Wananchi watakiwa kuzingatia mwongozo wa ulaji mzuri ili kuepuka magonjwa yasiyoambukizwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,920
2,000
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge, amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanafanya mazoezi na kuepuka ulaji usiofaa ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, saratani na kisukari ambayo yamekuwa chanzo cha vifo na usumbufu kwa wananchi.

RC Kunenge amesema hayo wakati wa ufunguzi wa wiki ya kitaifa ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza iliyoanza Novembea 07-14 mwaka huu, kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo amesema katika wiki hiyo wananchi watapata fursa ya kupima magonjwa mbalimbali bure na kupatiwa ushauri wa kitaalamu.

Aidha RC Kunenge amesema kwa kuwa magonjwa hayo yanaweza kuzuilika ni vyema wananchi wakaanza kuchukua tahadhari mapema kwa kuhakikisha wanazingatia ulaji bora, kupunguza ulevi usiofaa, kupunguza uvutaji wa sigara na kuzingatia michezo.

Pamoja na hayo RC Kunenge amesema kuwa kwa upande wa serikali itaendelea kutoa elimu ya kutosha ya namna bora ya kukabiliana na magonjwa hayo na kuendelea kuboresha na kuongeza miundombinu mbalimbali ya afya.
 
DIKASHWA

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
281
1,000
RC bana yaani, hata ungekuwa unakula majani kama ng'ombe wakati ukifika unaondoka na utaugua hzo sijui kansa au sukari, me baba yangu aliishi more than 90 years ila gambe kama kawa fegi sana na alitoboa.
 
LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,526
2,000
Hii itawahusu zaidi wenye hela za kula watakacho,kuna watu kupata mlo wa siku ni shughuli pevu.Milo milo ya ajabuajabu haipo kwao
 
Karungikana

JF-Expert Member
Jan 8, 2017
511
500
RC bana yaani, hata ungekuwa unakula majani kama ng'ombe wakati ukifika unaondoka na utaugua hzo sijui kansa au sukari, me baba yangu aliishi more than 90 years ila gambe kama kawa fegi sana na alitoboa.
Iga ufe! Total ignorance!
 
keisangora

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
2,877
2,000
RC bana yaani, hata ungekuwa unakula majani kama ng'ombe wakati ukifika unaondoka na utaugua hzo sijui kansa au sukari, me baba yangu aliishi more than 90 years ila gambe kama kawa fegi sana na alitoboa.
Don't lie to yourself mkuu. Ina mana hapo kama asingekuwa anavitumia angepiga hata 120 uelewe.
Pia kuna watu wana gene za kushambuliwa na magonjwa Fulani Fulani hata waleje.
Pia wapo wenye gene za kuishi miaka mingi hata kungetokea nini so plz kuwa muelewa Wa genetic kaka/Dada.
 
chafu3

Member
Jul 5, 2020
76
150
Kufa au kuishi ni mapenz ya Mungu na si vinginevyo hizo taratibu za wazungu ukizifuata ndo unaishi kwa hofu
 
Bitoz

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
30,804
2,000
RC bana yaani, hata ungekuwa unakula majani kama ng'ombe wakati ukifika unaondoka na utaugua hzo sijui kansa au sukari, me baba yangu aliishi more than 90 years ila gambe kama kawa fegi sana na alitoboa.
Elewa binadamu tutatofautiana uwezo wa kimwili/kiafya usiige
 
Bitoz

JF-Expert Member
Aug 27, 2015
30,804
2,000
Don't lie to yourself mkuu. Ina mana hapo kama asingekuwa anavitumia angepiga hata 120 uelewe.
Pia kuna watu wana gene za kushambuliwa na magonjwa Fulani Fulani hata waleje.
Pia wapo wenye gene za kuishi miaka mingi hata kungetokea nini so plz kuwa muelewa Wa genetic kaka/Dada.
Umemwelewesha vizuri na kisomi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom