Wananchi Wanataka Maji; Idd Azan Kawapa 50000 za Maji ya Chupa

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,830
2,000
Idd Azan amethibitisha namna CCM imajaa wabunge vihiyo.

Majira, Gazeti Huru la Kila Siku, inaripoti kuwa katika maeneo fulani Jijini Dar Es Salaam Mbunge wa Kinindoni, Idd Azan alikutana na genge la wafuasi wa CUF wakimsindikiza Diwani wa Kata yao.

Wakiwa kwenye msafara huo kwa kutumia TZ11 zao, walikutana na Idd Azan, wakapaza sauti kuomba maji. Kwa ujuha, ama ukihiyo, ama pupa, ama sifa, mzee mzima aliingia mfukoni akachomoa Tshs. 50,000 ili vijana wa CUF wanunue maji ya kunywa.

Kumbe jamaa walikuwa wanataka miundombinu ya maji, na si fedha.

Wakachomoa.

Wakamrudishia mpunga wake.

Ikawa aibu funga-mwaka kwa Idd Azan.

Source: Majira
 

Kipre tchetche

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
238
0
Hawajui kipao mbele chao kwa taifa na kwa
wananchi waliowapa Kura na kwa wabunge
walio wengi wa ccm walichakachua nafasi
sasa kipao mbele chao ni chama chao na
kweli ni vihiyo sana hawa.
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,523
2,000
toka lini CCM wanaelewa nini wananchi wanataka ndo maana wanakuwa wezi wa kura maana hawajui nini wananchi wanataka
 

kany

Member
Feb 20, 2010
53
0
Hii inasikitisha kwa kweli! Lakini inawakilisha aina ya viongozi tulio nao katika nchi hii
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom