Wanandoa tunaotundana na kuzodoana mara kwa mara ndo tunapendana kwa dhati kuliko nyie mnaoitana switie darling machoni pa watu

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Jaman mapenzi ya ngumi mkononi matam balaa!

Mke Wangu haipiti mwezi lazima Tundundane, tena inabidi nikaze kweli kweli kumchapa !

yeah; yaan kama hatujapigana lazima angalau tufinyaneeeeh tu;

Watu huwa wanafikilia tutaachana kwa vile ugomvi kwetu hauishi lakini kumbe walah tushazoea life style!

Na ugomvi ukiisha huwa umeisha huwa hatununiani, Tunaweza chapana makonde asubuhi halafu jioni tukatoka OUT;
Saingine hata hukohuko OUT zinapigwa tena, tunapatana tunarudi zetu nyumbani freshiiii!

Hivi majuzi alinizingua, akajitia umwamba kunikamata Pumb** nikamzibuaa manungu yakamtoka, hadi majilani wakaja, Akawachenjia, akawatimua yeye mwenyewe wasituamlie! Majilani wakajua tutaachana;

Baada ya siku tatu nilisafili kwenda Dodoma kikazi Haikupita wiki nikaanza kupokea simu za mashemeji na majilani anawasimulia kwamba kanimiss hadi chakula hali kwa mawazo,

Haikupita wiki naye akasema yuko njiani anakuja, eti kanimiss sana, hadi anafika Dodoma alikuwa kakamatwa Mara nne na traffiki njiani kwa overspeed.

Ninachompendea mke Wangu (road league) na changamoto za barabarani huwa anamaliza mwenyewe bila kunipigia simu, kuomba msaada!

Siku moja wife alichomekeana na daladala, yule Dreva akamtusi wife " We Malaya pisha hapo leseni zenyewe mmeletewa na Gari zenu za kuhongwa hizi mnakuja kujifunzia gari barabarani!"
Aisee, Wife alichomoa panga chini ya siti yake akamfuata yule dreva akamchoa huku kamkunja; Akamwambia nataka uniambie wewe aliyekwambia Gari tunatakiwa tujifunzie kitandani nani!! Yule Dreva alizibuliwa vitasa palepale! Wakashikana ubavu, aisee yule Dreva aliburuzwa mtaroni hadi polisi wakaja kuamulia nikaenda kumuwekea dhamana Central!

Kiufupi haya ndo maisha ya Mimi na mke wangu tunadundana sana Lakini mapenzi yetu ni matamu sana na hatujawahi fikilia kuachana na haitotokea ndoa na mwaka wa 13 sasa !!!
Hadi huwa nawashangaa sana watu wengine wanaoachana fasta wakati kutwa nzima huwa wanaitana switie Darling busy wanachat kila saa baby...baby.. lakini hawakawii kuachana!

Nini siri iliyopo kwenye penzi hili la kudundana halafu msiachane? Penzi lenu huko wenzangu likoje?


Tujuzane hapa wadau!!
 
moderator nisaidieni ku-edit Heading... Neno Tunatundana lisomeke Tunadundana
 
Duh aiseee umenikumbusha mapenz yangu nampenzi wangu. Alikuwa akikuta sms zakimaku kwenye simu yangu ananianzishia timbwili, tunapigana sana. Kuna siku ndio ilikuwa funga kazi tulidundana kinyama, majirani wakaja kuamua ila manzi yangu ikagoma. Mpaka wakapata wazo lakumwita mama yake ndio alikuja kuamua tena kwakumtoa ndani nawalisaidizana watu zaidi yawa5 alafu nikaambiwa kidume nijifungie ndani. Ikabidi mzee nijifungie ndani maana nilikuwa nimechoka kinyama, majirani walijua ndio tumeshaachana hivyo, alipokwenda kwao alizidiwa akalazwa, siku hiyo hiyo akanipigia simu nikamuone hospital, mzee nikatimba hsptl mida ambayo najua ndugu zake hawakuwepo mida mibaya saa6 usiku.

Wazazi wake walitaka waende wakanishtaki polisi ila bint aliwakataza akawaambia kama hawawezi kumuuguza bila yakunishtaki nibora wamuache afe.

Mpaka Sasa nipo nae nasasa nafikiria nimuoe2 maana ndio nimegundua anamapenzi yadhati wengine niwazinguaji2 wameendekeza mapichapicha.

Ila kiukweli ugomvi wake ulikuwa mbaya sana maana alikuwa anafunga kabisa mlango ndio analianzisha.
 
Back
Top Bottom