Wananchi wapendekeza uwakilishi wa majimbo ufutwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wapendekeza uwakilishi wa majimbo ufutwe

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Candid Scope, Sep 16, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wananchi wanaohudhiria Tamasha la 10 la Jinsia, wamependekeza utaratibu wa kupata wabunge kupitia majimbo , viti maalum na kuteuliwa na Rais ufutwe, na badala yake zianzishwe wilaya zisizozidi 150 ambazo zitakuwa ndiyo majimbo ya uchaguzi.

  Washiriki zaidi ya 100 kwenye tamasha kutoka mikoa mbali mbali waliohudhuria warsha ambayo jana iliangalia katiba inavyopaswa kulinda haki za uchumi, usawa na usalama wa jamii katika maazimio yao, walisema katika utaratibu wa sasa Bunge linakuwa na wabunge wengi bila kuzingatia ufanisi na usawa kati ya wanawake na wanaume na makundi maalum wakiwepo walemavu.


  Wamesema kwa sasa ambapo kuna wabunge zaidi ya 300, fedha nyingi za taifa zinapotea kwa ajili ya kuwalipa wabunge ambapo baadhi yao hawana ufanisi wowote katika kuendeleza ustawi wa jamii. "Tunataka Bunge la Jamhuri lenye watu wasiozidi 150, nusu wakiwa ni wanawake na nusu wanaume waliochaguliwa na wananchi kutoka kwenye wilaya Tanzania Bara na Visiwani," alipendekeza Peter Nalopori, kutoka Mkoa wa Kagera na kuungwa mkono na washiriki. Kadhalika washiriki wengine 39 waliozungumza na kuungwa mkono na wenzao walisema Katiba Mpya inapaswa izuie mbunge kupewa uwaziri na kwamba idadi ya wizara iwekwe kwenye katiba ili fedha za umma zielekezwe zaidi kwenye shughuli za maendeleo ya wananchi badala ya kuhudumia idadi kubwa ya mawaziri.


  Wametaka pia Katiba Mpya iweke ukomo wa muda wa mtu kuwa mbunge kuwa ni vipindi viwili vya miaka mitano na kwamba mtu akishafikia umri wa miaka 70 katiba mpya ikataze kuwa asipewe kazi hiyo ya utumishi wa umma badala yake aachwe apunzike na kubaki kuwa mashauri wa taifa.


  Kuhusu Spika, wametaka Katiba Mpya ibadilishe utaratibu wa kumpata Spika wa bunge ili asiwe mbunge na mwanachama wa chama chochote cha siasa.


  Kuhusu uongozi wa wilaya na mikoa, wananchi hao wamependekeza kuwa Katiba Mpya iwe na kipengeke kinachowapa wananchi mamlaka ya kuwachagua wakuu wao wa wilaya na mikoa.


  Katika ngazi za vijiji wamependekeza kuwa viongozi wake wawe ni wale wenye sifa ikiwa ni pamoja na elimu na kwamba katiba mpya iweke bayana kuwa mtu asiye na elimu ya sekondari hana sifa ya kuwa hata mjumbe wa nyumba kumi.


  Ili kuimarisha haki na usawa kwa wananchi wote kwenye elimu, wamependekeza kuwa Katiba Mpya iweke wazi kuwa kila mwananchi atapata elimu hadi chuo kikuu. "Tuna rasilimali nyingi za nchi zinazotumika vibaya, zikielekezwa kwenye elimu kila mtoto wa taifa hili anaweza kusoma bure hadi chuo kikuu", alisema Andres Njau.


  Kuhusu madaraka ya Rais, walipendekeza kuwa Katiba Mpya impunguzie Rais madaraka ikiwa ni pamoja na yale ya kuteua majaji na viongozi wa Tume ya Uchaguzi badala yake viwekwe vyombo huru ambavyo vitapewa madaraka ya kuteua watu hao kwa kuzingatia vigezo .


  Kuhusu haki za kijamii na kiuchumi wamependekeza vipendele maalum viwekwe kwenye katiba mpya vinavyoahinisha haki za wananchi katika masuala ya afya, ajira, usalama na haki lugha ya alama kwa walemavu wasioona kutambulika kitaifa na kwamba katiba iweke kipengele ambapo kitaunda chombo cha kufuatilia utekelezaji wa katiba mpya. Wananchi hao walitoa mapendekezo hayo baada ya watoa mada za uchokozi Magdalena Mkolere na na Annmarie Mavenjina kutoka FemAct kueleza jinsi ambavyo katiba na sheria za sasa hapa nchi zisivyokidhi haki za kiuchumi na kijamii.

