Wananchi warudi kwenye makazi yao bila ukaguzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi warudi kwenye makazi yao bila ukaguzi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KIDUNDULIMA, Feb 18, 2011.

 1. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  katika jambo lililonisikitisha jana ni jinsi ambavyo serikali yetu isivyokuwa makini katika kushugulikia majanga. Rais wa nchi tena amiri jeshi mkuu anawatangazia wahanga kuwa warudi majumbani kwa sababu hakuna mabomu yatakayolipuka tena hali imedhibitiwa. Au kwa vile yameacha kulipuka kwenye kambi ndo hali imezibitiwa? Wao wenyewe wamewatahadharisha watu kuwa kuna wabomu ambayo yametawanyikia kwenye makazi ya watu hivyo watu wachukue tahadhari. kwa layman tahadhari ya kuokoa maisha si ni kukaa mbali na eneo la tukio. Wanafikiri wananchi wamesahau yaliyotokea mbagara baada ya wananchi kurudi kwenye makazi yao huku kukiwa na mabomu ambayo hayajaripuka?

  Mi nilitegemea kwa kuongozi wa nchi kuwaagiza wanajeshi wake wote kuingia mitaani kwenye maeneo yaliyoathirika na kufanya ukaguzi kuhakkikisha kuwa hakuna mabomu kwenye makazi ya watu ndipo wananchi wahamasishwe kurudi majumbani kwa kuwa maeneo yao ni salama. Lakini wapi ni rais yule yule wa utendaji uleule wa kulegalega.
   
Loading...