Wananchi waomba Bunge kumuongezea muda Rais Magufuli madarakani

Massivve

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
274
368
Wananchi wa vijiji vya Bulangwa na Katente mkoani Geita wameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya marekebisho ya muda wa ukomo wa urais kutoka miaka 10 ya sasa hadi miaka 20 ili kumuwezesha Rais Dk. John Pombe Magufuli kuendelea kubakia madarakani kunusuru rasilimali za taifa.

dai.jpg

Wananchi hao wametoa ushauri huo katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mbunge wa jimbo la Bukombe Mh. Dotto Biteko kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa namna anavyosimamia rasilimali za nchi.

Akiwahutubia wananchi Mbunge wa jimbo la Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini Mh. Dotto Biteko amesema kazi ya kupigania rasilimali za taifa inayofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli sio ya lelemama.

Ripoti ya kamati ya pili ya mchanga wa madini (Makinikia) iliyowasilishwa Juni 12 mwaka huu kwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Nehemiah Osoro ilibaini taifa linapoteza shilingi Trilioni 168 kupitia usafirishaji wa mchanga wa madini ya makinikia nje ya nchi kuanzia mwaka 1998 hadi kufikia Marchi mwaka huu.

Ripoti hiyo ya pili ilihusisha baadhi ya Mawaziri wa zamani wa nishati na madini kuhusika na mikataba mibovu iliyopelekea taifa kupoteza rasilimali.

Chanzo:ITV
 
Binafsi Kama ataendelea hivi hivi Naunga mkono hojaKwani kwa Afrika kupata aina ya viongozi wa Magufuli Inachukua miaka 100

Tunachotaka Afrika si kubadili viongozi
Ni kupata kiongozi mwenye nia ya dhati
Pia katiba bora sio kigezo sana, Kwani kuna nchi zinakatiba bora sana, Ila mambo ya ufisadi ndio yanaongezeka,mfano Kenya na Afrika ya kusini

Ishu kubwa Afrika, ni kupata viongozi wenye dhamira ya kweli

Kwa kipindi kifupi, Binafsi niamini mh John Pombe Joseph Magufuli

Ni kiongozi mwenye dhamira ya dhati kabisa
Kutoka moyoni Japokuwa kama binadamu naye ana mapungufu yake

Kwa sasa Tanzania tumepata kiongozi, Rais
Asanteh Mungu

Mungu mbariki Magufuli
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
 
Walioshikilia bango ni makada wa ccm .
Nafikiri kwenye kichwa cha habari wangetumia neno wanaccm na sio neno wananchi.
Kutumia neno wananchi badala ya neno makada wa ccm kinawafanya wananchi wanaojielewa wa maeneo hayo kuendelea kuichukia Serikali kwa kuamini kuwa inampango wa kukiuka katiba ya jamhuri ya Tanzania.
 
Watu hawajui kwanin kuna ukomo wa madaraka. Rais hawezi ishi milele, hivyo maana yake akija rais kilaza au 'mpole' kama yule wa awamu ile, nchi inaweza kufilisika. Ukomo wa miaka 10 tu ni muhimu ili tukipata rahisi wa bahati mbaya, tumvumilie amalize miaka yake aondoke.
 
Mimi atakapofanikiwa kufukua makaburi kama lile la Kiyeyeu pale Iringa njiani basi nitaunga mkono hata awe mfalme.
 
Wananchi wa vijiji vya Bulangwa na Katente mkoani Geita wameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya marekebisho ya muda wa ukomo wa urais kutoka miaka 10 ya sasa hadi miaka 20 ili kumuwezesha Rais Dk. John Pombe Magufuli kuendelea kubakia madarakani kunusuru rasilimali za taifa.

dai.jpg

Wananchi hao wametoa ushauri huo katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mbunge wa jimbo la Bukombe Mh. Dotto Biteko kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa namna anavyosimamia rasilimali za nchi.

Akiwahutubia wananchi Mbunge wa jimbo la Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini Mh. Dotto Biteko amesema kazi ya kupigania rasilimali za taifa inayofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli sio ya lelemama.

Ripoti ya kamati ya pili ya mchanga wa madini (Makinikia) iliyowasilishwa Juni 12 mwaka huu kwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Nehemiah Osoro ilibaini taifa linapoteza shilingi Trilioni 168 kupitia usafirishaji wa mchanga wa madini ya makinikia nje ya nchi kuanzia mwaka 1998 hadi kufikia Marchi mwaka huu.

Ripoti hiyo ya pili ilihusisha baadhi ya Mawaziri wa zamani wa nishati na madini kuhusika na mikataba mibovu iliyopelekea taifa kupoteza rasilimali.

Chanzo:ITV
Ukisoma tu sura zao utajua nini maana yake. Vitambaa kichwani, tshirt za mgao na za chagula, na vitenge kiunoni kama wanatoka shamba
 
Back
Top Bottom