Wananchi watozwa faini na kijiji kwa kosa la kushindwa kulima mazao ya biashara

Mr mtaani

New Member
Jul 4, 2021
3
5
Wananchi watozwa faini na kijiji kwa kosa la kushindwaazao ya biashara

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wananchi wa kijiji cha Usililo kata ya Luwumbu wilayani Makete mkoani Njombe,wameilalamikia serikali ya kijiji hicho kwa kuwatoza shilingi elfu 3 mpaka elfu 5 kutokana na kushindwa kulima mazao ya Chakula na biashara ikiwemo Viazi.

Katika mkutano baina ya wananchi wa kijiji hicho pamoja na uongozi wa kata wakiongozwa na diwani wao ambaye wananchi hao walimuomba awepo ili asikilize kero zao wamefika kwenye mkutano huo kwa lengo la kuwasikiliza wananchi hao na kutolea ufafanuzi malalamiko yao.

Anjelo Ngailo, Ester Sanga, Kastory Kyando, na Anifa Kyando ni baadhi ya wakazi wa kijiji hicho wametoa kero zao kwa diwani wao na kudai kulazimishwa kulima zao la viazi huku wengine wakidai kwamba hawakupewa elimu ya kutosha kuhusu kilimo hicho, ambapo kwa walioshindwa kutekeleza maagizo hayo wamedai kuchukuliwa hatua.

“Imekuwa ajabu kutozwa faini ingekuwa ni kutoa elimu kusudi mwakani tuweze kubadirika”alisema Anjelo Ngailo

Ester Sanga amesema”Mimi nilijikita sana kwenye ngano ila viazi hapana lakini sahizi naambiwa unatakiwa kufika ofisini unashtakiwa hujalima viazi faini elfu 50,tuangaliwe kwaupekee tuna michango mingi hizo faini mtatusamehe”

Kastory Kyando“Pamoja na kwamba baadhi ya watu wamelima viazi lakini Changamoto ipo kuna watu viazi vimenyauka kwa kukosa elimu sahihi walimaje viazi wengine huko shambani vimeungua sasa ofisi itamsaidiaje”

Diwani wa kata hiyo Felix Kyando amejibu kero hizo za wananchi katika mkutano huo na kusema wananchi hao wanatakiwa kushikamana na kujituma kufanya kazi za maendeleo kwa kuwa serikali hupeleka miradi kwa wananchi ambao wanaonesha juhudi za maendeleo ikiwemo kujishughulisha na kilimo na ndiyo maana wanawahimiza kulima mazao tofauti tofauti

“Parachichi na kahawa tutakagua 2022,viazi tutakagua sasa kwasababu ni zao la muda mfupi,nilisema hapa kwenye mkutano kwa hiyo kipaumbele ilikuwa ni kukagua viazi huku umeonyesha mazazo mengine ya kahawa na parachichi,kama umekuja utaratibu mwingene tofauti mimi sikuagiza.Unajua serikali inapotaka kuleta maendeleo inaangalia watu hawa wanazalisha nini”alisema Felix Kyando

Diwani huyo amesema pamoja na changamoto zilizojitokeza katika maagizo yaliyotolewa ikiwemo ukosefu wa elimu ya kilimo cha viazi bado muitikio wa wananchi wa kata hiyo ni mkubwa

Katika hatua nyingine ameagiza wananchi wote wa kata hiyo ambao wanadaiwa faini kutokana na kushindwa kulima mazao hayo kama maagizo yalivyotolewa kusamehewa huku pia akiagiza wananchi wawili waliotozwa faini mmoja shilingi elfu 3000 na mwingine elfu 5000 warudishiwe fedha zao papo hapo na pia wananchi wadai risiti kwa kila fedha wanayolipa serikalini.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Usililo ameelezea kufurahishwa na namna suala hilo lilivyotatuliwa ili kuondoa sintofahamu iliyojitokeza na wananchi waendelee na shughuli zao za maendeleo

“Nashukuru sana diwani kwa majibu mazuri na kwa kuwa wamesamehewa waliopelekwa kwenye baraza la kata na faini.na sababu iliyosababisha kurudishiwa fedha ni kwa kuwa elimu hamkupata hili lilikuwa linatuumiza sana kwasababu wananchi wengine walitaka kukimbia”alisema mwenyekiti wa CCM tawi.
 
Back
Top Bottom