Wananchi wasiburuzwe kudai Katiba mpya -Shivji

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Wananchi wasiburuzwe kudai Katiba mpya -Shivji

Thursday, 09 December 2010 19:59 newsroom

NA SELINA WILSON

BAADHI ya wanasiasa wanadaiwa kuwaburuza wananchi katika madai ya Katiba mpya, imeelezwa. Wanasiasa hao wametakiwa kuwaacha wananchi kupitia mijadala waamue wenyewe kuhusu mabadiliko ya Katiba ya nchi. Imeelezwa wanasiasa hao wanapaswa kuelekeza nguvu katika kujenga uchumi imara, ili taifa liweze kujitegemea. Profesa Issa Shivji, ambaye ni mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesema baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanafikiri Katiba mpya ndiyo mahali pa kuanzia katika kuleta mabadiliko, lakini jambo la muhimu ni kujenga Tanzania mpya. Alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari katika Kigoda cha Mwalimu Nyerere, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 49 ya Uhuru. Pia alizindua kitabu chake cha Cheche.

ìWanasiasa wanataka hatua za haraka kuwaburuza wananchi kutaka Katiba mpya, kinachohitajika ni Katiba mpya ambayo wananchi wenyewe wataamua iweje kupitia mjadala,î alisema. Profesa Shivji aliyebobea katika masuala ya kisiasa na kijamii alisema mwaka 1961 Tanzania ilipopata Uhuru ilikuwa ni hatua ya kwanza. Alisema hatua ya pili ilikuwa kuwezesha uhuru wa wananchi katika ngazi ya jamii, ili wajenge uwezo wa kujiamulia mambo yao wenyewe, jambo alilosema bado halijafikiwa. Profesa Shivji alisema mwaka 1992 mfumo wa vyama vingi vya siasa ulipoanzishwa, wananchi waliburuzwa na kuingia bila kujua nini cha kufanya. ìIlitakiwa wananchi wapewe hata miaka miwili kuamua juu ya mfumo huo,î alisema Profesa Shivji.

Naye Profesa Karim Hirj wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi za Tiba Muhimbili (MUHAS), alisema viongozi wanapaswa kujikita katika kuboresha sekta za madini na utalii, ili mapato yake yaweze kuinufaisha nchi kupiga hatua kimaendeleo. Alisema hoja ya kubadilisha Katiba si jambo muhimu, kwani Watanzania wanahitaji mabadiliko katika nyanja ya uchumi ili wanufaike na matunda ya rasilimali zilizopo nchi. ìMabadiliko ya Katiba yana umuhimu wake lakini jambo kubwa linalopaswa kutiliwa mkazo ni kuboresha uchumi, tunufaike na mazao ya sekta za madini na utalii,î alisema. Kumekuwa na malumbano miongoni mwa wanasiasa kuhusu mabadiliko ya Katiba, baadhi ya vyama, ikiwemo CHADEMA ikishinikiza wananchi kudai Katiba ya nchi ibadilishwe.

Akizungumzia kitabu cha Chehe, ambacho amekihariri, Profesa Hirj alisema kinatoa historia ya mambo yaliyotokea miaka iliyopita baada ya Uhuru, likiwemo jarida la Chehe lililokuwa likiandaliwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kabla ya kupigwa marufuku kutokana na kukemea ubepari.
Kitabu hicho kilizinduliwa na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), Dk. Adolf Kibogoya. Wasomi wengine walipata fursa ya kukifanyia mapitio kitabu hicho.
 
BAADHI ya wanasiasa wanadaiwa kuwaburuza wananchi katika madai ya Katiba mpya, imeelezwa. Wanasiasa hao wametakiwa kuwaacha wananchi kupitia mijadala waamue wenyewe kuhusu mabadiliko ya Katiba ya nchi. Imeelezwa wanasiasa hao wanapaswa kuelekeza nguvu katika kujenga uchumi imara, ili taifa liweze kujitegemea. Profesa Issa Shivji, ambaye ni mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesema baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanafikiri Katiba mpya ndiyo mahali pa kuanzia katika kuleta mabadiliko, lakini jambo la muhimu ni kujenga Tanzania mpya. Alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari katika Kigoda cha Mwalimu Nyerere, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 49 ya Uhuru. Pia alizindua kitabu chake cha Cheche.
Mimi binafsi siamini ya kuwa Profesa Shivji anaweza akawa kigeugeu namna hiyo..............ni karibu wiki moja tu imepita tangia aseme wakati huu ni mwafaka kwa katiba mpya..........sasa hawa Uhuru Publications...........wametoa hii mpya leo jioni........................Yawezekana hakusema hivyo..........................na jingine hapa twaona jinsi serikali ya CCM inavyokazana kuchelewesha jitihada za katiba mpya...............................

Hivi bila uhuru zaidi hayo maendeleo yatatoka wapi? Uthibiti wa malighafi utaanzia wapi kama taasisi za utawala bora ni dhaifu..............Hawa kweli ni wasomi wachovu...............................
 
Sijaelewa hawa wasomi! Yani wanaona madai ya katiba si ya muhimu!? Wanataka maendeleo ya uchumi kwanza?! Hawajui katiba ndo moyo wa nchi,ikiwa mbovu maendeleo ya uchumi yanakua ndoto. Labda pengine mwandishi hakuwaelewa. Yani Shivji leo anasema hayo?! Siamini.
 
i real dont believe this at all! I need reliable source pleaseeeeee.......Nimemfahamu shivj kwa muda na hata ukiangalia past kwenye jarida la cheche alikua naibana sana system leo hii aseme tusihangaike na katiba mpya!
 
Wananchi wasiburuzwe kudai Katiba mpya -Shivji
Asante mkuu kwa juhudi zako za kuwa unatuhabarisha...... Lakini kwanini Source Zako nyingi huwa ni Uhuru?.... Sio kwamba sioni mchangu wako narudia tena kusema asante lakini kama ungekuwa unapata na source nyingine mbadala I would have really appreciated. Asante tena ndugu nagundua mchango wako na Mungu akubariki
 
Yawezekana ikiwa suala la katiba likiruhusiwa kujadiliwa sasa wananchi wakasahau kujenga nchi na badala yake wakabaki wanajadili katiba tu.
yawezekana mtizamo huu ndio wanaouzungumzia hawa wakongwe wa siasa. Binafsi mimi nimewaelewa. Pengine suala la kujiuliza je, ni wakati gani Muafaka kama sio SASA?
 
Hoja za uchumi sasa hivi zielekezwe kwa CCM kwani wao ndiyo wanaoshikilia serikali inayoendesha uchumi.

CHADEMA hata wajikitaka kwenye hoja za uchumi bado hawatasikilizwa na mifano ipo ninaitaja. Waliposema watashusha bei ya mfuko wa simenti CCM wakaja juu kwa Dr. Slaa ni mbumbumbu wa uchumi.

Waliposema watasomesha bure hadi form six Samwel Sitta akaomba mdahalo na Dr. Slaa kwamba ni saizi yake amuumbue jinsi isivyowezekana kutoa elimu bure.

CHADEMA waliposema watapunguza baraza la mawaziri Shivji na wenzake walisikia.

Hoja zote zilikuwa ni za kiuchumi. Kwamba wangekama dola basi hayo wangeyatekeleza.

Shivji anakumbuka kwamba kuanzia mwaka 1981 hadi 1984 kulikuwa na maoni kuhusu marekebisho ya katiba. Je, watu waliacha shughuli za kiuchumi na kujikita kwenye mjadala?

Ukweli ni kwamba uchumi ulikuwa mbaya na tuliokuwa watoto tunasimuliwa kwamba tulikula una wa yanga na kuvaa matairi. Lakini Shivji akumbuke tunavisoma vitabu vyake na vya wengine kwamba matatizo ya wakat huo yalitokana na vita ya Kagera ambayo miezi 18 ya njaa iligeuka miaka 18 kama ilivyotabiri katuni pekee ya wakati ule iliyoitwa Chakubanga ambayo hadi leo mama yangu anayo.

Hakuna kinachogusa mtu kama kampeni za siasa hasa za mwaka huu. Mbona watu hawakuacha shughuli za kiuchumi na kampeni zilifurika huku za Slaa watu wakiitana kwa message na za Kikwete watu wakisombwa kwenye gari.

Nilimsoma geniuos hesabu na physica wa dunia hii aliyeitwa Albert Einsten. Siku moja akiwa mzee sana alpanda basi (daladala) na akakosea kuhesabu nauli. Kondakta akamtukana na kumwabia kama hajui hesabu aende akafundishwe na mtoto wa kindergarten.

Yule konda hakujua anamwambia genious wa dunia aliyefanya hata likagunduliwa atomic bomb. Sasa kama kweli hili ni tamko la Prof. Shivji basi na huyu naye uzee unamuingia vibaya.

WWapinzani wajikite kwenye kwenye Katiba kwani hata bajeti yao kivuli kule bungeni hakuna anayeifuatilia. CCM watekeleze sera zao za walizoahidi kuwatimizia watanzania.
 
Hata mie nilikuwepo newsroom prof shivji alisema katiba mpya ndio msingi wa mambo yote na kwamba kilio cha kudai katiba mpya ya wananchi hakijaanza leo kilianza siku nyingi wakati wa mchakato wa vyama vingi. Amesema katiba ya sasa ni ya kulinda maslahi ya vigogo wachache sio katiba ya kumkomboa mtanzania na kwamba katiba hii haikuundwa na watanzania bali kikundi cha watu wachache. Alisisitiza kwamba bila katiba mpya hakutakuwa na maendeleo yoyote. Ameweka bayana kuwa nchi ya tanzania haihitaji manaibu mawaziri na pia haihitaji wizara zaidi ya 20. Huyu ni mwiba kwa mafisadi na ccm ni mtu safi na anaongea ukweli bila woga
 
Naye Profesa Karim Hirj wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi za Tiba Muhimbili (MUHAS), alisema viongozi wanapaswa kujikita katika kuboresha sekta za madini na utalii, ili mapato yake yaweze kuinufaisha nchi kupiga hatua kimaendeleo. Alisema hoja ya kubadilisha Katiba si jambo muhimu, kwani Watanzania wanahitaji mabadiliko katika nyanja ya uchumi ili wanufaike na matunda ya rasilimali zilizopo nchi. ìMabadiliko ya Katiba yana umuhimu wake lakini jambo kubwa linalopaswa kutiliwa mkazo ni kuboresha uchumi, tunufaike na mazao ya sekta za madini na utalii,î alisema. Kumekuwa na malumbano miongoni mwa wanasiasa kuhusu mabadiliko ya Katiba, baadhi ya vyama, ikiwemo CHADEMA ikishinikiza wananchi kudai Katiba ya nchi ibadilishwe.
Uchumi hauwezi kuboreshwa na watu ambao kwao kujikosoa na kujirekebisha ni msamiati. Unfortunately, kufanya hayo maamuzi ya kuboresha sekta za madini na utalii itakuwa ndoto kama hao wafanya maamuzi hawaeleweki watapatikanaje na watabanwa vipi kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao..it is common sense kwamba nothing is going to change kwa hali iliyopo sasa, thats why we need to tighten up kisheria, ndipo unapokuja umuhimu wa katiba mpya.
 
Mtu anayepinga katiba mpya, manake anataka mambo yaendeleee hivihivi..huyo ni adui wa watz.
 
Back
Top Bottom