Wananchi wazishukia kauli za kitoto za Membe

KICHAKA

Member
Jun 17, 2009
58
9
Kupitia ITV jana kipima Joto wananchi mbalimbali wameshukia kauli za kitoto za Membe Joka la Mdimu zilizokuwa zikijifanya kuwa na nguvu ya Amri Jeshi Mkuu za kutangaza kuwa jeshi letu litaenda kupigana Kongo. Hii ni mara ya pili katika wiki moja ambapo kauli za Joka la Mdimu zinapingwa na wananchi ya kwanza ikiwa ile ya kutaka kuihusisha Sadc kama third party katika mgogoro wa Malawi kauli iliyopingwa mja kwa moja na Rais na hii ya juzi pia imepingwa katika mkutano wa wakuu wa nchi uliofanyika jana Uganda. My Take kweli tulikuwa hatumjui Joka la Mdimu hadi kufikia 2015 tutakuwa tumemfahamu vya kutosha na kwa papara hizi za kukimbilia matamko bila kuwa na baraka ya wakuu wake wa kazi, asubiri tu tumjue zaidi na mwisho kumpuuza kabisa
 
Kupitia ITV jana kipima
Joto wananchi mbalimbali wameshukia kauli za kitoto za Membe Joka la
Mdimu zilizokuwa zikijifanya kuwa na nguvu ya Amri Jeshi Mkuu za
kutangaza kuwa jeshi letu litaenda kupigana Kongo. Hii ni mara ya pili
katika wiki moja ambapo kauli za Joka la Mdimu zinapingwa na wananchi ya
kwanza ikiwa ile ya kutaka kuihusisha Sadc kama third party katika
mgogoro wa Malawi kauli iliyopingwa mja kwa moja na Rais na hii ya juzi
pia imepingwa katika mkutano wa wakuu wa nchi uliofanyika jana Uganda.
My Take kweli tulikuwa hatumjui Joka la Mdimu hadi kufikia 2015 tutakuwa
tumemfahamu vya kutosha na kwa papara hizi za kukimbilia matamko bila
kuwa na baraka ya wakuu wake wa kazi, asubiri tu tumjue zaidi na mwisho
kumpuuza kabisa

alitoa ufafanuzi wa alichomaanisha.
 
wewe ni KICHAKA cha EL huwezi kupost kitu objectively!??
 
Last edited by a moderator:
Kati ya viongozi ambao tutakapo kosea na kumchagua kua rais ni membe,yani kwanza hajiamini,mnafiki,mpenda majungu na zaid ya yote ni mburula ile mbaya apendi kushugulisha ubongo wake hata kidogo,sasa yeye anataka kwenda congo vitani wakati waasi wenyewe wanataka kukaa mezani na gvnt yao..z beta huyu dhaifu aendle kuliko membe.
 
Ni kawaida ya ccm kupishana katika utoaji wa habari na hasara yake ni kuwachanganya wananchi kuwa ni yupi anatoa kauli iliyosahihi kumbuka hapo mwanzo issue ya malawi ilivyotolea kauli zaidi ya tatu tofauti na Membe, Lowasa na Kikwete
 
Mtoa mada jaribu kuwa objective zaidi na usiwe subjective. Siasa na diplomasia za kimataifa wakati mwingine unatakiwa uwe na kauli thabiti,zilizo straight na hata makaripio ikibidi. Haujaona juzi tu Israel imesema itaanzisha tena mashambulizi kama itaona Hamas wanarusha tena makombora ingawa tayari kuna cease fire kule,haukumbuki wakati wa september 11 Bush jr. alisema waziwazi kwamba rafiki wa nchi adui wa US siku zote atakuwa nae ni adui wa US?. Tusingemwambia mama Banda kwamba utafutaji mafuta na gas kwenye upande wa Tanzania wa ziwa nyasa ni kosa na tuko tayari kulinda eneo letu hilo kwa gharama yoyote,wamalawi si wangekuja kutafuta mafuta na gas mpaka Kyela?.Wakati mwingine ukiwa kiongozi wa nchi au hata ukiwa baba unayeongoza familia yako,unatakiwa uwe na kauli straight na serious kwa watu insane watao kuchokoza. Ndipo hata wananchi wako au familia/watoto wako watakuheshimu na kukuamini kwamba unaweza kuwalinda. Unajuaje kama kauli hiyo ya Membe siyo iliyosaidia leo hii Jumapili viongozi wa M23 wapo kwenye kikao na Kabila?. Sidhani kama Membe anafaa kuwa rais kwa 2015,lakini kwa anayoyafanya mpaka sasa kwenye position yake hiyohiyo naona yapo sawa.
 
Back
Top Bottom