzi wangu Chuo Kikuu, sikuwafundisha hivyo...wameniaibisha," alisema.
  Akifafanua makosa aliyoyafanya Rais Kikwete kutokana na ushauri huo, Prof. alisema sheria za jinai ziko wazi-mtu ambaye amejipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, aliyeiba na yule aliyemsaidia kuipata wote wana makosa ya jinai, hivyo wanatakiwa washitakiwe mahakamani.

  Mbali ya muda kuongezwa kwa walioiba fedha hizo, Prof. Safari alishangazwa kusikia Rais akisema wafanyakazi wa BoT waliohusika kusaidia wizi huo wa mabilioni ya fedha, wanashughulikiwa na Bodi ya Wakurugenzi kinidhamu.

  Alisema wafanyakazi hao kama ilivyo kwa wale waliochota fedha za EPA nao wanatakiwa kufikishwa mahakamani kwani walifanya kosa la jinai la kusaidia kutendeka kwa kosa la wizi.

  Alimkosoa pia Rais Kikwete aliyewapa muda watuhumiwa warejeshe fedha hizo na wakishindwa ndipo wafikishwe kortini, akisema huo ni uvunjifu mwingine wa sheria kwa Rais kuingilia kazi za Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

  " Rais amevunja sheria, kosa la wizi adhabu yake ni kifungo si kurejesha kilichoibwa na pia chombo pekee chenye mamlaka ya kutoa uamuzi ni Mahakama si Rais...Mbona anamuingilia DPP?" alihoji.

  Prof. Safari alisema amewahi kuwa wakili wa Serikali kwa miaka mingi, lakini hata siku moja katika utumishi wake wa umma hakuwahi kuona mtu aliyetenda kosa la jinai anaambiwa arudishe fedha alizoiba tena hata kabla hajafikishwa mahakamani.

  Aliongeza kuwa pia katika uamuzi huo wa Rais kuna hoja ya kikatiba kwani katiba ya nchi inatamka bayana kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria, akahoji: "Iweje Rais anazuia hawa wasifikishwe mahakamani wakati kuna wananchi wengi wanaburutwa kortini kila kukicha na hazuii?"

  Aliongeza kuwa hata amri ya Rais kuwa mali za watuhumiwa wa EPA zikamatwe ni kinyumne cha sheria kama hakupata kwanza amri ya mahakama.

  Profesa Safari anasifika kwa utaalamu wake katika si tu sheria za jinai na ushahidi nchini bali pia umanju wake katika lugha adhimu ya Kiswahili na ameshatoa machapisho kadhaa ya kisheria katika lugha hiyo kikiwemo kitabu mashuhuri kiitwacho 'Mashitaka ya Jinai na Utetezi,' kinachosomwa na wanafunzi na wadau wengine wa sheria nchini.

  Amewahi pia kuwa wakili wa kujitegemea aliyeazimwa na Serikali ili kuendesha kesi ya rushwa dhidi ya aliyekuwa mfanyabiashara mashuhuri jijini Dar es Salaam, Bw. Mohammed Rafiq, maarufu Baghdad, ambaye alikutwa na hatia na kufungwa.

  source: gazeti la majira 31.08.2008
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ainiingii akilini kila nikijua wapo watu wengi magerezani wamefungwa sababu ya wizi na wapo wezi dhahiri wameachwa eti kwa maelekezo ya raisi.
  Sasa kwa nini nisiamini JK alikuwa ni mmojakati ya wafaidika wa pesa ya EPA?
  Je Prof. Safari hawezi kusaidia kufanya private prossecution dhidi ya wahusika wa wizi huo? Au ni kinyume na sheria za nchi yetu?
  Ina maana mtu unaweza kuiba kwa ruhusa ya Raisi na ukaachwa upete tu na hakuna namna nyingine yoyote mahakama inaweza kuingilia kati ikamtia mtu wa aina hiyo hatiani?
  Naomba nielezwe maana hili ni la kisheria.
  Fikiri shida walizo nazo watanzania na Kiongozi wa nchi anahutubia taifa huku wenye shida wakimsikia hapo tusemeje?
  Pesa yao wamekula kwa visingizio kibao na wao bado wanakejeliwa kwa hotuba mbofu na maandamano uchwara haya.
   
 16. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2008
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..kuna watu hawana kazi za kufanya tanganyika!
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hakika umesema kweli. Chukua 5 zangu
   
 18. D

  Darwin JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tuonyeshe hizo picha ziko wapi? na kama ni kaka yako mwambie aamue kwa wiki moja tu kuzionyesha kwenye blog yake kama hajapewa onyo.

  Mambo yetu mabaya mpaka mzungu wa nchi za nje atakapoyaandika au kuyaonyesha hadharani. [Darwin nightmare] hata wabunge walikasirika kuona filamu ile, hali halisi!
  Kilichobakia ni sisi wazalendo tuyafichue mabaya wenyewe ili wengine tuyaone, sio Michuzi kupamba picha ambazo zitawafurahisha watoto wa mafisadi walioko Ulaya na marekani
  [​IMG]

  Niambie kama mwanafunzi anayesoma hapo kwenye hilo banda hata la kuku lina nafuu umuambie amchague mkoloni au nchi iliyopata uhuru ma miaka na bado anaadhilika kama hivi[​IMG]

  Hapa utasema bora ukoloni
   
 19. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Nadhani anayepinga kuunga mkono Hotuba ya Rais Kikwete ni mbumbumbu.Haelewi lolote kuhusiana na maendeleo ya Tanzania.kama hamna la kuzuungumza la maana ni bora ukae kimya.Kila rais wa nchi ametoa mchango wake katika maendeleo ya nchi hii hao wanaoona haja fanya lolote ni haayawani.
   
 20. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  .Inaelekea hujui mfumo mzima wa ujenzui wa shule hizi za msingi.ni vyema ukajielimisha kabla ya kulaumu.maana Ni ujinga kulaumu bila kufahamu.Mfumo au utaratibu wa ujenzi wa shule hizo.Wakulaumu ni wanakijiji wenyewe,DiwaniNK
   
Loading...