Wananchi watawanywa kwa mabomu wakigombea kununua viwanja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi watawanywa kwa mabomu wakigombea kununua viwanja

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Nov 20, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,419
  Likes Received: 81,465
  Trophy Points: 280
  Date::11/20/2008
  Wananchi watawanywa kwa mabomu wakigombea kununua viwanja
  Na Habel Chidawali, Dodoma
  Mwananchi

  POLISI wa kutuliza ghasia, FFU jana walilazimika kutumia mabomu ya machozi kurejesha amani, baada ya vurugu kubwa kutokea wakati wakazi wa Dodoma walipokuwa wakigombea kuingia ofisi za Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kwa ajili ya kununua viwanja.

  Milio ya mabomu ya machozi na kelele zilitawala kwenye eneo hilo lililo katikati ya mji wa Dodoma, ambako zoezi la ugawaji wa viwanja 500 vilivyopimwa lilipoanza vibaya baada ya watu waliokesha kuwahi nafasi kwenye foleni ili waweze kununua viwanja mapema.

  Viwanja hivyo vilivyo maeneo ya Ndachi vinauzwa Sh250,000 kwa kiwanja kidogo kabisa, Sh270,000 kwa kiwanja cha ukubwa wa kati wakati viwanja vikubwa zaidi vinauzwa Sh370,000.

  Watu walikuwa wamewahi kujipanga kwenye foleni tangu juzi saa 4:00 usiku na hadi jana alfajiri ofisi hizo zilikuwa zimefurika watu kiasi cha kusababisha Barabara ya Nne (ya Msikiti wa Nunge) kutopitika na kulazimisha magari kutumia njia nyingine kuelekea kwenye shughuli zao.

  Baadhi ya watu waliofika eneo hilo juzi usiku walilazimika kupokezana na ndugu, ili waweze kwenda kula na wengine kulala na kurejea jana alfajiri kusubiri kumilikishwa viwanja vipya.

  Lakini, vurugu zililipuka baada ya wananchi hao waliokesha eneo hilo na wengine kuwahi alfajiri, kuona wenzao waliofika asubuhi wakifanya ujanja wa kujipenyeza na kupewa nafasi ya kuwahi kuingia ndani ya ofisi, huku polisi waliokuwa wakisimamia utaratibu wakionekana kubariki vitendo hivyo.

  Hapo ndipo walipoanza kurushiana maneno makali kabla ya kuanza mapigano yaliyosababisha FFU kuitwa eneo hilo na kutumia nguvu kutuliza ghasia. Polisi hao waliwapanga upya wananchi na kuanza kuingia ofisini kwa utaratibu.

  Wengi wa watu waliokuwepo ofisi za CDA ni wananchi kutoka katika mitaa ya Njedengwa, Mtube, Mjimwema na Bochela ambako mamlaka hiyo iliendesha bomoabomoa katika siku za karibuni na kukosa makazi, hali iliyowafanya wawe na matumaini kuwa zoezi la ugawaji viwanja lingewapendelea.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Omary Mganga alisema kuwa baada ya kupata taarifa hizo, aliwatuma vijana wake kwenda kutuliza ghasia hizo, lakini akafafanua kuwa hakuwatuma kwenda kupiga mabomu katikati ya mji na akaahidi kuwa atalitolea ufafanuzi zaidi suala hilo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa CDA, Martin Kitila alisema kuwa zoezi hilo ni zuri na kwamba, litakuwa endelevu kutokana na ukweli kuwa liliwashirikisha watu wa tabaka zote.

  Kitila alisema kuwa jana ilikuwa ni siku ya kugawa viwanja 500 katika eneo la Ndachi, lakini akaongeza kuwa wataendelea kugawa viwanja kadri watakavyokuwa wamepima na akawaomba wale wote watakaokosa kwa awamu hii wasubiri awamu ijayo.

  Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, zoezi la ugawaji viwanja liliwashirikisha wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya dola, Takukuru na watu mbalimbali ambao walifika kuona jinsi zoezi hilo linavyoendeshwa.

  Alisema uongozi wa CDA hauhusiki na tukio la jana kwa kuwa kazi hiyo alipewa mtu mwingine na kuwafanya wafanyakazi wa CDA kuwa na mapumziko jana.

  Katika siku za hivi karibuni, CDA wamekuwa wakilalamikiwa kuhusu kuchelewesha kukamilisha zoezi la upimaji viwanja na kuendesha bomoabomoa kwa nyumba za watu na hivyo kuwakosesha makazi. Suala hilo liliwakasirisha madiwani na kutoa tamko.

  Viwanja mkoani Dodoma vimekuwa lulu tangu vyuo vya elimu ya juu vianze kuongezeka na hivyo kusababisha biashara ya nyumba kuwa juu kutokana na wanafunzi na wahadhiri kupanga nje ya maeneo ya vyuo.

  Mbali na vyuo, shughuli nyingi za kiserikali, semina na Bunge la Jamhuri ya Muungano zinazofanyika mkoani humo zinaufanya mji huo uzidi kuchangamka, huku kukamilika kwa ujenzi wa barabara zinazoingia mkoani humo kukizidi kuingiza watu wengi zaidi.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sidhani hawa wote wanaogombania viwanja hivyo ni ''need'' persons!
   
 3. Piemu Esquire

  Piemu Esquire Member

  #3
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Viwanja vinagawanywa leo 2008,MasterPlan ya Capital iko wapi tangu 1973? Haya ndiyo matatizo yanayojitokeza hata Dar Es Salaam,Kwamba kama Land use Master Plan ingekuweko kusingekuwa na kujenga kiholela.Wizara ya ardhi alipewa John P.Magufuli akawa na mpango endelevu sana,Lakini wakamwondoa na kupewa Wizara nyingine.Hili ni tatizo sugu!!Kla kona ya nchi kuna matatizo ya ardhi,Hata makaburi yanawekwa kwenye migogoro kwa sababu hizo hizo.Ardhi ni Idara inayoongoza kwa rushwa nchini ikifuatiwa na Mahakama.Lakini cha kushangaza na kusikitisha ni pale wadau wa ardhi wanaponyanyaswa ,na kupuuzwa wapozungumzia matumizi sawa ya ardhi.Sera zipo kama hazipo.KULIKONI
   
 4. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mipango ilikuwepo, ila imecheleweshwa kwa makusudi. Miezi kadhaa kabla ya muda rasmi wa kuanza kampeni za uchaguzi, tutashuhudia mengi.

  CCM ni chanzo cha umaskini, kikwazo cha maendeleo....


  .
   
 5. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2008
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  jamani sidhan viwanya kwa sasa ni vyakugawiwa kama pipi kinamna iyo hapo natumai hata ambao si wahitaki na wanahela zao wataibuka tu kujichukulia ingawa si kivile wanavihitaji!
   
 6. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Matatizo ya ardhi yako kila pembe ya nchi yetu na wakuu wamekaa kama vile hawajui kinachoendelea.Hapa Mwanza kuna uvamizi wa viwanja vya michezo na hata vya kulelea watoto lakini Mkurugenzi wa Jiji pamoja na kulalamikiwa kwa zaidi ya nusu mwaka hadi hii leo hajachukua hatua yoyote.

  Kuna kiwanja cha chekechea Mecco Kusini kata ya Nyakato kilichovamiwa na madhehebu ya kilokole na kuwa na usumbufu mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo.Waamini wamekuwa wakijisaidia ovyo na kuchafua mazingira.Pamoja na Mwenyekiti wa mtaa kulalamika na kuomba waondolewe hakuna hatua zozote zilizochukuliwa pamoja na Master plan kuonesha kuwa kiwanja ni cha day care center kuna wala rushwa wameona ni bora wakabidhi eneo hilo kwa Walokole wakati wakazi wa eneo hawataki na wanahitaji kituo cha kulelea watoto wao.Sijui hawa wakubwa wa Jiji la Mwanza wnamfanyia nani kazi badala ya wananchi?

  Viongozi wa aina hii ni kama kansa katika jamii.Wanachezea hisia za wananchi bila kujua athari zake.


  Haka ni kaeneo kadogo tu lakini matataizo ya ardhi hayashughulikiwi na yanapuuzwa.
   
Loading...