Wananchi Washauriwa Kuwa Makini Kutetea Maslahi ya Zanzibar

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=1][/h]Written by amini // 31/01/2012 // Habari // No comments

382772_10150339307921176_721596175_8529287_127344737_n-564x272.jpg
Na Khadija Khamis
Mjumbe wa Baraza la Katiba Zanzibar na Mwanasheria wa kujitegemea Ali Saleh amewashauri Wananchi wa Zanzibar kuwa makini katika kuwasilisha maoni yao ya kutetea maslahi ya Zanzibar na sio kuburuzwa na Wanasiasa ambao wanajali zaidi maslahi yao.
Ushauri huo ameutoa wakati alipokuwa katika mdahalo wa kujadili dhana nzima ya marekebisho ya Katiba na Wananchi wa Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Mjumbe huyo alisema kuwa ndani ya mjadala wa Katiba kuna mambo mengi ya kujadiliwa lakini kwa upande wa Zanzibar la muhimu zaidi ni kujadili kero za Muungano kwani hii ndio nafasi pekee ya kuwakilisha mambo yanayowayima fursa Wazanzibar.
Akifafanua zaidi alisema kuwa suala la Muungano ndio muhimu kwa Wazanzibari kwa sababu limewaunganisha na sehemu ya pili ya Muungano ambapo kuwekwa sawa kwake kutaleta mabadiliko makubwa ya Kisiasa na Kiuchumi kwa Zanzibar
Alieleza kuwa kila siku jamii inazungumzia kero za Muungano jambo ambalo si sahihi kwani Muungano si kero ila Katiba iliyopo ina upungufu mengi ambayo yamepelekea kushindwa kukidhi haja kwa wakati na matumaini ya watu wa pande mbili za muungano huo.
Hata hiyo alisema pindipo Wazanzibari watakaa pamoja na kujadili kwa kina Katiba iliyopo kutawezesha mapungufu yaliyomo kuonekana jambo litakalowapelekea kufanya maamuzi bora zaidi wakati wa kupiga kura za maoni utapofika
Kwa upande wa Wananchi waliohudhuria kongamano hilo walisema kuwa umefika wakati wa kujenga mustakabali mpya wa mashirikiano ya pamoja na kuondoa itikadi za vyama kwa lengo la kujenga heshima ya Nchi ya Zanzibar.
“Tushikamane Wazanzibar tusipokuwa pamoja Zanzibar inakwenda zake lazima tuwe na msimamo mmoja bila kujali itikadi za vyama vyetu”alisema mmoja wa wananchi hao
Pia waliitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iwashughulikie katika kuwapatia vitambulisho vya Mzazibar Mkaazi ili kuweza kupata haki zao bila ya usumbufu.
Aidha walitoa wito kwa Serikali kuzidisha juhudi za kutoa elimu sahihi kwa Wananchi wa Zanzibar juu ya dhana ya marekebisho ya Katiba mpya ili wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba wawe na uelewa mpana.
 
Back
Top Bottom