Wanandoa: Kuna ulazima wa mume/mke kuweka wazi kipato chako?

Juma chief

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
2,763
2,364
Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa sana kwa baadhi ya wanandoa kuhusu uwazi wa vipato vyao, mathara ni mshahara.

Kuna wanaume ambao kwao ni mwiko tena hatari kumwambia au kumuonyesha mkewe salary slip yake.

Na kuna wakina mama nao kwakuwa wameolewa na ameajiriwa basi hawataki waume zao wajue vipato vyao.

Je, katika dunia hii ya haki sawa na uwazi ni sahihi baadhi yetu kufanya uficho yaani chako chetu, changu cha kwangu.
 
Ndoa inaunganisha ME\KE kuwa mwili mmoja kwahiyo unapaswa kumuonyesha kila kitu, hata ukipewa tip na bosi wako mjulishe mwenzi wako.

wanaofichana ni wabia wa maisha, wanaishi pamoja kusukuma maisha.
 
Kuna ulazima.

Hivi unaishije na mtu tena kiapo mmeapa na kufichana kitu muhimu kama hichi? Haipendezi kabisa.
 
Maisha ya ndoa yana manbo mengi ,haifai kuyachulia ki mchezo maana kuna wake / waume wakijua kipato chako unaweza ukwawa ndo mwanzo wa kuharibu ndoa
 
Muhimu kuaminiana na kwa mume kutimiza wajibu wake. Kuaminiana kwa maana mume akimwambia leo hali si nzuri "mfukoni" mke aamini anaambiwa ukweli. Kipato cha mke ni cha kwake na yeye ndio ataamua wapi na lini asaidie...
 
Kwa mke lazm na kwamwanaume anawez kuuza raman ya vita akifany hvyo kwa wanawake wetu wa kibongo
 
Kuna ulazima.

Hivi unaishije na mtu tena kiapo mmeapa na kufichana kitu muhimu kama hichi? Haipendezi kabisa.
Mshahara na madeni atajua ila kipato halisi sio rahisi kuambiwa, maana tunawaelewa mkishajua kunahela....
 
Back
Top Bottom