Wanandoa waliokamatwa kwa kuongea uongo kuhusu Corona wafikishwa mahakamani, waachiwa kwa dhamana

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wanandoa wakazi wa Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kutoa lugha hatarishi kwa lengo kupotosha jamii kuhusu ugonjwa wa Corona.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mkunde Mshanga akisaidiana na Wankyo Simon amesema kuwa kuwa Machi 20 mwaka huu Boniphace Mwita (49) na mke wake Rosemary Jenera (41) washtakiwa hao wakiwa kwenye daladala pamoja na abiria wengine, walitoa matamshi hatarishi kwa nia ya kupotosha umma wa Watanzania yanayosema “Ugonjwa wa Corona serikali inadanganya hakuna ugonjwa wowote na imefunga mashule kwa kuwa haina hela na ada za kusomesha watoto bure.”

Jamhuri imeiambia mahakama kuwa matamshi hayo yangeweza kuleta hofu au hisia mbaya dhidi ya nchi yao ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wameachiwa kwa dhamana.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na itakuja tena Mei 6 mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Chanzo: TBC
IMG_20200422_194540.jpg

Pia Soma: Jeshi la Polisi Dar es Salaam linawashikilia mume na mkewe kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kuhusu ugonjwa wa COVID 19 (CORONA) - JamiiForums
 
sedition... kwenye judiciary ambayo siyo compromised, wanashinda ila kwa hapa wajiandae kwa lolote!

Sedition is about when a person's speech,behaviour,language,written words attracts the group of people or a mob acts rebellion against authority of state or create incitement to public disorder or violence.

In the Maneka Gandhi vs Union of India, the court unambiguously held that critcising and drawing general opinions against government policies and decisions within a reasonable limit that doesn't incite people to rebel is consistent with freedom of speech and expression.
 
Hilo Ni kosa...sio kila kitu kuongea kwa kua una Uhuru.....ila wanaweza pigwa faini au jela mwaka mmoja Kama kutakua na ushahidi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom