Wananchi waone mabadiliko katika huduma muhimu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,825
287,846
mbali mbali kufuatia ongezeko hili la makusanyo ya kodi
~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

Biashara na Fedha TRA yakusanya bilioni 320/- Septemba
Shadrack Sagati, Mbozi
HabariLeo; Wednesday,October 24, 2007 @00:01

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mwezi uliopita ilikusanya Sh bilioni 320, ikiwa ni kiasi cha juu ambacho hakijawahi kufikiwa na mamlaka hiyo.

Naibu Kamishna wa TRA, Placidius Luoga alimweleza Waziri Mkuu Edward Lowassa kuwa mamlaka yake imedhamiria kuongeza makusanyo kutokana na kuboresha vitendea kazi, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa ofisi katika maeneo mbalimbali.

Luoga aliyasema hayo wakati Lowassa alipozindua Ofisi ya TRA ya mjini Vwawa ambayo imejengwa na mamlaka hiyo kwa lengo la kuboresha makusanyo ya mamlaka hiyo. Wilaya ya Mbozi inakusanya kati ya Sh milioni 80 na Sh milioni 120 kwa mwezi. Waziri Mkuu yuko ziarani mkoani Mbeya.

“Naamini kuwa kwa kuungwa mkono na serikali malengo ya kukusanya zaidi yatafikiwa,” alisema Luoga.

Alisema ujenzi wa ofisi za namna hiyo unafanywa katika wilaya mbalimbali za Monduli, Ifakara, Masasi, Kibondo na Mbinga. Alisema ujenzi wa ofisi tano kati ya hizo uko katika hatua za mwisho kukamilika.

Luoga alisema mradi huo ulianza Machi 12 mwaka huu na ulikamilika Juni 8, mwaka huu, ikiwa ni muda wa wiki 12 tu. Alisema mradi huo umegharimu Sh milioni 84 na umehusisha kazi za ujenzi wa jengo lenyewe, kibanda cha walinzi, mnara wa matangi ya maji, mashimo ya maji taka, mahali pa maegesho ya magari, slabu ya jenereta, uzio na kazi za maeneo ya nje.

“Jengo hili ambalo lengo lake kuu ni kuhudumia wateja wa Mamlaka ya Mapato wa Wilaya ya Mbozi, ni la kisasa kutokana na vifaa vilivyotumika kulijengea na linakidhi lengo letu la kuwa na mamlaka ya kodi ya kisasa,” alisema Luoga.

Alisema katika kipindi cha miaka 10, TRA imekamilisha ukarabati na ujenzi wa majengo mbalimbali yakiwapo ya makao makuu ya mikoa na wilaya. Alisema baadhi ya vituo vingine vidogo vya mipakani, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa mamlaka wa kuboresha mazingira ya ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Uboreshaji wa majengo umewezekana kupitia mradi wa usimamizi wa kodi ambao umefadhiliwa na wahisani na serikali ya Tanzania, alisema.

Copyright @TSN 2006 All Rights Reserved
 
Nadhani hawa TRA wangeenda kujenga office zao kweny kila mgodi mkubwa kama Bariki na Kahama mining ili waweze kukusanya mapato zaidi na si ukuwanyonga wananchi masikini na kisha kupiga kelele tumeongeza makuasanyo.
Inawezekana ukuaji wa mapato ni kutokana na kuongeza kuodi na sio kutokana na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji na kuwa na vyanzo vipya va kuodi na kukusanya kodi zilizokuwa zinakwepwa,


http://www.nationmaster.com/graph/eco_gdp_percap-economy-gdp-nominal-per-capita
 
Nadhani hawa TRA wangeenda kujenga office zao kweny kila mgodi mkubwa kama Bariki na Kahama mining ili waweze kukusanya mapato zaidi na si ukuwanyonga wananchi masikini na kisha kupiga kelele tumeongeza makuasanyo.
Inawezekana ukuaji wa mapato ni kutokana na kuongeza kuodi na sio kutokana na kuongeza ufanisi katika ukusanyaji na kuwa na vyanzo vipya va kuodi na kukusanya kodi zilizokuwa zinakwepwa,


Countries Compared by Economy > GDP per capita. International Statistics at NationMaster.com

Uzinduzi wa Data Center Leo utasaidia.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom