Wananchi wavamia North Mara, mmoja auawa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wavamia North Mara, mmoja auawa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 12, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Habari zinaingia sasa hivi wananchi huko Tarime wamevamia mgodi wa North Mara kwa kile walichodai kutokufaidika na uwepo wa mgodi huo hapo na yaa kuwa maisha yao "hayajaboreshwa". Pia habari hizo zinadokeza kuwa katika kuondoa vurumai hiyo kikosi cha kuzuia ghasia (FFU) kilitumia nguvu na katika kufanya hivyo mtu mmoja ameuawa (stay tuned)
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mzee wa mabreaking Nyuuzi!
  Hongera baba!
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Habari hii imekaa kivipi Mzee wa Kijijini ? Kauwawa na FFU ama amekufa kwa kufika mgodini ? Wacha nivute waya Tarime nijue kulikoni
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Dec 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  inadaiwa kauawa mikononi mwa FFU!
   
 5. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35

  Hawa watu around huu mgodi ni shughuli kubwa sana. Management ya Mgodi inajitahidi sana kuvumilia.
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Du hii sasa ni shughuli kwa serikali, ukiona hivyo jua wana-Mara wamekata tamaa. Je wana-TZ wengine nao?
   
 7. M

  Mama JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Lau tena, duh
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Dec 12, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Michuzi anayo habari kamili na KLHN itaupdate in a minute...
   
 9. M

  Mama JF-Expert Member

  #9
  Dec 12, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Hivi haya mambo huwa yanalipuka tu kama volkano (no hata volkano ina viashiria kama vile metetemeko ya ardhi) au kama kipindupindu (no, una viashiria vya maji machavu na uchafu kwa ujumla), labda kama tsunami (sijui)?

  Ninachotaka kuuliza hapa, je huko mgodini hakukuwa na dalili zozote za kutokea vurugu kama hizi kabla? What is the root cause ya vurugu hizi? Kwa nini huu mzizi haushughulikiwi ipasavyo ili kuepusha madhara kama haya yasitokee?
   
 10. F

  Fisadi.Jones Senior Member

  #10
  Dec 12, 2008
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tarehe 2 Jan. 2007, kuna kijana mmoja kwa jina la Prosper alifanya kitu North Mara ambacho sidhani kama kuna mtanzania amefanikiwa kufanya. Kwa maoni yangu ingebidi apewe nishani ya ushujaa. Lakini sidhani kama story yake ilisikika. Lakini kwa kuwa inahusiana na hii, naomba niwakilishe.

  Prosper alifukuzwa kazi na mwenzake mwingine, tumuite Peter, kwa kosa la kushiriki kuiba mafuta katika magari ya kazi. Kila mtu mgodini, alikuwa anajua haiwezekani Prosper alishiriki kwa sababu ni kijana tofauti kabisa na wenzake wengine mgodini. Mpaka Peter mwenyewe, ambaye alikubali alifanya hilo kosa, alikiri Prosper hakuhusika. Na kila mtu alikuwa anajua Prosper haibagi mafuta kabisa, kwa sababu ndivyo alivyo.

  Lakini kwa sababu wazungu ni Mungu mtu kule, basi huyo mzungu aliyewasemea akachukuliwa anaongea ukweli tupu, na akasikilizwa kama kawaida, vijana wakapewa summarily dismisal, bila lipo lolote. Ilikuwa ni kawaida kwa wabongo kufukuzwa bila sababu za msingi na bila kupewa haki zao, ilimradi tu kuna mzungu kamsemea.

  Prosper alijaribu sana kuomba haki yake lakini hakusikilizwa. Akafanikiwa kupata mtu wa kumlengesha kwa meneja wa mgodi ili aelezee side yake ya story, meneja akasema hana time.

  Baada ya kuchoka, kijana prosper akaenda mgodini akawaambia walinzi anaenda Mwanza, atarudi baada ya siku 3 kuchukua hela yake, kwa hivyo wamtayarishie. Kwa kuwa Prosper ni kijana mpole mno ni rahisi sana kudharau kauli zake, hawakugundua kwamba kijana hasira ilikuwa ishamzidi kimo.

  Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tatu. Asubuhi saa 2, watu (wazungu kwa waswahili) wanakurupushwa kutoka maofisini na kwenda kujificha high-security area. Wazungu jasho linawatoka, waswahili meno nje. Kijana Prosper ameamua kuwafunza watu adabu.

  Prosper ni mtaalamu wa mashine zote za kazi, kuanzia kubwa kabisa mpaka ndogo. Na wenzake walikuwa wanamuita "baba". Ndiye mtu wa kwanza kuendesha excavator lao kubwa kabisa pale North Mara, na kila mtu anatambua yeye ndio mtaalamu na mwalimu wao wa lile likitu. Na mtaalamu wa makitu mengine yote yanayotembea mule ndani.

  Asubuhi hii, Prosper alikuwa juu ya loader lao kubwa kuliko yote, akilizungusha zungusha mbele ya maofisi yao. Kumbuka tairi la hii mashine linaipita urefu Land Cruiser; haya yanayovunja nyumba za watu huko tabata ni chamtoto kabisa. Prosper akawa ameshawaambia kwamba wampe hela yake, au atashusha na kusawazisha kila kilichosimama kwenye eno hilo. Na kila mtu alikuwa anajua hatanii, kwa sababu yeye ndio mtaalamu wa kutengeneza level-ground pale mgodini.

  Wakati anafanya haya, production imesimama, kwa sababu loader hilo ndilo lililokuwa linatumika ku-feed mtambo wa kusaga mawe na kuzalisha dhahabu. Ni hasara kubwa tu huu mtambo usipofanya kazi hata kwa dakika kadhaa. Na prosper alikuwa anajua hili, na akawa anawaambia kwamba anajua wanaingia hasara kwa hiyo wampe hela yake haraka.

  Na Prosper, jisni alivyomuungwana, alisisitiza kwamba hataki kingine chochote zaidi ya hela yake, aondoke. Na alifanya hivyo bila kumtusi mtu.

  Sasa utapenda pale utaposikia kwenye redio koli Prosper akipewa taarifa kwamba dude lile lipo full-tank, kwa hiyo asiwe na wasiwasi hata siku mbili anaweza kukaa nalo. Utapenda zaidi pale utaposikia kwenye redio koli prosper akipewa taarifa kwamba FFU wamefika na wako maeneo gani. Utapenda zaidi na zaidi pale utaposikia Prosper akipewa taarifa kubadili njia kwa sababu FFU wanelekea anapoenda. Na utapenda zaidi na zaidi na zaidi pale utaposiki kwenye redio koli Prosper akiamuru hayo magari ya polisi yageuze la sivyo atafanya kitu mbaya, na yanageuza.

  Naomba nisiielezee story nzima ingawa ni nzuri kama movie. Huwezi kuamini jinsi alivyokuwa anawapeleka-peleka wenye mgodi na wanausalama wa mgodi na wa serikali. Walijaribu kumkamata lakini wapi. Wakawa wanapanga wam-time akiliacha hilo dude wamkamate, lakini wapi. Yaani movie nzima ilipangwa na ikapangika.

  Lakini mwisho wa siku, Prosper akawa amelipwa, summarily dismisal ikawa imefutwa akapewa barua aliyokuwa anataka yeye. Na ni jinsi gani amekabidhiwa bila kukamatwa, pia ni bonge la movie. Yaani utagundua dogo alikuwa sio kama wengi wetu. Na utazidi kubaki mdomo wazi ukijiuliza aliwezaje kulipata hilo dude asubuhi hiyo wakati yeye ashafukuzwa kazi na security kule ni ya hali juu.

  Na kuanzia siku hiyo, wazungu, hasa mkuu wa mgodi, heshima tele. Kuna siku kijana mwingine alikwa anataka mafao yake, mkuu wa mgodi, ambaye zamani alikuwa na kiburi, na ambaye kumbuka alikuwa hana time ya kumsikiliza Prosper, alimshika mkono na kumpeleka mwenyewe kwa malipo haraka haraka.

  Ingawa walikuwa wanawatishia wengine kwamba Prosper is on the run, na anatafutwa na polisi, Prosper hakuwahi kukamatwa. Ilisikika baadaye kwamba Polisi nao waliingiwa na ubinadamu baada ya kuona wazi kwamba kijana alikuwa anapigania haki yake, kwa hiyo juhudi za kumsaka Tanzania nzima zilikufa. Na hata kama zisingekufa, nadhani kijana angewapa tabu kidogo kumpata.

  Nina-propose tutoe nishani ya ujasiri kwa Prosper maana aliweza kuitafuta na kuipata haki yake katika mazingira ambayo wengi hugwaya. Na pia aliweza kuwaekea mazingira mazuri wafanyakazi wenzake waliobaki baada ya yeye kuondoka
   
 11. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #11
  Dec 12, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mpaka sasa ni mtu mmoja amefariki na magari matatu ya mgodi yamechomwa moto.Hali ni tete kwani...kundi la watu lilikuwapo hapo ni kama kijiji kizima na usishangae kusikia wamefunga mgodi kama hali itakuwa ni e tete namna hii...

  Ni wakati wa christimas na watu hawana pesa...hali kama hii si ajabu kutokea....watu hawalimi wala kufuga...gold is just around..huwezi tegemea kutokuwa na mchakato wa kutaka kuchukua mali hizi.Ni mara kwa mara sehemu unapo kwenda kuchukua mali za watu harafu hutegemei resistance ya aina yoyote si rahisi.

  Kwa sasa nimeona kuna gari la Maji ya pilipili(Ngunguli)....limepaki tayari kwa ajiri ya kazi ya kupambana na Wananchi...

  Ingekuwa wakati wa awamu ya tatu nadhani wazee wa kazi jeshi...wangeshuka hapa na kufanya mchakato mkali..kwa kuwa alisema atamlinda mwekezaji kama mboni a jicho.
   
 12. Baba Sangara

  Baba Sangara JF-Expert Member

  #12
  Dec 12, 2008
  Joined: Dec 16, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  hebu hao watuonyeshe hio hasara ya billioni 16 tuthibitishe wenyewe! Hao watu wa migodini wanatabia mbaya ya ku-overprice mitumba yao.. njia nyingineya kukwepa kodi...waweke hadharani mashine zilizoharibika!
   
 13. A

  August JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2008
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  naona wananchi nao wanataka mrahaba wao, kama alivyo chukua mawaziri wetu watukufu.
  nb: naona michuzi kaondoa picha za dhahama ya North Mara gold mine.
   
 14. k

  kadata Member

  #14
  Dec 13, 2008
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  a very good precedent...bravo my Tanzanians from Tarime!!! sasa pandora box ndo linafunguka, migodi mingine wajandae!! upuuuzi mtupu,Nyerere alikataa U-Mangungo,hakukosea!!
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ni bora ujeruiwe au kufa kwa kutetea haki yako kuliko kubweteka na kuambulia maisha magumu at the expense of few individuals.
  Wana North Mara keep it up,tuko pamoja
   
 16. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Hii ni dalili tosha ya kuwaeleza wakuu kuwa yaliyotangulia kutokea hayakuwa bahati mbaya. kuzomewa kwa viongozi, migomo katika sekta mbalilmbali na sasa madini. Wanachuo waliitwa wahuni na JK akasema ni ukosefu wa maadili! Hawa sijui atasema nini.
   
 17. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #17
  Dec 13, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  MMKJ, Tunafika mbali sasa. Matumizi yadola yanaonekana ni sawia hasa pale watu wanapodai mamo ya msingi!
  Lakini naamini siku moja fursa itatulia,tutakuwa na nchi tunayoweza kusema ni yetu,tutakuwa na makao tunayoweza kusema ni yetu.Tusiache kushiriki katika vita ya kuleta uhuru wa kweli wa Mtanzani. Tukumbuke samaki ana miengi yakusema lakini ana maji mdomoni so sisi ambao japo kwa shida tunaweza kusema tusiache kusema yumkini katika kumi mawili yakasikika!
   
 18. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,186
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  Mama, panapofuka moshi..........
  Kwa mujibu wa blog ya Michuzi uvamizi huu ni wa mara kwa mara na unafanywa na vijana.
  Sasa swali la kujiuliza ni hatua gani zimeshachukuliwa na serikali kutatua mgogoro huu?
   
 19. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Behind all this ...Kujifanya hakuna swala la Haki na Usawa katika kumiliki rasilimali za taifa ni kujidanganya kabisa.

  That is the effect of the BIG CAUSE ...ambayo lazima ifanyiwe kazi vinginevyo...itakuja kulipuka in very big picture...!

  Na hiyo eruption italazimu kulipitia tena Azimio La Arusha katika Upya wake .... Katika kizazi kijacho.
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Dec 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,784
  Trophy Points: 280
  Date::12/13/2008
  Wananchi wawazidi nguvu polisi mgodi wa Nyamongo

  Florence Focus, Musoma
  Mwananchi

  VURUGU kubwa juzi zilizuka kwenye mgodi wa Nyamongo mkoani Mara wakati wananchi walipovamia na kupambana na polisi ambao walilazimika kufyatrua risasi zaidi ya 40 pamoja na mabomu ya machozi na kumuua mtu mmoja.

  Watu hao wanasadikiwa kuwa walikuwa wakitaka kuchukua dhahabu kwenye mgodi huo ambao umekuwa ukikumbwa na mapambano ya mara kwa mara baina ya wananchi wa eneo hilo.

  Watu hao, ambao wameelezewa na kampuni ya Barrick kuwa walikuwa karibu 400, wanasemekana walivamia mgodi huo baada ya kusikia mlipuko mkubwa wa mwamba ambao unasadikiwa una dhahabu nyingi na hivyo kuvamia kwa lengo la kuokota mawe yenye dhahabu.

  "Juzi kulikuwa na mlipuko mkubwa sana na hivyo watu wa huko wanajua kuwa sehemu hiyo huwa ina dhahabu nyingi na hivyo waliamua kukimbilia ili kwenda kuchukua mawe yenye dhahabu," alisema afisa uhusiano wa Barrick Gold, Teweli Teweli.

  Vurugu hizo za aina yake kutokea eneo hilo, pia zilisababisha askari wanne kujeruhiwa vibaya.

  "Zaidi ya wavamizi 4,000 walivamia mgodi wa North Mara wa kampuni ya Barrick Gold ulio wilayani Tarime mkoani Mara Desemba 11, 2008," inaeleza taarifa ya Teweli.

  "Uvamizi ulianza karibu saa 12:30 wakati karibu wavamizi 400 waliposhuka kwenye eneo la Nyabirama ambako wafanyakazi wa Barrick walikuwa wakijiandaa kulipua mwamba, wakati wavamizi wengine 3,000 walikuwa wakiangalia.

  "Wavamizi hao walianza kuwarushia mawe watu wa usalama kwa kushambulia bila ya kikomo na kufanikiwa kuwazidi kwa idadi na hivyo askari hao kukimbia na kurejea sehemu zenye usalama. Ilipofikia hapo, watu wengine walianza kuingia Nyabirama na kuanza kuteketeza mitambo ya kuchimbia."

  Taarifa hiyo inaeleza kuwa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia, FFU waliwasili saa 4:00 wakiwa kwenye magari mawili na kufanikiwa kutuliza fujo na hivyo kitengo cha dharura cha Barrick kuzima moto katika jitihada za kuokoa mitambo hiyo.

  Miongoni mwa vifaa vilivyoharibiwa ni pamoja na gari kubwa la kubebea mawe la CAT Loader 988, mtambo wa RH 170 na RH120 na mtambo wa kuchimbia wa DI 600, vitu ambavyo Barrick imesema thamani yake ni dola 15 milioni za Kimarekani (sawa na zaidi ya Sh18 bilioni za Tanzania), kwa mujibu wa Teweli.

  Afisa upelelezi wa jeshi la polisi mkoani hapa, Deusdedit Katto aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa polisi ililazimika kutumia nguvu hiyo kubwa kutokana na fujo walizokuwa wakifanya wananchi hao.

  Kwa mujibu Katto, kutokana na vurugu hizo mwananchi mmoja aliuwawa na askari wanne walijeruhiwa na wananchi kwa kupigwa na mawe na mishale wakati wakijaribu kuvamia eneo la mgodi huo.

  Alimtaja aliyeuwawa kuwa ni Hezron Mwita baada ya kupigwa risasi tumboni na askari kutokana na wananchi hao kutotaka kuacha kufanya fujo.

  Alisema askari waliojeruhuliwa ni D689 SGT Hashimu, E4508 Copro Girigori, E7131 PC Bwagosi na E240 Copro Javila ambae alisema kuwa alijeruhiliwa vibaya sehemu za kichwa na kwamba amelazwa katika hosptali ya mkoa kwa matibabu.

  Afisa huyo alisema kuwa chanzo cha mapigano na vurugu hizo ni kutokana na wananchi wa eneo hilo kuwa na tamaa ya kutaka kuchukua dhahabu kwa nguvu katika eneo la mgodi wakati mgodi huo ulipokuwa ukifanya kazi ya kupasua miamba.

  Alisema kuwa wananchi hao waliusababishia mgodi huo hasara ya kuchoma moto mashine mbili, moja ya kusafirishia mchanga na nyingine ya kupandisha maji.

  Alisema kuwa jeshi la polisi limepeleka vikosi vya maaskari kwa ajili ya kutuliza ghasia na kwamba hali kwa sasa ni shwari na zoezi la mgodi huo la kupasua miamba katika eneo hilo limesimamishwa.

  Mgodi huo umekuwa ukikumba na matukio kama hayo mara kwa mara tangu wananchi walipohamishwa kutoka eneo hilo mwaka 2001 kupisha kampuni ya Barrick kufanya kazi ya uchimbaji.

  Zaidi ya watu sita wameshauawa katika mapambano yao dhidi ya askari wa usalama.

  Mgodi wa North Mara una maeneo matatu, lakini uchimbaji madini unaendelea katika maeneo ya Nyabirama na Nyabigema, wakati Gokona bado unaendelezwa. Mgodi wa North Mara unazalisha dhahabu kati ya aunsi 280,000 na 300,000 kwa mwaka tangu ulipopanuliwa mwaka 2004.
   
Loading...