Wanane warudisha fomu Sioi ashindwa kujieleza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanane warudisha fomu Sioi ashindwa kujieleza

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by EasyFit, Mar 9, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wagombea wanane wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki jana waliteuliwa kuwakilisha vyama vyao. Wagombea hao ni Siyoi Sumari (CCM), Joshua Nassari (Chadema), Shabani Kirita (SAU), Mohamedy Mohamed (DP), Abrahamu Chipaka (TLP), Charles Msuya (UPDP), Hamisi Kihemi (NRA) na Abdalah Mazengo (AFP).

  Siyoi alirudisha fomu kwa kushuka kwenye gari nje ya Halmashauri na kutembea kwa miguu umbali wa meta 200 hadi ofisi ya Msimamizi.

  Mgombea wa CCM Sioi alipopewa nafasi ya kujieleza, alimwomba Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Arumeru, Joseph ole Saivoiye azungumze kwa niaba yake.

  Mwenyekiti huyo alisema watafanya kampeni za kistaarabu na si kuchafuana, kwani watu wanajua CCM ni ya amani na utulivu.

  Naye mgombea wa Chadema, Nassari alisindikizwa na pikipiki na magari yenye bendera za chama chao na kusababisha wafanyakazi wa Halmashauri kutoka ofisini kushuhudia.

  Naye alisema chama hicho kitafanya kampeni za amani na utulivu kipindi chote cha kampeni na kuahidi kuwa hatapanda jukwaani kutoa lugha za matusi wala kumchafua mtu yeyote.

  Alisema katika kampeni hizo, atajikita kueleza sera za Chadema na jinsi ya kutatua matatizo ya Arumeru Mashariki, ili wananchi wanufaike na rasilimali walizojaaliwa jimboni hapo.

  Aliomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mecy Silla na Polisi, kutenda haki kwa kusimamia sheria bila upendeleo kwa chama chochote.

  Alisema watu wanataka Arumeru apatikane mtu anayestahili na aliyekubalika na kupewa kura na si chama gani kipitishwe au mgombea wanayemtaka wao

  Meneja wa Kampeni wa Chadema, Vincent Nyerere, alisema tayari chama kimejipanga kuzindua kampeni kesho.

  Katika uzinduzi huo, alisema kutakuwa na pikipiki, magari, baiskeli na helikopta ambayo itazunguka eneo la maandamano ya chama hicho yatakayotokea KIA na Arusha Mjini na kukutana Usa River watakaofanya uzinduzi huo.

  Kwa niaba ya CCM, Saivoiye alisema watazindua Jumatatu.

  Source: Habari leo
   
Loading...