Wananchi wasisitizwa nidhamu ya matumizi

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Na Mwandishi wetu Mihambwe

Wananchi wameaswa kuzingatia nidhamu ya matumizi ya fedha kwa kuweka akiba, kuwekeza ama kufanya biashara ili kukuza uchumi wao.

Hayo yamesemwa na Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu wakati akizungumza kwenye mikutano ambayo imewashirikisha ugeni toka Benki Kuu ya Tanzania iliyofanyika Kata ya Mihambwe na Kitama.

"Mbele ya ugeni toka Benki Kuu ya Tanzania niliowaalika napenda niwasisitizie Wananchi juu ya nidhamu ya matumizi ya fedha kwa kujiepusha na anasa badala yake mfanye ujenzi wa nyumba za kisasa, uwekezaji kwenye biashara na hata kuwekeza kwenye Elimu ya Watoto wetu." Alisisitiza Gavana Shilatu

Ugeni huo kutoka Benki Kuu ya Tanzania ulikuja na ujumbe wa namna ya kutambua fedha halali; Elimu ya uhifadhi wa fedha kwa njia salama; na namna ya ubadilishaji wa fedha ambapo Wananchi walipata fursa ya kuuliza maswali na kupatiwa majibu.

Wakati huo huo Gavana Shilatu alitumia mikutano hiyo kuwasihi Wazazi wenye Watoto waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza kuwaruhusu na kuwapeleka shuleni Watoto wao kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Katika mikutano hiyo ilihudhuliwa na Watendaji wa Kata, halmashauri Serikali za Vijiji, viongozi wa dini na viongozi wa vyama vya kisiasa.
FB_IMG_1579016103735.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
daah wewe jamaa nimecheki nyuzi zako usipoukwaa uDC sijui

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawezi pewa U-DC huyu, alikuwa anawapiga majungu DC wa Tandahimba na DAS wake na kuwachoma kuwa hawafanyi kazi huko kwenye vikao vyao vya CCM ila mpaka sasa hivi amepuuzwa.
Jamaa kwenye Tarafa yake kuna matatizo lukuki kwenye vijiji vya Chikongo, Kitama, Mkoreha na hata Mihambwe yenyewe ila amekalia majungu tu kwa viongozi wa Wilaya akifikiriankuwa atateuliwa yeye kushika nafasi hiyo.

Inasikitisha sana uroho wa madaraka walionao CCM wenyewe kwa wenyewe wanapigana majungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom