Wanandoa wafariki dunia kwa kudaiwa kunywa chai yenye sumu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,598
2,000
Lushoto, Tanga. Watu wawili ambao ni mtu na mkewe wamefariki dunia wakati wakipata matibabu kwenye zahanati baaada ya kunywa chai inayohofiwa kuwa ilikuwa na sumu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amezungumza na wanahabari leo na kuthibitisha kuwa wanandoa hao wamepoteza maisha baada ya kunywa chai hiyo.

“Walikunywa chai hiyo jana saa 7.00 mchana katika Kijiji cha Baga, Tarafa ya Mgwashi wilayani hapa,” amesema.

Amesema majirani wa wanandoa hao walishtuka baada ya kuona muda unakwenda bila jirani zao hao kutoka nje ndipo walipoingia na kukuta wamelala huku wakiwa hawajitambui ndipo wakawakimbiza katika zahanati ya Baga.

Kamanda Wakulyamba amewataja waliokufa katika tukio hilo kuwa ni Rajab Ali Rajab (72) na mkewe Amina Rajabu (62) huku mpwa wao Adamu Said(12) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mashine akinusurika.

Amesema Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kujua chanzo cha kifo hicho ingawa taarifa za awali kutokana uchunguzi wa daktari unaonyesha walikunywa chai inayodhaniwa kuwa na sumu.

“Tunachunguza kujua kama sumu hiyo ilitoka wapi na waliwekewa na nani na kwa sababu zipi hatimaye ili kujiridhisha na kama litakuwa tukio lakuwekewa sumu hiyo tutahakikisha tunawakamata walioshiri.” amesema Wakulyamba.
 

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,241
2,000
WATU wawili wa familia moja, mke na mume wakazi wa Kijiji cha Baga. Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, wamefariki dunia baada ya kunywa chai ya rangi inayodhaniwa kuwa na sumu.


Mbali ya hilo, mpwa wao amenusurika katika tukio hilo ambalo limeacha maswali mengi.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, alithibitisha kutokea tukio hilo.


Alisema lilitokea Juni 19, mwaka huu saa saba mchana wakati familia hiyo ilipoandaa kinywaji hicho.


Aliwataja waliofariki wakati wakipatiwa matibabu katika Zahanati ya Baga kuwa ni Rajabu Ally (73) na Amina Rajabu (62).


Kamanda Wakulyamba alisema katika tukio hilo, mpwa wao Adam Saidi (12), mwanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Mashine, alinusurika kifo.


Alisema miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi wa awali na kukabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi, huku Jeshi la Polisi likiendelea na upelelezi wa tukio hilo.


“Katika tukio hilo ambalo limepoteza watu wa familia moja, mpwa wao alinusurika baada ya kunywa chai idhaniwayo kuwa ni yenye sumu, tunaendelea na upelelezi wa tukio hili,” alisema Kamanda Wakulyamba.


Chanzo: Mtanzania
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom