Wananchi wenye hasira kali mwamvuli wa maovu

Mwana-G

Member
Jan 9, 2016
45
15
Kila kona mauaji ya kujichukulia sheria mkononi ukiuliza huyu kafa kwasababu gani utaskia wananchi wenye hasira kali ukiskia kauli hiyo bas jua hakamatwi mtu, ila wakiuawa tembo serikali inashituka kwamba huko hakuna raia wenye njaa kali? Uhai wa binadamu ni bora kuliko tembo?

Kwanini hawa watu wenye hasira kali wasikamatwe kwasababu ya kupotezA uhai wa binadamu wenzao wakati mahakama zipo?

Kinachouma zaidi ni pale unapogundua kuwa aliye uwawa alikuwa hana atia bali hisia za watu au aliyeuwawa walikuwa na ugomvi na mtu furani huwenda wa madai au la kisha akaitiwa mwizi.

MUNGU WAREHEMU WALIOLALA KWAKULAZIMISHWA.

Naomba kuwasilisha ili serikali itazame upya hawa raia wenye hasira kali.
 
Back
Top Bottom