Wananchi wazidi kususia mikutano ya Wabunge wa CCM majimboni. Shida ni nini?

jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
19,059
35,840
USHIRIKI WA WANANCHI WA KIBADA KWENYE MIKUTANO YA HADHARA HAURIDHISHI - MHE. NDUGULILE

"Nimesikitishwa na ushiriki wa wakazi wa Kibada katika mikutano wa hadhara. Mahudhurio yenu hayaridhishi. Taarifa imetolewa takribani wiki moja imepita, lakini ushiriki umekuwa hafifu, lakini kwenye mitandaoni watu wanasema sana, tunapoitana, hawatokei. Wanataka nitoe majibu kwa Whatsapp na mitandao ya jamii.

Lengo kuu tunapoitana kwenye vikao ni kupeana mrejesho nanyi kunipa kero zenu.

Kwa mahudhurio haya viongozi na wananchi wa Kibada mnapaswa kujitathmini."

Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni

MKUTANO WA HADHARA - KATA YA KIBADA
#KigamboniMpya
#KaziIendelee

#MaendeleoHayanaChama
 
Ukweli ni kuwa wabunge wa CCM wako kisheria lakini hawana uhalali wowote wa umma. Wote tunafahamu 2020 hakukuwa na uchaguzi bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura. Hali hii imefanya umma kuwasusia viongozi hawa wa CCM.

Kibaya zaidi chaguzi kwa Sasa zitakuwa na wapiga kura wachache sana, sababu hasa ni kuwa wananchi hawawachagui CCM, bali CCM hutumia chaguzi hizo kuhalalisha kuwepo kwao madarakani kwa shuruti. Kwakuwa wananchi wanaogopa kupigwa risasi wakiandamana kukutaa kutawaliwa bila ridhaa yao, basi kususia ndio njia yao pekee kuonyesha nguvu ya umma kuwa hawawataki CCM.

Nawashauri wananchi kuendelea kususia mikutano yote ya viongozi wa CCM, na kwenye chaguzi wasitokee kabisa ili kutuma ujumbe kuwa tumeichoka CCM.
 
Ngoja ifike 2025,mama na watu wake,watapata kura za wanufaika wa matunda yake tu,mfano watumishi wa umma na wale waliopata kazi kwa koneksheni tu.Wananchi wengine hali ni ngumu,atakosa kura na atajua hajui,maana chawa wake wanamdanganya kua anaupiga mwingi sana.Nguvu ya dola iandaliwe vyema,kwani mama atashinda kwa ufinyu sana,na kuhusu wabunge,wajue hali itakua mbaya, polisi na JW,hawataweza kufanikisha utangazwaji wa washindwa sehemu zote.
 
Ngoja ifike 2025,mama na watu wake,watapata kura za wanufaika wa matunda yake tu,mfano watumishi wa umma na wale waliopata kazi kwa koneksheni tu.Wananchi wengine hali ni ngumu,atakosa kura na atajua hajui,maana chawa wake wanamdanganya kua anaupiga mwingi sana.Nguvu ya dola iandaliwe vyema,kwani mama atashinda kwa ufinyu sana,na kuhusu wabunge,wajue hali itakua mbaya, polisi na JW,hawataweza kufanikisha utangazwaji wa washindwa sehemu zote.

Kwa taarifa yako hakuna mtu wa kuandamana ili kuzuia CCM kutangazwa washindi kwa shuruti. Ila kilicho dhahiri ni watu kususia chaguzi. Sioni wananchi wakijitokeza kupiga kura. Utawala wa mabavu wa Magufuli ulichangia pakubwa box la kura kudharaulika. Na kile kitendo cha wapinzani kuacha nafasi zao kwenda kuunga juhudi, kimeshusha moja kwa moja ari ya wananchi kwenye siasa. Itachukua miaka mingi kurejesha imani ya wananchi kwenye siasa na hata kupiga kura.

Kwa sasa wananchi wamebaki kushabikia mpira, maana huko ndio watabaki salama kuonyesha hisia zao bila kutekwa, au kuhujumiwa sehemu zao za kuwapatia kipato. Lakini usitegemee tena hivi karibuni kuona wapiga kura vituoni, au kuhudhuria mikutano ya viongozi wa CCM. Mikutano ya rais inapata watu wengi wengi, maana 80% inatumika nguvu ya dola kuwakusanya.
 
Ngoja chadema waanzshe mikutano ndo tutajua

Wangalau CDM wakianzisha mikutano inaweza kurejesha ari ya wananchi kwenye siasa. Tatizo ni kuwa mikutano ya CDM itachukuliwa kama uchochezi. Na CCM hawatakuwa tayari kuona CDM wakihubiri udhaifu wa CCM huku wakipata wahudhuriaji wengi, wakati huo huo mikutano ya wanaccm ikidoda.
 
USHIRIKI WA WANANCHI WA KIBADA KWENYE MIKUTANO YA HADHARA HAURIDHISHI - MHE. NDUGULILE

"Nimesikitishwa na ushiriki wa wakazi wa Kibada katika mikutano wa hadhara. Mahudhurio yenu hayaridhishi. Taarifa imetolewa takribani wiki moja imepita, lakini ushiriki umekuwa hafifu, lakini kwenye mitandaoni watu wanasema sana, tunapoitana, hawatokei. Wanataka nitoe majibu kwa Whatsapp na mitandao ya jamii.

Lengo kuu tunapoitana kwenye vikao ni kupeana mrejesho nanyi kunipa kero zenu.

Kwa mahudhurio haya viongozi na wananchi wa Kibada mnapaswa kujitathmini."

Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni

MKUTANO WA HADHARA - KATA YA KIBADA
#KigamboniMpya
#KaziIendelee

#MaendeleoHayanaChama
Mheshimiwa salama,
Hicho unachokiona huko kwako Kigamboni kwa sasa ni kila kona ya nchi, labda maeneo machache. Sababu nyingi sana na nyingine unazijua fika kuwa ndizo ulizotumia kuombea kura na hazijapata suluhisho. Kuzungumza jambo lile lile bila utekelezaji ni sababu tosha ya kutoshiriki vikao na mikutano, yaani hakuna jipya. Ukiwa Bungeni na wenzako huwa mnapitisha mambo kana kwamba nyie mnaishi nje ya Tanzania.

Pengo la uchumi katika jamii linachochea hali hii, tukianza na nyie Wabunge dhidi ya kada zingine, ushahidi unao mwenyewe Dr Ndugulile. Kukosekana kwa sera mujarabu kwa changamoto za Watz kunachochea watu kuacha kuwasikiliza. Mlipoamua kutumia miguvu kuhakikisha hakuna mtu mwingine wa kutoa sera mbadala anasimama, ndo mliua kabisa hamu ya watu kuja kuwasikiliza, sbb hamna jipya zaidi ya kuzungusha maneno.

Unaweza usione kilio cha watu sbb (nyie wabunge) mna ulimwengu wenu tofauti. Hivi Mkulima aliyepandishiwa bei ya pembejeo kwa asilimia 100, anapata wapi hamu ya kuja kukusikiliza? Huyu aliyeambiwa umeme atapata kijijini kwake, mpaka leo nguzo zimesimama zina miaka, anapata wapi hamu ya kuja. Kijana graduate ana miaka mitano mitaani jobless, mzazi wake anapataje hamu ya kuja kukusikiliza wakati anaona watoto wenu kimeeleweka.

Kwa ufupi mambo ni mengi yanayokiondolea chama chenu uhalali wa kusikilizwa, bila shaka unajua wanaokuja kwenye mikutano yenu ni wale mnaowalipa posho au mishahara. Ila kama mtaweka uhuru wa kuchagua hiyo 2025, zaidi ya wabunge asilimia 95 hawatorudi mjengoni. Labda muendelee na kile mlichofanya 2020.
 
Kimsingi wabunge wengi hawajatokana na ridhaa ya wananchi, hawa ni wabunge waliopatikana kwa uhuni wa Magufuli kuanzia kwenye chama mpaka kwa wananchi kwenye uchaguzi mkuu na ndio maana ukabatizwa jina la "uchafuzi mkuu".

Kwa mantiki hiyo huwezi kutarajia mwananchi ambaye hakubaliani na hao wabunge kupoteza muda wake kwenda kuwasikiliza.

Pia hali ya maisha ni mbaya sana, Leo unaongelea Kipande Cha sabuni Tena locally made inauzwa shilingi 800, hivi ingekuwa tunaimport sabuni so Kipande kingeuzwa 1500, Sasa kwa style hii ya maisha Hakuna mtu anaweza kupoteza muda wake kusikiliza upuuzi wa wanasiasa especially wa CCM maana wanayoongea ni yaleyale na hayajawahi kumsaidia mtanzania wa kawaida zaidi ya wao kutengeneza mental slaves .
 
Back
Top Bottom