Wananchi watahadharishwa na Mamlaka ya dawa za kulevya kuhusu vitafunwa vya mtaani

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
Wananchi watahadharishwa na Mamlaka ya dawa za kulevya kuhusu vitafunwa vya mtaani




Jamii imetakiwa kuwa makini na vitafunwa vinavyouzwa mitaani, ikiwamo keki na kashata kwakuwa kumeibuka mtindo mpya wa kuchanganya bangi na dawa nyingine za kulevya.

Akizungumza katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu Sabasaba, ofisa kutoka Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya (Adu), Sajenti Chad Ngatunga, alisema kadiri siku zinavyokwenda, watumiaji wa mihadarati wamekuwa wakitumia mbinu mpya ili kutenda uhalifu.

Alisema watumiaji wa mihadarati hiyo wanafahamu maeneo wanayouziwa bidhaa hizo zilizochanganywa na dawa.

“Wapo wengine wanakwenda duka la madawa wananunua dawa kisha wanahangaika na kimiminika aina ya Energy na kujikuta wakilewa kupitiliza,” alisema Ngatunga.

Alisema mabadiliko ya sheria yaliyofanyika mwaka 2015 kuhusu bangi na dawa za kulevya yameongeza adhabu za matukio hayo ili kukomesha vitendo hivyo ndani ya jamii.

“Mabadiliko ya sheria kwa sasa yamebadilika, hivyo kwa anayekamatwa na dawa za kulevya gramu 20 anaweza kufungwa maisha au adhabu kali na akikutwa na bangi kilo 50 anazuiwa dhamana,” alisema Ngatunga.

Alisema mwaka huu kuna binti alikwenda kumtembelea rafiki yake wa kiume, hakumkuta, akaangalia ndani ya friji na kukuta keki akala, lakini ilikuwa na dawa za kulevya.

“Baada ya kula ile keki akaanza kulegea na kukimbizwa hospitali, polisi walipopewa taarifa wakafika eneo la tukio na wakaichukua keki hiyo, ilipopimwa walibaini ilichanganywa na dawa za kulevya,” alisema Ngatunga.

Alisema utafiti mdogo walioufanya wamebaini watu wengi hawana uelewa kuhusu dawa za kulevya na athari zake.
 
dah ndo maana yani sku hizi nmekuwa mpenz wa kashata kwa kuona zinanikata njaa maana nkila kidogo tu nkifika home nalala mazima kumbe kuna poda
 
Wamuangalie sana magufuli nina hofu na yale madafu aliyokula magufuli siku ile mtaani
 
Nashukuru sana kwa kuleta hili bandiko.
Sidhani kama wanachanganya tu ili kila mtu ale. Kashata bei gani na kete ya dawa bei gani? Na wanapata faida gani wakichanganya? Naona huenda ni mbinu ya wauza madawa ya kulevya ya kutembeza dawa zao kwa kuficha. Anajua kashata au keki fulani ina dawa na wanunuzi wake wanakuwa ni watu maalum wanaojua kinachoendelea. Ikitokea amekula mtu asiyehusika itakuwa ni muuzaji kujichanga au labda kama wanataka kumlewesha ili wamwibie.
 
Hapo huyo alotoa tamko ndo kabariki biashara,wacha tutafune kashata kwa kwenda mbele sasa
 
NILISTUKA MAPEMA NDO MAANA VITAFUNWA VYANGU NATOKA ZANGU MBAGALA NAENDA JINUNULIA MLIMANI CITY(SITAKI KERO NDOGO NDOGO MIMI)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom