Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,511
Wananchi zaidi ya 170 wakiwemo wafanyabiashara waliokamatwa na mamlaka ya mapato nchini TRA mkoani Arusha kwa kosa la kuuza na kununua bidhaa bila kutoa risiti wametozwa faini ya zaidi ya milioni 900 na baadhi yao wameanza mchakato wa kulipa.
Wanachi hao ni wale waliokamatwa katika msako unaoendelea wa kukamata watu wanaouza na kununua bidhaa bila risiti unaofanywa na mamlaka ya mapato TRA mkoa wa Arusha.
Wakizungumzia hali hiyo wananchi hao licha ya kuomba kuwa wasamehewe kwani wamesahau,watendaji wa mamlaka hiyo wamesema zoezi linaendelea na wote wanatakaoendelea kukaidi agizo hilo watakamatwa.
Chanzo: ITV