Wanandoa tuache unafiki na huu msemo “amelala na mchepuko kwenye kitanda wanacholalia na mkewe/mmewe”

Me too

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
7,325
9,182
FB_IMG_16493654862081508.jpg

Hakuna watu wanafki kama watu walioingia kwenye NDOA na hata hawa wapambe. nasema ni wanafki zaidi ya walio nje ya ndoa...

Kama una hako kamsemo kakuwaambia watu au kuelezea kesi za watu huku ukiitaja hii sentensi hebu iache mara moja unajiaibisha.

“amelala/kafumaniwa na mchepuko tena kwenye kitanda cha mumewe /mkewe”.

Nataka tu niwaambieni wenye hizo sentensi mara nyingi huzitumia kwa

1/Kujiweka mtakatifu kinafki
2/Kupalilia moto ugomvi unoge
3/Kumvimbisha hasira mtendwa.

Nawauliza nyie wenye hizo kauli mmeshatafakali juu ya hiko kitanda mnachosemea tena cha mkewe / mumewe wa ndoa? nitawaelezea tu ili muache kuwa wajuaji kwa kuitumia hiyo sentensi kwa umwamvuli wa kukoleza ugomvi.

FB_IMG_16493658100008024.jpg
Kitanda mnacholalia mnauhakika ni kipya kabla hamjawahi kubanjuana? (tendo la kubanjuana ni ndoa tyr isipokuwa huwa mnabariki baada ya hapo) kama NDIYO 🙌 ruksa kujitetea na hiyo sentensi na kama jibu SIYO nitakuambia haya..

1/Unauhakika gani hiko kitanda wewe ndiye wa kwanza na wa mwisho kulazwa kubanjuliwa?

2/ Je, baada ya kubariki ndoa huwa mnabadirisha vitanda na kuwa vipya au tu mnaendeleza vya zamani? kama hukubadiri acha ujuaji kujifanya unapepelea hiyo sentensi?

Kitanda mlale na THUMA,SADA,MUDY,SIA, Uje ubariki ndoa na SIKITU wapambe waanze kupepelea hiyo sentensi.

Nitawauliza tu mnajua hiko kitanda mnachokiona kama mtetezi kililaliwa kwa ndoa ngapi kabla ya kubariki na mmoja wapo?

FB_IMG_16493656431080353.jpg

Hope jibu mnalo mkatafte vitanda vipya mpate kujitetea bhandugu?
 
Sasa hapo kuna unafiki gani, kama mtu amekudharau kiasi cha kulala na mtu mwingine kwenye kitanda chenu huoni kama imepitiliza?

Hakuna unafiki wowote hapo, lazima kitanda chako na mumeo kiheshimiwe, hata kama kabla yako waliletwa mamluki!
 
Ndoa ni makubaliano ya mwanamke na mwanaume kuishi kama mke na mume.

Baada ya hapo mnaingia mkataba (kisheria) mbele za watu:
• Mahakamani
• Kanisani/Msikitini/Sehemu ya ibada
• Jamii (ndoa za kimila)

Ndoa hiyo inakuja kurasmishwa na tendo la ndoa baada ya kuwa mmefanya yote hapo juu.

Kukosekana kimojawapo kati ya hayo juu kunaibatilisha ndoa na inakuwa ni kujamiiana tu.

Acha kutupotosha.
 
Ile tu kuitwa NDOA maana yake ni muunganiko Wenye baraka za MUUMBA au MAMLAKA HUSIKA, ikiwa ni hivyo basi ni lazima kienziwe na kitukuzwa na kutenganishwa na kila uchafu....

Nakupa mfano; Kipato cha halali na kisicho cha halali havikai pamoja kama utakqtishaji wa fedha na mfano wake, kimoja kinalipiwa kodi na kingine ni miaka kadhaa cello....

Ndoa ni tendo takatifu na maingiliano kati ya wawili walioko kwenye ndoa ni maingiliano yenye baraka na kinyume chake hivyo nyumba achilia mbali kitanda unayoishi na mkeo lazima iheshimike kama inavyoheshimika ndoa.....

NDIYO MAANA SIYO KILA MTU ANA RUHUSA KUFUNGISHA NDOA......

Jamii isiyoluwa na ETHICS ni jamii iliyokufa hivyo TUTUKUZE tamaduni na imani zetu zinazotufanya TUITWE Watanzania [Mfano]
 
Ndoa ni makubaliano ya mwanamke na mwanaume kuishi kama mke na mume.

Baada ya hapo mnaingia mkataba (kisheria) mbele za watu:
• Mahakamani
• Kanisani/Msikitini/Sehemu ya ibada
• Jamii (ndoa za kimila)

Ndoa hiyo inakuja kurasmishwa na tendo la ndoa baada ya kuwa mmefanya yote hapo juu.

Kukosekana kimojawapo kati ya hayo juu kunaibatilisha ndoa na inakuwa ni kujamiiana tu.

Acha kutupotosha.
Siyo kweli.... ndoa ikishafungwa hata kama hamjashiriki tendo la ndoa tayari ninyi ni wanandoa Rasmi.... hata Akifa mmoja kabla ya kukutana kimwili anayebaki atamrithi mwenzake kulingana na sheria bila kujali walishiriki tendo au hawakushiriki....

Ukisema tendo linarasimishe maana yake kabla ya kushiriki basi ndoa hiyo siyo rasmi.
 
Sheria ya wapi hii: Rwanda au Burundi?

Mnaoana ili kurithi?
 
Sheria ya wapi hii: Rwanda au Burundi?

Mnaoana ili kurithi?
Dini zote na katiba ya nchi yako....🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Wanyarwada ni ndugu zetu wala hawana shida....

Tembelea Kigali ujifunze, hata barabarani askari hawazunguki nyuma ya gari kama huku bongo, kama una kosa ni kosa na sii vinginevyo....

Hakuna kula miea barabari na kutupa maganda ovyo ovyo kama ndugu zangu flani hivi....
 
Dada unaolewa lini?? au basi....😁
😄😄 kuwa mchache wa maneno na wewe

haka kasentensi nimekatafakari nikaona ni unafki tu ni sawa na mchungaji anamseminisha muumini kuhubiri na kukemea shetani mbaya ghafla mkakutana kwa mganga.😂
 
Hakuna watu wanafki kama watu walioingia kwenye NDOA na hata hawa wapambe. nasema ni wanafki zaidi ya walio nje ya ndoa...

Kama una hako kamsemo kakuwaambia watu au kuelezea kesi za watu huku ukiitaja hii sentensi hebu iache mara moja unajiaibisha.
"Tunapofungaga" Ndoa LAZIMA tubadili vitu vya zamani KITANDA, Chupi, n.k. (sina hakika kwa wengine).

Kwa Wanandoa, "Kitanda" ni Kitu pekee na Maalumu kwa ajili ya Mwenzi.

Hata "Penzi" kwa mkeo au Mchumba wako linatakiwa liwe maalum, kiasi kwamba akikaa awe anakuwaza kila wakati (Hii ni Pande zote).

Kwahiyo, acha heshima ya KITANDA ibaki kwa wenye ndoa yao.
 
km paragrap yako ya kwanza isemavyo wew hutokuwa mnafiki inabidi ndoa yako iheshimiwe ipasavyo
 
Zamanu niliambiwa na wazee wangu kua mwanamke atasamehe makosa yote ya uchepukaji ya mume wake, lakini kosa pekee ambalo halina msamaha ni mumewe kuchepuka kwenye kitanda wanachokilalia wao mume na mke.
Sa sijui, labda niulize wadada waliomo humu jukwaani, je ni ya kweli hayo??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom