Wanandoa wafariki kwa kuning’inia

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Wanandoa wafariki kwa kuning’inia Send to a friend Wednesday, 29 September 2010 08:40 0diggsdigg

Joyce Joliga, Songea

WATU wawili ambao ni mume na mke wamekutwa wakiwa wamefariki kwa kuning’nia juu ya mti uliopo kwenye shamba la mikorosho wilayani Tunduru bila kuacha ujumbe wowote.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 1:30 katika kijiji cha Liwangula wilayani humo.

Alisema marehemu hao ambao ni mume na mkewe walikutwa wakionekana kama waliojinyonga katika shamba la mikorosho la baba wa mwanaume ambaye amejulikana kwa jina la Mzee Mtepere Omary (66).

Kamanda aliwataja watu hao kuwa ni Hamis Said (30) pamoja na Fatuma Kaupwe (25) ambao inadaiwa kuwa kabla ya kujinyoonga walionekana wakiwa na furaha na walienda kumtembelea mzazi wao huyo .

Alisema, siku ya tukio watu hao walimwaga mzee Omary kuwa wanaenda kwenye sherehe ya harusi na watalala huko huko.

Mzee huyo naye alikwenda kwenye sherehe hiyo na kwamba alipofika hakuwaona na hakuwa na wasiwasi akiamini watafika baada ya muda mfupi.

Kamanda alisema siku hiyo, wanandoa wote wawili hawakurudi nyumba, lakini siku iliyofuata mzee huyo alienda shambani na kukuta wanawe wakininginia na tayari walikuwa wameshajinyonga hivyo aliwaita majirani na kwenda kutoa taarifa polisi.

Kamuhanda alisema polisi wanaendelea kuchunguza chanzo cha watu hao kujinyonga na kwamba taarifa za awali za uchunguzi uliofanywa na daktari umeonyesha walijinyonga.
 
Sidhani kama wote wawili wanaweza kujinyonga kwa pamoja! Ila yawezekana wameuawa kisha wakaning'inizwa... Polisi wachunguze...
 
Sidhani kama wote wawili wanaweza kujinyonga kwa pamoja! Ila yawezekana wameuawa kisha wakaning'inizwa... Polisi wachunguze...


jeshi ra porisi tumee hiyooooooooo tupeni kazi jamani kwenye haya matume yenu sio kujigawia wenyewe urajiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom