Wananchi wavamia kituo cha Polisi,wachoma moto nyumba 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wavamia kituo cha Polisi,wachoma moto nyumba 3

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Pdidy, Jun 2, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  [​IMG][​IMG] Wananchi wavamia kituo cha Polisi,wachoma moto nyumba 3 [​IMG] [​IMG] [​IMG] Monday, 01 June 2009 16:46
  *Ni baada kuvamia machimbo ya dhahabu Geita
  *Mmoja apigwa risasi,Polisi naye ajeruhiwa

  Na Faida Muyomba,Geita

  WATU watatu wamejeruhiwa mmoja kwa risasi akiwemo Polisi mmoja katika vurugu, zilizotokea kijiji cha Busolwa B, kata ya Nyarugusu, wilayani Geita baada ya wananchi zaidi ya 1,000 kuvamia eneo la uchimbaji dhahabu linalomilikiwa na kampuni ya IAM Gold.

  Mbali ya watu hao kujeruhiwa, kundi hilo la watu lilivamia Kituo cha Polisi Nyarugusu na kuanza kushambulia kwa mawe kabla ya kutawanywa na askari huku nyumba tatu za Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, zikiteketezwa kwa moto.

  Akizungumza na Majira kwa njia ya simu,Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Bw. Elias Kalinga ,alithibitisha kuwepo tukiuo hilo na kutaja waliojeruhiwa kuwa ni Polisi wa Kituo cha Nyarugusu, Koplo Fabian aliyejeruhiwa mguu kushoto kwa mawe.

  Mwingine ni mgambo aliyemtaja kwa jina moja la Bw.Joseph ambaye alijeruhiwa kichwani na mguu wa kulia kwa mawe. Majeruhi mwingine ni Bw.Pambano Maige(30) ambaye ni mchimbaji mdogo wa dhahabu alijeruhiwa kwa risasi mguu wa kulia na amelazwa hospitali ya Wilaya ya Geita.

  Kaimu Kamanda huyo wa Polisi, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 9 alasiri ambapo watu wapatao 20 wote wakiwa wachimbaji wa dhahabu, walivamia eneo hilo linalomikiwa na IAM Gold na kuanza shughuli za uchimbaji kinyume cha sheria.

  Alisema kutokana na vurugu hizo,watu watatu akiwemo Bw.Maige na wenzake wawili aliowataja kuwa ni Bw.Jimmy Mathias (32) na Bw.Jonas John (30) walikamatwa na Polisi na watafikishwa mahakamani wakati wowote.

  Alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Geita,ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Bw.Fillemon Shelutete, imekwenda kijijini hapo kufanya mazungumzo na wanakijiji hao pamoja na uongozi wa Kampuni ya IAM Gold.

  Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Geita, Dkt.Joram Mpemba,aliliambia Majira kuwa majeruhi Bw. Pambano ambaye amelazwa hospitalini hapo wodi namba nane hali yake inaendelea vizuri na majeruhi wengine walitibiwa na kuruhusiwa kuondoka.

  Habari zinasema kuwa baada ya watu hao kufika huku wakiwarushia mawe Polisi ndipo askari hao hao wakiongozwa na mkuu wa kituo hicho, walilazimika kufyatua risasi angani kwa lengo la kuwatawanya.

  Katika vurugu hizo, risasi moja ilimpata Bw.Maige ambaye alianguka hali iliyozidisha hasira za wananchi hao ambao waliondoka na kwenda nyumbani kwa Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho, Bw.Joseph Mhangila na kuchoma moto nyumba zake zote tatu.

  Baada ya hapo, wananchi hao waliondoka na kwenda Kituo cha Polisi na kuanza kutupa mawe ingawa hata hivyo hawakuweza kufanya uharibifu kwa kuwa Polisi walifanikiwa kuwatawanya kwa kufyatua risasi angani.

  Akizungumza na waandishi wa habari, majeruhi huyo Bw.Maige,alisema wakati tukio hilo likitokea yeye pamoja na wenzake walikuwa eneo hilo wakichimba dhahabu na kusikia sauti za Polisi wakiagiza kufukiwa shimo walimokuwa.

  Alisema wenzao walishikwa hasira ndipo walianza kuwarushia mawe Polisi na mgambo waliokuwa hapo na bunduki, ndipo alishtukia akianguka baada ya kupigwa risasia mguu wa kulia.
   
Loading...