Wananchi wazuia wafanyazi na magari ya mgodi wa geita kuingia mtaani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wazuia wafanyazi na magari ya mgodi wa geita kuingia mtaani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanta, Apr 5, 2012.

 1. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wadau, wananchi wanaoingia mgodini kwa ajili ya kuchukua mali yao wameanzisha vita na mgodi kwa kukataza wafanyakazi na magari ya mgodi kuonekana mtaani. Siku za hivi karibuni wamekuwa wakiingia kwenye mgodini kundi kubwa kama la watu 300 huku wakiwa na silaha, juzi mlinzi mmoja alipigwa panga la kichwa na watu hao na leo asubuhi magari ya mgodi yanayopeleka wafanyakzi mgodini ilibidi yabadilishe njia baada ya wananchi kuweka vizuizi kwenye barabara ya kuingilia mgodini.Ujumbe ambao umetolewa na uongozi wamgodi muda mfupi uliopita ni huu hapa chini;
  "Due to an increase of illegal miners with high level aggression to both GGM and contractors we have received a threat that any ‘vehicle with a flag’ seen in town will be burned. MD ha
  s requested security to stop vehicle access via Mike 1 to Geita Town until further notice.


  We will inform you know when the situation has stabilized."

  Thank you
   
 2. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli
   
 3. mbota

  mbota JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 745
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 60
  ten pa.
   
 4. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe kanta inaonekana ni mfanyakazi wa mgodi,wambie hao mabwana zenu tanzania ya leo cio ya jana,wale wafanyakazi wanaoua watz wenzao kisa kulinda wazungu waibe mali yetu mungu atawalaani
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Is this 2012???????
   
 6. Crucial Man

  Crucial Man JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 3,277
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  kazi ipo,yetu macho,mda si mrefu ffu watamuagwa hapo geita kama njugu.
   
 7. N

  Njaare JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Who are the illegal miners? Poor citzens who want copasation for their land or GGM which took peoples' land by force?
   
 8. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mabomu ya machozi sasa yanarindima mjini, kaaaaaazi kwelikweli Geita mjini hapo.
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Uh,GEITA HUWA HAPAKOS JAMBO HAPO,
  ANY WAY LETS WAIT N C
   
 10. T

  Thesi JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kanta wewe ni mfanyakazi wa mgodi tena unayepokea mails. Ukweli ni kuwa hawa ni wahalifu. Kuingia mgodini na kuchukua mawe ya dhahabu kwa nguvu au kwa kuvizia sio uzalendo. Najua maisha magumu tuliyonayo wananchi lakin si kweli kuwa ugumu wa maisha unachangiwa na mgodi. Pengine unaweza kusema mgodi unasaidia maisha ya Geita kuwa rahisi zaidi kuliko ambavo usingekuwepo. We are to think and be above grudge we have towards investors. Hatupendi kuona mali zetu zikitoroshwa na wazungu kwa jinsi inavofanyika Tanzania lakini hiyo siyo tiketi ya kuvamia migodi ambayo inawaajiri watanzania wenzetu. Mchawi wetu hapa ni serikali wala si mgodi. Serikali inatakiwa iangalie njia za kuchukua kodi sahihi toka wa wawekezaji kisha kuzitumia vizuri kutoa huduma za jamii lakini haifanyi hivo. |Hata hizo kidogo wanazopewa hawazitumii vizuri. Wanazichezea na kuzitapanya kama wehu waisokuwa na akili. Na nikuambia serikali ni nani? Serikali ni wewe mtanzania unayeandika hapa. Hivo ubovu wa serikali inabashiri jinsi tulivo watanzania. Kwamba hatuchagui serikali nzuri, hatuwajibishi walio serikalini, hatukusanyi kodi toka kwa wawekezaji, hata tukikusanaya kidogo tunazitumia hovyo.
  Those are really ILLEGAL MINERS. and purely they reflect how we Tanzanians we are low. They reflect how Tanzanian government and administration is irresponsible.
   
 11. T

  Thesi JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  GGM acted on the inferior law Tanzania that was acted by Tanzanians for Tanzanians. It paid all required compasations but to their suprize people who were being paid were not the right people. Shame on us Tanzanians. And to be honest that is how we African race and those incivilized are. No morals. No even bounderies for morals to respect and give the people who deserve payments their payments. At the end of the day we take all our angers to investors when it is we Tanzanians who shamefully coned our poor men. Dont blame GGM blame Tanzanians for being so fools especially those elites who instead of acting on their integral duty to protect vulnarables, they use the opportunity to cone them. This illegal practice of paying millions to Geita goverment officials, civil workers, businessmen and leaving poor Nyakabale residents penilles was done and ochestrated by the Geita district leaders of that time. How can you blame GGM? Mzungu hakuonea mtu ni sisi waswahili tuliotapeliana na vviongozi wa serikali wakati huo wakiwemo mkuu wa wilaya Halima Kiemba. Sijui sikuhizi yuko wapi huyu mshenzi.
  Sheria nayo ilikuwa mbovu kwamba mtu analipwa mali zilizoko juu ya ardhi badala ya thamani ya ardhi ikiwepo madini. Nani alitunga hiyo sheria. Mzungu? give me break.
   
 12. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,401
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Hiki kiingereza kwenye red mimi hoi.
   
