Wananchi wataja sababu za ukubwa wa takwimu za maambukizi Njombe

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
320
154
1552317169396.jpeg

Wananchi wa kijiji cha Njomlole kata ya uwemba mkoani Njombe wanasikitishwa na takwimu za maambukizi ya virusi vya ukimwi kuendelea kuwa kubwa huku mkoa huo ukiongoza kitaifa na kutaja kuwa kupima mara kwa mara katika vituo tofauti kunaongeza idadi hiyo.

Wakizungumza kwa lugha ya kibena mbele ya mbunge Mh. Edward Mwalogo katika mkutano na mbunge huyo kijijini hapo wananchi wa Kijiji cha Njomlole wamesema sababu zinazopelekea Mkoa wa Njombe kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya Maambukizi ya UKIMWI ni kutoamini majibu katika kituo kimoja na hivyo kwenda kupima kituo kingine hali hiyo hufanya taarifa za mtu mmoja kujazwa zaidi ya Mara moja.

"Avanu viwila nyakahano ukupima UKIMWI, unene ndipatikine pazahanati ipo ndina UKIMWI lakini ndibita kukituo na ihingi na hingi na hingi kutokana kuva sitwikwamini na chetwifanya ndio maana Njombe yiwonekana inaongoza kwa UKIMWI" amesema mmoja wa wananchi

Katika hatua nyingine wananchi wa Kijiji hicho wameonyesha kuhamasika na swala la vijana wakike kwa wakiume kutakiwa kujitokeza kufanya mazoezi Kama hatua ya kukabiliana na tatizo hilo kwani mazoezi husaidia kupunguza mihemuko inayopelekea kuhitaji tendo la ngono.

"Utige avana vawedzage kumazoezi ilyo twishukuru baba na vahinza vabitage kudzumbadzumba kusudi pevapilwike vigona tulo ino visemwa kubita kusaka vayagwe" alisitiza Mama huyo.

Naye EDWARD MWALONGO mbunge wa jimbo hilo amesema kuwa umefika wakati wa kuwasiliana na wizara ili kujua ukweli juu ya upimaji wa kujirudia huku akiendelea kuhamasisha wananchi hao kupima na kuanza kutumia dawa mapema na kuonya tabia ya watu kuacha dawa kufuatia madhara kuwa makubwa zaidi na hata kupelekea vifo.

Mkoa wa Njombe unashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na asilimia 11.4 za maambukizi ya virusi vya ukimwi kitaifa,huku mkoa wa Lindi ukiwa wa mwisho kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kuwa na asilimia 0.1
 
Binafsi niliwahi kumuuliza Dokta mmoja wa Kibena Njombe kwanini huu mkoa unaongoza kwa maambukizi hata yeye mwenyewe alisema hana sababu za kitaalamu ambazo anaweza kuzieleza zaidi ya kushangaa tu.
 
Sasa mkuu na wewe umetuwekea hiyo lugha yako ya Kibena wote tutaelewa?

Em fafanua basi hapo exactly amesemaje!

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom