Wananchi waruhusiwe kuikosoa Serikali?

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,487
2,000
Nimejaribu kuvuta picha ya darasani, kwamba mwalimu anauliza swali na wanafunzi karibu wote wanajibu kwa sauti kubwa 'Ndiyooooo''

Hiki ndicho kilichotokea pale wananchi wengi walipoulizwa swali husika hapo juu.. Ni imani yangu Serikali na wenye mamlaka watakuwa wamesikia jibu la wananchi..

Hata hivyo matusi sio njia sahihi ya kukosoa. Tujifunze kukosoa kwa ustaarabu. Hakuna anayependa kukosolewa kwa dhihaka aisee!

11.JPG
 

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,213
2,000
Huu mjadala ufike mwisho. Rais ameshasema hakuahidi Katiba Mpya kwenye kampeni zake.... Tusubiri utawala mwingine.
Full Stop..
 

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Nimejaribu kuvuta picha ya darasani, kwamba mwalimu anauliza swali na wanafunzi karibu wote wanajibu kwa sauti kubwa 'Ndiyooooo''

Hiki ndicho kilichotokea pale wananchi wengi walipoulizwa swali husika hapo juu.. Ni imani yangu Serikali na wenye mamlaka watakuwa wamesikia jibu la wananchi..

Hata hivyo matusi sio njia sahihi ya kukosoa. Tujifunze kukosoa kwa ustaarabu. Hakuna anayependa kukosolewa kwa dhihaka aisee!

View attachment 648501
Mkuu Beth, hii sio hoja valid, kwasababu hakuna popote wananchi walipokatazwa kuikosoa serikali, kipengele cha freedom of expression kwenye katiba yetu kiko wazi kuwa kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo, maoni na kuzungumza lolote ili mradi uhuru huo usiingilie uhuru wa mwingine, uhuru huo ni pamoja na uhuru wa kuikosoa sio tuu serikali, bali hata kumkosoa rais wa nchi, na kila siku tunamkosoa humu.

Hoja hii imekaa as if wananchi wanakatazwa kuikosoa serikali, hawajakatazwa popote, ila wananchi wengi wa Tanzania, hawajui haki zao, wamejawa na nidhamu ya woga, heshima ya ukondoo, na kutojitambua na kujielewa, hivyo kuigopa serikali kwa uoga wao tuu, au kumuogopa rais as if rais ni mungu, kumbe ni binadamu tuu kama sisi, asiogopwe, bali aheshimiwe.

Hili nimelizungumza sana hapa
Rais Magufuli na serikali yake wakosolewe kwa hoja sio kwa viroja ...
2017 JF Tubadilike, Tupunguze Kuwa "Barking Dogs, Seldom Bite", Tusiishie Kubweka Tuu, Tung'ate!.
Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli | Page ...
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote | Page ...
Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade ...
Paskali
 

Poise

JF-Expert Member
May 31, 2016
7,578
2,000
Ukiona wawakilishi wameshindwa kuikosoa serikali hadi Unaona kuwa sasa wananchi moja kwa moja wafanye hivyo tambua kabisa kuwa machafuko makubwa yanakaribishwa kwenye nchi husika.

Kwa sababu, hakutakuwa na namna tena ya kuwadhibiti watu kujiepusha na mob-justice phenomenon na vitendo vingine vya kiuhalifu.

Kwa hiyo, hilo wazo / utafiti haututakii mema kwenye nchi yetu.
 

Vin Diesel

JF-Expert Member
Mar 1, 2011
9,097
2,000
Kukosoa hakujawahi kuwa kosa...sema sio kila mtu anapenda kukosolewa. Mie mwenyewe mmoja wapo, ukinikosoa lazima ule vitasa, upo hapo?
 

Sam bm

JF-Expert Member
Oct 25, 2017
285
250
Tatizo la wananchi wakiambiwa wakosoe, watachofanya ni matusi tu kwa kwenda mbele
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom