Wanangu wanaona ni bora wapate pesa za matanuzi na starehe kuliko kuwafanyia maendeleo

Mchimwachimego

JF-Expert Member
Jun 15, 2020
358
271
Historia yangu na wanangu ni ya kusikitisha, kufurahisha, inatia huruma na kushangaza. Mwaka 2015 niliwaita wanangu wanieleze wanakerwa na jambo gani ambalo mimi baba yao silisimamii vyema, wengi zaidi 80% walisema hawapendendezwi na udhaifu wangu katika kusimamia shamba na walieleza mengi sana baadhi ya hayo yalikuwa kuwa shamba linatumiwa vibaya na baadhi yao, wapo wanaouza mazao bila kushirikisha wengine, wapo wanakata miti na kuuza,wapo wanaolima bhangi na kuvuta,wapo wanaochimbisha mchanga na kuuza, wapo wanaouza mifugo hovyo, wapo wanaofanya shamba njia ya wahuni, NK.

Baada tafakari ya muda nikawauliza kuwa lakini hayo yote si mnayafanya ninyi wenyewe miongoni mwenu na mnapata pesa na mnafurahia maisha ya starehe, wakajibu ni sawa lakini baba mambo haya hayawezi kuwa na faida za muda mrefu ni bora ukomeshe na uwe mkali ili hizi mali zitunufaishe wote.

Baada ya miaka mitano watoto wangu wamekuwa kama nyati aliyejeruiwa maana wanalalamika kwamba eti hapo zamani wakati shamba lilikuwa chini ya bibi walikuwa wanapata sana pesa za matanuzi na starehe tena bila kazi ngumu lakini tokea bibi yao amefariki na kunipa mimi usimamizi na uthibiti wamekuwa ombaomba wakati mali ipo pia wanalalamika kuwa nawajengea ukuta kuzunguka shamba na ninawajengea nyumba shambani, shule, mabwawa, vyote hivyo vya nini wakati pesa hawana wanasema.

Ni bora wapate pesa za matanuzi na starehe kuliko kuwafanyia maendeleo. Nimewauliza vipi mbona mmebadilika wakati ninyi mlisema kuwa nisimamie matumizi mabaya ya shamba ili mnufaike wote au mlidhani kuwa nikithibiti pesa itakuwa kama zamani?

Wakasema kabisa kumbe ukidhibiti uhalifu na pesa inapotea tulikuwa hatujui bora turudi tulikotoka hata kama shamba likiisha watoto wetu watajijua kivyao, sisi tunataka uhuru wa manyani yaani kila kitu ruksa hata tukiangamia au tukiishiwa sawa tu! walikuwa wanaongea huku wakiwa wanapiga kelele.

Sasa ndugu zangu, nimeona niwasimulie ili mnisaidie maana kuna mtoto mmoja yeye anaoneka yuko tofauti na wengine amenidokeza kuwa wamepanga waniue ili shamba walitumie wanavyotaka bila kubughudhiwa, sasa nawauliza wanajamvi wenzangu niwaachie ili wasiniue au nipambane nao ili kulitunza kwa ajili ya vizazi vyao baadaye nao walikute Shamba.

Asanteni.
 
Ngoja niulizie ushauri kwa middle men wa kule yani kuleee mbaliii naweza nikakupatia na ww utakusaidia huo ushauri mi hayo nilishawahi kushuhudia kwa jicho moja kule mashariki ya kule namaanisha kule yani mashariki ukooo,ngoja nitakupa kizuri cha kukupa
 
Naona umezungumza machache tu, toka 2015 umekuwa na kawaida ya kutusingizia watoto mambo ambayo hatujafanya na kutufunga eti tunahujumu shamba.

Kuna wenzetu wanaopotea na tukikutaka ufanye uchunguzi unakaa kimya.

Kulikuwa na karani ambaye kazi yake kubwa ni kuhakiki mavuno na matumizi yatokanayo na mapato, akagundua kwamba kuna 1.5t haijulikani ilikoenda, ukamfukuza kazi kazi kwa vitisho.

Kwa miaka yote mitano ulisema ni wewe tu unayetakiwa kuzungumzia hali ya shamba, sisi tukizungumza tunapigwa.

Tumeendelea kupokea kile kile tulichokuwa tunapokea kwa kipindi chote, huku bei za vitu zikipanda na wakati tunazalisha sana, tena shamba letu limesifiwa kwa kuingia kwenye mashamba yenye uchumi mzuri.

Halafu umekuwa na tabia ya kununua vitu bila kutushirikisha, na tukiuliza bei unatukaripia.

Bila kusahau wale wenzetu uliowafukuza shambani eti hawana vigezo, ukaamua kwamba hata viinua mgongo vyao wasipate.

Waambie pia kuhusu kutuzuia tusipate malimbikizo ya viinua mgongo mapema eti mpaka tuzeeke, huku wewe na rafiki zako mnachukua kila baada ya miaka 5.

Tumechoka.
 
Bora ufe tu kwakweli!!..

Yaani mimi ni wakukosa" sh: 400 ya kush!!! A k A Dawa kwel!!!!! Daaa

Imbombo ngafuu/ hali ngumu:
 
Historia yangu na wanangu ni ya kusikitisha, kufuraisha, inatia huruma na ni yakushangaza. Mwaka 2015 niliwaita wanangu wanieleze wanakelwa na jambo gani ambalo mimi baba yao silisimamii vyema, wengi zaidi 80% walisema hawapendendezwi na udhaifu wangu katika kusimamia shamba na walieleza mengi sana baadhi ya hayo yalikuwa kuwa shamba linatumiwa vibaya na baadhi yao, wapo wanaouza mazao bila kushirikisha wengine,wapo wanakata miti na kuuza,wapo wanaolima bhangi na kuvuta,wapo wanaochimbisha mchanga na kuuza, wapo wanaouza mifugo hovyo, wapo wanaofanya shamba njia ya wahuni, NK.

Baada tafakali ya muda nikawauliza kuwa lakini hayo yote si mnayafanya ninyi wenyewe miongoni mwenu na mnapata pesa na mnafurahia maisha ya starehe, wakajibu ni sawa lakini baba mambo haya hayawezi kuwa na faida za muda mrefu ni bora ukomeshe na uwe mkali ili hizi mali zitunufaishe wote.

Baada ya miaka mitano watoto wangu wamekuwa kama nyati aliyejeruiwa maana wanalalamika kwamba eti hapo zamani wakati shamba lilikuwa chini ya bibi walikuwa wanapata sana pesa za matanuzi na starehe tena bila kazi ngumu lakini tokea bibi yao amefariki na kunipa mimi usimamizi na uthibiti wamekuwa ombaomba wakati mali ipo pia wanalalamika kuwa nawajengea ukuta kuzunguka shamba na ninawajengea nyumba shambani, shule, mabwawa, vyote hivyo vya nini wakati pesa hawana wanasema.

Ni bora wapate pesa za matanuzi na starehe kuliko kuwafanyia maendeleo. Nimewauliza vipi mbona mumebadilika wakati ninyi mlisema kuwa nisimamie matumizi mabaya ya shamba ili mnufaike wote au mlidhani kuwa nikithibiti pesa itakuwa kama zamani?

Wakasema kabisa kumbe ukidhibiti uharifu na pesa inapotea tulikuwa hatujui bora turudi tulikotoka hata kama shamba likiisha watoto wetu watajijua kivyao, sisi tunataka uhuru wa manyani yaani kila kitu ruksa hata tukiangamia au tukiishiwa sawa tu! walikuwa wanaongea huku wakiwa wanapiga kelele.

Sasa ndugu zangu, nimeona niwasimulie ili mnisaidie maana kuna mtoto mmoja yeye anaoneka yuko tofauti na wengine amenidokeza kuwa wamepanga waniue ili shamba walitumie wanavyotaka bila kubughudhiwa, sasa nawaulinza wanajamvi wenzangu niwaachie ili wasiniue au nipambane nao ili kulitunza kwa ajili ya vizazi vyao baadaye nao walikute Shamba.

Asanteni.
Waachie Karima wewe Anza maisha upya.
 
Baba ndio umeamua kuja kututangaza huku JF ? Au kwakua ni wavuta bangi unadhani hatupo huku?
 
Back
Top Bottom