 13. M

  MCHUMIPESA JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 2,095
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hatuwataki hao wawekezaji matapeli na wakoloni wa kuletwa na serikali ya ccm,we want our natural resources 2b used equally while benefiting all people in our country!,wazungu wamekuja kuwekeza migodini but still we are poorest of the poor,hawana faida kwetu na tutawamaliza kwa kuwachoma moto au vingnevyo,serikali iangalie upya migodi iwanufaishe wazawa na siyo vigogo na familia na mademu zao.
   
 14. J

  Jozdon Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mtemiwao nadhani ww ni gamba. Hayo matusi tena humu JF ya kumwambia jamaa "hao mabwana zao" sidhani kama ni sehemu yake. Umekuwa Lusinde??
  Haya yote si kosa la muwekezaji, hii ni nchi, serikali ndiyo iliyoruhusu haya kwa njaa ya baadhi ya maofisa. Jk, Mkapa and others on decision making level should be blamed! Wana kila sababu na uwezo wa kuzuia unyonyaji huu.
   
 15. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe thes acha mambo yako na vingereza vya kuungaunga,inaonekana na wewe ni tarishi wa wakoloni ila una kacheo kidogo hivo unajiona umewini,washauri sasa mabosi wako ....wawalipe wananchi wa nyakabale,katoma nk
   
 16. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Nipo geita Mjini,

  Kwa kweli huwezi kuamini kama ni eneo la Tanzania.Risasi na mabomu ya machozi ilikuwa sehemu ya maisha ya wananchi wa Geita leo.

  Watu wameshindwa kutekeleza wajibu wao somewhere wanahisi watu vibaya,Wiki iliyopita na sasa napewa vitisho kwamba ni miongoni mwa wachochezi Geita.Nilitishiwa maisha na niliripoti polisi nilipewa RB no. GE/RB/1092/2012

  Kuna kambi ya wakimbizi Geita (NIGER DELTA) ya Tanzania.Haya ndiyo matunda ya uwekezaji holela.Vijana wanakamatwa na kunyanyaswa hovyo kulinda maslahi ya makaburu.Hili ni jambo lisilokubalika
   
 17. M

  MALAGASHIMBA Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Ndugu usikurupuke kwa kitu usichokijua,unaijua Geita kabla ya kuja hawa wezi?Wanapochimba sasa palikuwa na watanzania wengi waliokuwa wamejiali kwa shuguli za uchimbaji na maisha hayakuwa magumu kiasi hiki.Mtakuja,Mgusu,Katoma na maeneo yote wanayochimba yalikuwa yao,sasa kwa nini wasiende kuchukua mawe yao?Wewe unaonekana ni mmoja wa hao mbwa wa wazungu.
   
 18. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,787
  Likes Received: 2,684
  Trophy Points: 280
  na utaambiwa kuwa huyo ni "expert" kutoka nchi za nje.
   
 19. T

  Thesi JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ben,there is somewhere those who call themselves or are activists miss the point including we who support CDM. Mtu akifanya uhalifu usimtetee eti unamtetea mtanzania. Tumefanya haya makosa Nyamongo tumewatetea watu ambao wanaingia mgodini wanafanya uhalifu, wanakijiji wanaoiba miundo mbinu ya kukinga maji machafu kwenda kwenye mazingira, wananchi wanaodhurika kwa zebaki wanayosafishia dhahabu mwisho wasiku wanaonesha waandishi wa habari na watu wasiojua mambo haya kuwa wameathirika kwa sumu za migodini. Kutokana na frustruation za maisha, hasira dhidi ya serikali na wawekezaji siku zote tunaishia kuwahukumu wawekezaji kana kwamba wananchi wanaogombana nao ni malaika. Mwisho wa siku tunatumia hizi hasira za wananchi kama mtaji wa kisiasa hata kama tunawajenga kuwa walaghai, wahalifu na wasiojali chochote ila kupata pesa na kujifanya wanaonewa ili umma uwaoneee huruma.
  Mimi napinga kabisa upumbavu unaoendelea kwenye rasilimali zetu lakini siwezi kumuunga mkono mhalifu anayejifanya ni mzalendo kwa kuiba mali ya mwekezaji. Hao wanaoingia mgodini na kuleta rabsha zote sio wenyeji wa Geita. Ni wahalifu waliojikusanya toka sehemu mbalimbali kwenda kuchukua mawe ya dhahabu mgodini. Kama jambazi anavovamia nyumbani kwako akiwa na panga na kutokuwa na huruma kwa maisha ya watu ndivo walivo.
  Wameshakufa wengi mno mgodini kwa kuingia sehemu wasizozijua madhara yake, wengine kwa kipigo wanazopewa na walinzi lakini hasa ni kudondoka kwenye mashimo marefu. Huu ni ujinga hatuwezi kupoteza maisha ya watu kirahisi hivo eti kisa wanatafuta dhahabu. Serikali lazima iwadhibiti japo nna wasiwasi na njia duni wanazotumia askari wetu kukabiliana na wahalifu, inakuwa ubabe kuliko sheria.
  Hivo Ben unavodeal na mambo haya uwe makini sisi tunaojua japo hatuungi mkono serikali wala unyakuaji wa rasilimali zetu tunaweza kukuona kama unawaunga mkono wahalifu kumbe tatizo hujui game inavochezwa. Unakuwa umeingizwa mjini.
   
 20. Mkomamanga

  Mkomamanga JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 818
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  No no no there is no excuse for people who are smuggling our wealthy, the frequently heard story of citizens corruding with the foreigners has no logic since from 1948 (year of charter for human rights), all them and our leaders and we ourselves have a duty of protecting others.
   
Loading...