  IPPMedia
   
 2. koo

  koo JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wamekosea sana hapo kwa wakuu wa mikoa na wilaya hawana kazi zaidi yakuligharimu taifa na walipa kodi pasipo tija nashauri kuwe na wakuu wa kanda pekee na makatibu tawala wa wilaya na mikoa wanatosha kusimamia na kutekeleza majukumu yote yakiuongozi katika maeneo husika tunahitaji kupunguza matumizi yasiyo yalazima ili kuelekeza nguvu zaidi kwenye huduma nyeti kwa wananchi
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Idadi ya wabunge kwa nchi yetu ni kubwa mno. Majimbo mengi yameongezwa kwa malengo ya kufaana si kwa misingi ya uwakilishi halisi unaotakiwa.
  Zanzibar na Pemba ukubwa wa majimbo ni sawa na ukubwa wa kata huku bara. Na hivyo ni kuliongezea mzigo mzito Jamhuri ya Muungano. Bora kama walivyopendekeza kila wilaya iwe na mbunge kama ilivyokuwa hapo awali.

  Viti maalum viongolewe kabisa kwa maana hakuna wanachowakilisha ziadi ya kupana fanasi hiyo kwa kujuana na wengi wao kutafanya kile tunachotazamia bungeni bali ni uhudhuriaji na kupokea posho tu.
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ushauri usiozingatia au kuambatana na ushauri wa hasara za uwakilishi huo ni kukurupuka na kudhani kwamba matumizi ya fedha kwa kupanua uwakilishi ndiyo tatizo kubwa kuliko kukosekana kwa fursa pana zaidi za uwakilishi. Hao waliotoa ushauri huo walipaswa kwenda mbele zaidi kutuambia kwamba ukiondoa kupunguza gharama za matumizi, kuna faida gani tutapata ka kuwa na wawakilishi wachache kwa nchi hii kubwa na hali hiyo itachocheaje maendeleo ya nchi.
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  How big is our country? Nenda Kenya na Uganda, angalia geographical areas za nchi hizo, angalia idadi ya wabunge wao halafu jiulize idadi ya wawakilishi wetu kama inakidhi haja maridhawa!
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Sep 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Serikali legelege inafikiri kuwa uwakilishi wa wabunge wengi unaongeza ufanisi zaidi....
   
 7. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  na wewe uwe na huruma bana kila kitu kutetea tu kisa umetumwa
  hivi mbunge aliye na jimbo linayoingilia wilaya mbili anawezaje kufanya uwakilishi wa kueleweka?
  Pili kama mkuu wa wilaya anaweza kuongoza wilaya mbunge anashindwa vipi kuwakilisha wilaya?
  ndio maana wabunge wengine wanaingia bunge kwa miaka mitano na hakuna kutoa mchango
  kuna wafanyabiashara wengi tu wamejificha kwenye ubunge, tupunguze bunge letu liende kihalimashauri
  yaani kila wilaya na mbunge hiyo italeta uwajibikaji na maendeleo
  kwa mfano huko ZANZIBAR wana wabunge 50 kwa eneo lipi la kuwakilisha?
  kuna mikoa mitano ina maana kila mkoa una wabunge 10?
  NJOO DAR KUNA majimbo mangapi ya uchaguzi? linganisha na idadi ya watu?
  unataka kusema hiyo mikoa ya ZANZIBAR ina watu wengi kuliko walio DAR?
  mbona huko kuna mwajimbo machache yaani 7 tu
  hakuna uwiano hii ni siasa tu
   
 8. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  "Tunataka wabunge wawe 150, nusu wanaume na nusu wanawake"- Geez!... Hapo siwaelewi, nildhani wangeshauri kuwepo na vigezo vya kupata wawakilishi competent bila kutazama jinsia...

  Hata hii ya wazee wa miaka 70 katiba itamke wasipewe majukumu ya umma, jamani hapa naona tatizo. Allan Greenspan, Federal Reserve Chairman enzi za G.W. Bush alikua na miaka 80 wakati anastaafu 2006 kwenye public service, na alikua the most respected man kwenye world financial markets. Licha ya kwamba yupo kwenye taifa lenye wasomi lukuki wa kila fani.

  Umri siyo issue, UWEZO ndio tatizo la watanzania wengi wanaokimbilia uongozi wa umma. Maana wengi wao mtaani hawana shughuli inayoeleweka.
   
 9. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  futa kabisa cheo cha mkuu wa mkoa na wilaya!
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ukweli ni kwamba wabunge wawakilishi wanafuja tu resource za serikali sio wa chama tawala wala upinzani
   
Loading...