Wananchi wapiga kura ya maoni ya kupanda bangi

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Wananchi wa mji wa Rasquere (Raskera) katika Mkoa wa Catalonia Spain jana walipiga kura ya maoni juu ya kupanda bangi kama njia ya kukabiliana na madeni yanayoukabili mji huo. Asilimia 56.3 ya kura ilikubali wazo hilo.

Hata hivyo, uamuzi wa kupanda bangi hautafikiwa mpaka hapo Mwanasheria Mkuu wa Spain atakapoamua uhalali wa kura hiyo ya maoni. MAELEZO ZAIDI HAPA
 
Acha wapande bwanaee!
Kwani hiyo Sirkali yao itawasaidia ku'pay hiyo mideni? Ofcoz Not!
 
Acha wapande bwanaee!
Kwani hiyo Sirkali yao itawasaidia ku'pay hiyo mideni? Ofcoz Not!
Serikali yenyewe inadaiwa kope si zake. Isitoshe, wao wanataka kuwaruhusu wawekezaji tu waje kupanda (Ingawaje udongo ulio chini ya waridi nao hunukia).
 
Nadhani hata hapa TZ itabidi tupige kura ya maoni ili baadhi ya mikoa iruhusiwe kupanda bange kwa ajili ya chakula ama biashara. Mfano kule Mara ama Iringa.
 
Mmmh, afu kuna mmoja wa huko kwenye ngazi ya maamuzi inasemekana anatamani bangi ihalalishwe TZ.

Naunga mkono hoja ya kuhalalishwa bangi kwa sasabu suala la kuizuwia ni janja tu ya wakubwa kudhibiti soko, kwani hata isipohalalishwa watumiaji wataipanda japo chini ya mivungu.

Mwisho wa yote, bangi ni dawa. Kuna jimbo moja Marekani (sikumbuki jina), daktari wako akikuandikia cheti unaenda kununua pharmacy na baadhi ya mataifa wanaruhusu kuwa na kiasi kidogo (kama grams 10) kwa matumizi binafsi.

Kwa taarifa ya ziada tu, pia kuna mmea mmoja jamii ya marihuana unaitwa Hemp (Cannabis sativa) ambao unafanana sana na bangi na unalimwa kibiashara na una matumizi mengi yakiwemo dawa na chakula kama bangi. Wajanja huulima pamoja na bangi authentic.
 
Nadhani hata hapa TZ itabidi tupige kura ya maoni ili baadhi ya mikoa iruhusiwe kupanda bange kwa ajili ya chakula ama biashara. Mfano kule Mara ama Iringa.

mkuu watu wataipinga sana ktk matamshi ila kwa vile kura ni siri utaona watakapiga kura ya ndiyo ni wengi
 
Back
Top Bottom