Wanao fanya kazi ya Umalaya Afrika wana HIV nyingi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanao fanya kazi ya Umalaya Afrika wana HIV nyingi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Simba Mkali, Mar 21, 2012.

 1. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 592
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Duu! Hiii inatsisha sana

  MALAYA WA AFRIKA WANAONGOZA KWA HIV
  NAIROBI, KENYA


  WANAWAKE wa naofanya kazi ya umalaya katika nchi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara, imebainika kuwa, wanaongoza duniani kwa maambuzikizi ya virusi vya HIV.
  Pamoja na matokeo hayo utafiti umeonesha kwamba umalaya uruhusiwe kisheria ili kusaidia mazingira yao ya kufanya kazi yaboreshwe na hivyo kuchangia kupunuza maambukizi ya HIV.
  Utafiti huo uliotolewa Alhamisi iliyopita ulifadhiliwa na Benki ya Dunia na Umoja wa Mataifa na ulifanywa na taasisi ya Afya ya John Hopkins yenye makao yake Marekeni.
  Malaya wapatao 100,000 walichukuliwa kiholela kutoka nchi 50 za Afrika,, Asia, Ulaya Mashariki, Amerika Kusini, Caribbean na Mashariki ya Kati.
  Watafiti walibaini kwamba kati ya malaya wote kutoka nchi hizo 50, wale wa kutoka nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara ndio waliokuwa na kiwango cha juu cha maambukizi hayo.
  Utafiti ulifanywa kati ya Januari 1, 2007 na Juni 25, 2011, malaya waliogunduliwa kuwa na viwango vya juu ni wa Kenya wakifuatiwa na Uganda, Madagascar, Afrika Kusini, Malawi na Zimbabwe.
  Katika Afrika, malaya wapatao 7,000 waliteuliwa kutoka Kenya huku kutoka Senegal walikuwa 1,656.
  Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na Halimashauri ya Nairobi kuna malaya wapatao 7,000 ambao uhudumia wateja watatu au wanne kwa siku
  Matokeo hayo yalichapishwa katika Jarida liitwalo The Lancet, ukubwa wa kiwango hicho hautoi picha nzuri kwa nchi zetu zilizpo Afrika Mashariki kwa Ujumla.... Unasemaje?
   
 2. Achahasira

  Achahasira JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ushoga kwanza,sahv umalaya ,,,,, kesho tujiue kisa tupo wengi duniani.
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kumbe dawa ya kuzuia maambukizi ya Ukimwi ni kuruhusu Umalaya?
   
Loading...