Wanandoa wafanye nini wanapokabiliwa na mgogoro wa kiuchumi.............? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanandoa wafanye nini wanapokabiliwa na mgogoro wa kiuchumi.............?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Mar 29, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ndio, inaweza kutokea wanandoa mkajikuta mna wakati mgumu kifedha. Kama mnavyojua kwamba hali ya uchumi imebadilika na maisha yamekuwa magumu sana, inaweza ikawa imesababishwa na kuyumba kwa biashara zenu, au mmoja wa wanandoa kufukuzwa kazi au labda tu niseme kwa kifupi kuwa familia imekumbwa na mgogoro wa kiuchumi.

  Je ninyi kama wanandoa mnafanya nini ili kuondokana na jinamizi hilo la mgogoro wa kiuchumi?

  Hapa chini nitajaribu kuainisha hatua tano za kuchukua:

  1. Kuwa na matumaini- hata kama hali ni ngumu kiasi gani, kuwa na matumaini ni hatua muhimu sana itakayowawezesha wanandoa kuondokana na msongo wa mawazo. Kuwa na hali ngumu hakumaanishi kwamba ndio mwisho wa maisha na kuwa na matuamaini ni moja ya nguzo muhimu zitakawafanya mfikiri vizuri ili kuondokana na hali hiyo

  2.
  Umoja ni nguvu- Kuna usemi usemao umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, msemo huu una maana pana sana, maisha yetu kwa kiasi kikubwa yanategemea ushirikiano ili kufikia malengo yetu, iwe ni huko makazini kwetu, katika biashara zetu na hata katika ndoa zetu, tunahitaji sana kushirikiana ili kumudu kufikia malengo yetu. Kama wanandoa wanakumbwa na hali ngumu kiuchumi halafu kila mmoja akawa anajali maisha yake itawachukua karne kuondokana na hali hiyo au ndoa hiyo inaweza kukumbwa na mgogoro mkubwa na hata kuvunjika.

  3.
  Matumizi- Usisubiri mpaka hali iwe mbaya sana kiuchumi ndiyo mchukue maamuzi magumu ya kuachana na matumizi yasiyo ya lazima. Inatakiwa matumizi yasiyo ya lazima yasitishwe mara moja. Manunuzi ya vipodozi ghali kwa wanawake, simu za gharama au kamera kwa wanaume zisubiri kwanza hali ya uchumi itengemae. Kumbukeni kujiuliza kabla ya manunuzi kama ni muhimu kununua bidhaa hiyo kwa wakati huo au inaweza kusubiri. Ni vyema wote mkajadili kwa kuangalia faida na hasara za kununua bidhaa hiyo.

  4.
  Kuomba msaada-Msione aibu kuomba msaada pale inapobidi, kwa mfano wazazi au marafiki wa karibu ni vyema ukawashirikisha katika masaibu uliyo nayo, wanaweza kuwa msaada mkubwa kwenu na sio lazima uwe msaada wa fedha bali pia hata wa mawazo.

  5.
  Madeni-kama mnadaiwa ni vyema kuwajulisha wadeni wenu hali yenu kifedha ilivyo kabla ya tarehe mliyoahidi kulipa haijafika. Hiyo itakusaidia kuwajengea uaminifu kwao na huenda wengine wakawasaidia kuondokana na jinamizi hilo la ukata.

  Kama mkikubaliana kama familia kufuata hizo hatua tano, basi mnaweza kuondokana na jakamoyo na maisha mkayaona ya kawaida.
   
 2. M

  MBULI YAPI Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ushauri mzuri unaofaa kuzingatiwa na wanandoa wote
   
 3. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  I will keep that in mind -thx bro! Ni mara chache sana utapata ushauri kama huu....
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  Asante
   
 5. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hakuna lolote kama Mungu kakuandikia yes, ni yes tu...Hata kama utatumia mshahara wako wote, utaona zingine zinajitokeza kutoka kwa wazazi wako, ndugu zako, marafiki zako ni bahati tu.

  Unaweza ukabana wewe usitumie pesa zako ukafaa njaa bure, au ukabaana wee ukajinyima kesho yake unakufa... wanachukua ndugu zako urithi :cool2:
   
 6. Ndetirima

  Ndetirima JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 60
  Asante kwa Darasa la bure kabisa Mtambuzi, hii maneno ikifanyiwa kazi jamii itajikwamua sio tu wakati wa shida hata wakati wa raha ili kujiendeleza haya mambo ni muhimu kuzingatiwa.
   
 7. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Thanx. Mada imetulia.
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Umenichekesha sana mkuu....................................
   
 9. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Asante kwa kutukumbusha.

  Mkuu unatuchapa dose mapaka inazidimaana bado tulikuwa kule kwenye kichapo kwa mke hatumaliza umekuja na hii.

  Thanks
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Baada ya kusoma maoni ya wanaume wengi jana kwenye ule uzi wa wanaume kuwashikisha adabu wake zao kwa kichapo lau kidogo, nimegundua vichapo kwa wake zao vinarindima zaidi inapotokea familia kukumbwa na mgogoro wa kiuchumi................Hapa nimejaribu kupunguza vipigo kwa wanawake.....LOL.
  Naamini wakishirikiana vizuri katika kipindi hicho cha mpito mambo yatakuwa shwari...........
   
 11. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Namhurumia mume atayeuvaa mkenge kukuoa wewe.
   
 12. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Umetoa ushauri mzuri kwa wanandoa,ebu toa na kwe2 wenye wapenz hatuna ndoa!
   
 13. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  dogo mimi sio faiza ni fazaa :cool2:
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Bora umefafanua, maana nilishtuka sana.............................
   
 15. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Duh Mtambuzi hiki huwa kipindi kigumu sana na msipoangalia ndoa yaweza kwenda na maji pia.Cha msingi ni kumuomba mungu tupate mke/mume mwema anayeweza kula bamia na sukuma wiki au mlo mmoja kwa siku.
   
 16. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mkuu halafu kuna wale wanawake ambao uchumi ukiyumba tu nyumbani mwanamke anakuona huna maana kabisa, au ndipo kisirani kinaanza unakumbuka ule uzi wako wakumalizia hasira nyumbani? maana kama mwanaume unapiga hesabu za hali ya uchumi halafu mwanamke naye ndio anakuwa kisharwala kweli inaweza kupelekea ugomvi utakaoishia kwenye kipigo kwa wale wanaume ambao mikono yao ni mwepesi.
  kuna wale wanawake ambao hapendwi mtu hii inapelekea baadhi ya wanaume ili kumrithisha mke wake anajikuta akifanya vitu vya ajabu mjini. au kujiingiza hata kwenye dili zinazomrisk maisha yake, wengine wanakuwa hata wezi, ili kuokoa hali ya uchumi nyumbani yaani usipokuwa mvumili kwelihali inweza kuwa mbaya zaidi, maana ukute mwanamke alikupendea pochi kama wale walikuibia pochi lako wakati ule ukiwa mreno sasa kama wasingekupora pochi ukafanikiwa kumtwaa na kuuona utukufu wake mara ukajikuta unaweka ndani ebu niimbie mwanamke kama yule uchumi ukiyumba kidogo inakuwaje? unaweza hata kunyimwa yale mambo yetu yale atii.
  ndiposa unakuta hata mtu inabidi upige madili hata ofisini ku-rescue hali ya uchumi home.

  Thank God uchumi ukiyumba mke wangu anapaki gari anadandia daladala ingawa huwa sijisikii vizuri kwani huwa ananiambi mi napaki yangu natumia daladala lakini ananikataza mimi kutumia daladala kutokana na nature ya kazi yangu siwezi kufanya bila kausafiri hivyo tunajipigapiga kupata walau hela ya mafuta kwa gari moja.

  Kuna na wale wanawake wengine nao wanaona kabisa hali ya uchumi sio nzuri lakini utasiki unajua nilikuwa napita nikakutana na mama nanii anauza nguo nzuri nimezichukua ameniambia nitamlipa baadae.

  pia kuna wale ambao hawaju hata kuweka akiba wakati hali ikiwa nzuri mwanamke mwenye busara na akili hali ikiwa nzuri nyumbani unatikiwa uweka na akaakiba atii sio hela yote iaishia kwenye chakula jaribu kubana matumizi maana nimeshuudia idadi kubwa ya wanawake huwa wananua vitu ambavyo hata hawana kazi navyo ili mudari amekuwa nacho au unakuta ananunu nguo anaivaa siku moja halafu ndio basi inawekwa ndani kugawa hagawi kutumi hatumi ili mradi katumia tu hela kununu. au basi nywele ndio za kubadilishwa dizaini kisa siku hata ikiwa bado ziko vizuri.

  kuna rafiki yangu alikuwa anaomba ushauri siku moja kuwa mke wake huwa ananunu mno takataka maana ananunu vitu vingi ambavyo hata hana mahitaji navyo unakuta huko ndani kubejaa mpaka inakuwa takataka kila akienda sokoni lazima arudi na kitu hata kama ni nguo au viatu vya mtumba akifika tu anasema amekuta inauzwa vitu vizuri ilifika maahli ikwa kama ugonjwa.
   
 17. A

  Aisha Adam JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Shukran sana Mtambuzi darasa zuri nimelipenda!
   
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Huu ulipaswa uwe ni uzi unaojitegemea..........................
  Ahsante kwa uchambuzi wako makini.
   
 19. P

  Paul mathew JF-Expert Member

  #19
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Dah, ni kweli kabisa, me nimekuwa namnunulia mke wangu vipodoz vya gharama sna, yani uki convert unaweza nunua mifuko ya ciment hata mi5, ushauri wako nimeufaidi sana. Asante mkuu
   
 20. M

  Mocrana JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 532
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ushauri mzuri sana mkuu, ingawa kuna wanaume wengine jamani ata hali ya uchumi iwe nzuri vipi wala hashituki na wala hatakwambia leo mambo mazuri basi hata twende nikutoe outing mpenzi wangu, yeye kila siku analalamika hana hela, na akikukuta mwanamke ndo una kazi nzuri basi wewe ndo utakuwa unabeba majukumu yote, na hasa ukiwa ni mwepesi wa kutoa anapokuwa na shida yani hadi unachoka, mpaka unafikiria sasa huyu mtu tukifunga ndoa kweli huko nyumbani mambo yatakuwaje, lakini kwasababu unampenda inabidi tu uvumilie ukitumai labda kuna suku mambo yatabadilika
   
Loading...