Wananchi Wenye Hasira Kali Vs Askari Wa Jiji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi Wenye Hasira Kali Vs Askari Wa Jiji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mambo Jambo, Jul 24, 2008.

 1. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Kumetokea patashika nguo kuchanika kati ya ASKARI WA JIJI na wananchi WENYE UCHU NA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA muda wa dakika kama kumi zilizopita.
  Patashika hiyo imetokea mtaa wa samora ambapo askari wa jiji wakiwa ndani ya gari lao la wazi (lorry) walipoanza kupigishana kelele na wamachinga wa mtaa huo, punde lile lorry la askari wa jiji lilizunguka na kurudi tena mtaa wa samora, baadhi ya askari wale walishuka ndani ya gari hiyo nakuanza kuwakimbiza wamachinga, sasa hapo ndipo patashika ilipotokea, kama wengi mnavyo fahamu sasa hivi mtaa wa samora nyumba nyingi zimevunjwa na mpya zinapandishwa, kutokana na sababu hiyo basi MAWE, MATOFARI na MBAO ziko kila kona, kuna mawe mengi kuliko idadi ya viatu vya wapiti kwa miguu mtaani pale, huku machinga wale wakiwa wanakimbia na wengine wakiwa wanaangalia mali zao, wananchi wenye uchu na maisha bora kwa kila mtanzani walianza kuwarushia maaskari wale matofari, mawe na mboa kiasi cha askari wale kutawanyika na kukimbia kila mmoja na upande wake, wengine wakidondosha marungu yao. Gari lao lilikuwa limeshatoweka, hadi natoka eneo lile kulikuwa hakuna taarifa ya majeruhi wala uharibifu wowote.

  My take:- Ni marufuku kuchukuwa sheria mkononi kama sheria za nchi yetu zinavyosema, lakini hawa askari wa jiji wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi mara kwa mara, kuna kipindi huwa wanachukua vitu vya hawa wamachinga au hata mama ntilie na kugawana wenyewe bila kuvifikisha sehemu husika, sasa inaonekana wanachi wamechoshwa na vitendo vyao
   
 2. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli sipendi kupigia debe wananchi kuchukua sheria mikononi lakini hao wanamgambo wananikera hata mimi! Wacha wapate fundisho na wakome kufanya uonevu usio wa maana. Basi tunaomba kama kuna picha uziweke hapa JF ili tupate kufaidi hiyo action movie!
   
 3. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi naona machinga wana makosa ya kufanya biashara katika sehemu zisizoruhusiwa kwa upande mmoja na kwa upande wa pili sipendi wanamgambo kuwanyanyasa kwa kuwapiga virungu na kufanya vurugu kwenye eneo husika.
  Kuchukua sheria mkononi kwa kwa machinga au mwanamgambo ni makosa.
   
 4. N

  Nahene Member

  #4
  Jul 24, 2008
  Joined: Feb 18, 2008
  Messages: 32
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huu ni mwanzo tu wa matatizo kama haya. Wa-Tz wamechoka na mfumo wa utawala uliopo kwa kuwa hauwatendei haki hivyo wanaamua kuchukua sheria mkononi. nafikiri kwa siku zijazo tutakuwa hali ya kama watu wa pale N'robi-Kibela.
   
Loading...