~~Wananchi wangu eeeeh, mimi Rais wenu, eeeh~~ (continued..)

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
~~ # Wananchi wangu eee, - eeeeeh?
~~# Mimi Nahodha wenu, - eeeeh
~~# Pia kiongozi wenu, - eeeeh
~~# Sina nguvu tena, - eeeeh
~~# Ya kuendesha injini, - eeeh



~~# Uongozi si lelema, - eeeh
~~# Kuna ma EPA, - eeeh
~~# Mwafaka wa Muungano, - eeeh
~~# Kuna ma OIC, - eeeh
~~# Mahakama ya Kadhi, -eeeh
~~# Madai ya walimu, - eeeh
~~# Na mauaji ya Albino, -eeeh


~~# Yote yamenishinda, - eeeh
~~# Na nguvu sina tena, - eeeh
~~# Nabaki kuwa msema, eeeh
~~# Kuwapotezea muda, eeeh


~~# Mtajiju akina mama, - eeeh
~~# Mtajiju akina baba, - eeeh
~~# Mtajiju Mashekhe, - eeeh
~~# Mtajijua Maaskofu, - eeeh
~~# Mimi chaguo la Mungu, - eeeh

~~# Kutoka safari za mbali, - eeeh
~~# Na hii ni hotuba yangu, - eeeh
~~# Na hatma ya majukumu, - eeeh
~~# Kama mnamachungu, - eeeh
~~# Basi niondoeni, - eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeh!!!!




Mwangwi wa Handaki
 
Last edited:
kwi kwi kwi...

angalau JF tuna SteveD wetu anaweza kutupatia hili...... na hii ijumaa ilivyojaa mambo na hotuba za muungwana, basi tu....
 
JK: "Watanzania eh"

WTZ: "Eh"

JK: "Mimi Rais wenu!"

WTZ: "eh!"

JK: "Sina nguvu tena!"

WTZ: "Eh"

JK: "Ya kukamata mafisadi"

WTZ: "Eh"

JK: "Mafisadi ni wajanja"

WTZ: "Eh"

JK: "Wamekomba Benki Kuu"

WTZ. "Eh" kwa shauku!

JK: "Wamelangua na Rada"

WTZ. "Eh" kwa shauku!

JK: "Wameiba Meremeta"

WTZ. "Eh" kwa shauku!

JK: "Wamechota nayo EPA"

WTZ. "Eh" kwa shauku!

JK: "Sasa kimbieni!

Watanzania kila mmoja anaanza kutimka kivyake na mwenye kuweza kufanya ufisadi zaidi anaendelea kufanya tu kwani rais keshashindwa; na kupelekea ufisadi kuendelea kukomaa siku hadi siku. Hivyo ndivyo anvyoonekana Rais Kikwete.
 
Fisadi hawezi kumkamata fisadi mwenziye. Ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya, mabilioni ya Kikwete, Nitaipitia upya mikataba yote ya uchimbaji wa madini ili kuhakikisha Tanzania inanufaika na rasilimali zake. Kumbe ilikuwa ni usanii tu wa kuingia Ikulu hana uwezo wa kuiongoza nchi na matokeo yake nchi inayumba na hakuna dalili za ahueni yoyote. Chaguo la Mungu kumbe ni chaguo la mafisadi ambo wanaendelea kupeta na mali zao za kifisadi. Halafu anamalizi hotuba yake kwa kusema Mungu ibariki Tanzania!!!! :( Aibariki kwa lipi kwa mafisadi!!!!! Au anasubiri Mungu aje kuwakamata mafisadi!!!! :(
 
Very funny and very interesting. Hivi Chiligati huwa haji huku? Maana kama Mbowe alisema Rais kashindwa kuongoza nchi na asipewe kipindi cha pili ikawa mzozo mpaka kutukanana. Huku akija si ndio atameza viwembe? Teh teh teh!
 
Nimeshangazwa kusoma kwenye vyombo vya habari kuwa hadi leo, hakuna mtu yeyote aliyechukuliwa hatua za kisheria kwa kuiba hela za epa.

Kikwete amendelea tena kuboronga na kudidimiza mioyo ya watanzania kwa kutokuwa na meno ya kupambana na ufisadi nchini.

Eti ameongeza muda usiojulikana kwa mafisadi hawa kurudisha pesa? Ni nani hawa na kwanini hawachukulii hatua? Nini kina mshinda huyu jamaa?

Amenitibua, amenihudhunisha, amenifedhehesha!
 
Stev,hako kawimbo kaminikumbusha zamani utotoni.Nilikuwa nafanana na avatar yako enzi hizo.kumbe nyimbo za utotoni zi maana!teh teh teh!
 
Hivi hawa waandishi wa habari wal;ikuwa hawana hata tape recorder au chombo chochote cha mawasiliano kunasa hotuba ya rais na kuandika japo machache tu aliyoyasema.

Au ndio usalama wa Taifa waliwabana vilivyo na vitisho kibao.
 
Kinachomshinda Rais ni kwamba kwenye ripoti nzima ya EPA inaonekana yeye aliinitiate baadhi ya watu kuchukua zile Fedha na anahofu akiwapeleka mahakamani ukweli wote utajulikana.

Kwahiyo anachokifanya ni kuwachuja jamaa zake na awabakishe ambao anajua kwamba hawatamzuri ndio apeleke kesi mahamani.

Its real weird inn
 
Kinachomshinda Rais ni kwamba kwenye ripoti nzima ya EPA inaonekana yeye aliinitiate baadhi ya watu kuchukua zile Fedha na anahofu akiwapeleka mahakamani ukweli wote utajulikana.

Kwahiyo anachokifanya ni kuwachuja jamaa zake na awabakishe ambao anajua kwamba hawatamzuri ndio apeleke kesi mahamani.

Its real weird inn
 
Stev,hako kawimbo kaminikumbusha zamani utotoni.Nilikuwa nafanana na avatar yako enzi hizo.kumbe nyimbo za utotoni zi maana!teh teh teh!

....na bado tuko kwenye beti ya pili tu, chorus bado haijapamba!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom