Wananchi wanaoishi jirani na Bwawa la Nyumba ya Mungu wametakiwa kuondoka haraka kutokana na kujaa maji na hatari ya kupasuka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,481
9,242
BONDE la Maji la Mto Pangani limewatahadharisha wananchi wanaoishi jirani na Bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, kuondoka haraka kutokana na kujaa maji na kufikia mita 688.91 kutoka usawa wa bahari.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Moshi, Mkurugenzi wa Bonde la Maji la Mto Pangani, Segule Segule, alisema kuwa bwawa hilo kwa sasa tayari limeshafikia kiwango cha ujazo unaotakiwa ambapo kwa kawaida likifikia lazima litoroshe maji.

Segule alisema kuwa maji hayo yasipotoroshwa mapema athari yake ni kubwa kuliko, kwani yanaweza kuvunja bwawa na kusambaa kwenye makazi ya watu.

“Lengo likishafika tunaruhusu maji yatoroke kwani tusipoyaruhusu yaweza kuvunja bwawa na kusambaa kwenye vijiji vinavyolizunguka na kuleta maafa kwani maji hayazuiliki,” alisema Segule.

Alisema kuwa mvua zilizoanza kunyesha mwishoni mwa mwaka jana na kuunganisha hadi mwaka 2020, zilijaza bwawa na kuna dalili ya kunyesha mvua nyingi zaidi.

Segule alisema kuwa wametoa taarifa kwa wenzao wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuongeza uzalishaji wa umeme ili maji yaendelee kupungua katika bwawa hilo.

Alisema kuwa mvua bado zinaendelea kunyesha huenda zikawa nyingi zaidi kuliko mvua za masika.

“Kwa hali ya kawaida mvua zilizonyesha mwaka jana zimetosheleza kabisa, na kwamba zaidi ya miaka 10 mfululizo bwawa hilo halijawahi kujaa,” alisema Segule.

Alisema kuwa Bwawa la Nyumba ya Mungu kuanzia Januari 1, mwaka huu tayari limeshafikia kiwango kinachotakiwa.

“Tulipoona mwelekeo wa bwawa hilo kujaa tulitoa taarifa kwa wakuu wa wilaya ambazo zinazunguka bwawa hilo ili kutoa tahadhari kwa wananchi kuondoka mapema kabla ya madhara hayajatokea,” alisema Segule.

Alisema kuwa mwelekeo wa bwawa mwaka huu hautabiriki kutokana na kwamba bado mvua za vuli hazijaanza.

Alisema kuwa timu ya wataalamu wa bonde hilo wako katika maeneo ya bwawa kufanya utafiti kama mvua zitaendelea wanaweza kudhibiti vipi bwawa hilo lisiathiriwe.
 
Kweli sisi mijitu mweusi sijui tuna tatizo gani kama bwawa lina overflow facilities linapasuka kwasababu gani? Kwanini zisifanye kazi kama lilivyisanifiwa? Kwama kingi zilishuka kina hao wanaojiita bonde walifanya nini? Au kazi yao na kuleta tu tahayari kwa wananchi? Watuambie vitu vya maanayake kama either capacity ya overflow facility ni ndogo kuliko inflow ndio tutawaelewa.
Kama sio hivyo wanahofia nini? Kingo zina nyufa au kunanini? Kama zina nyufa walifanyanini kabla ya mvua? Hakila nina maswali mengi kuliko haya maelezo ya blaa blaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo Kama overflow isipofanya kazi maana yake hayo Ni mafuriko.

Kwa akili yako overflow ilkizidiwa nini kinafuata? Katika bwawa la Mtera tanesco wamewatahadharisha watu wanaoishi chini ya bwawa hilo uwezekano wa kukumbwa na mafuriko kwa sababu wanafungulia maji ili yapungue bwawani.

Hali kadhalika katika bwawa la Nyumba ya Mungu maji yamefunguliwa katika kiwango chake cha mwisho na overflow imezidiwa, kinachofuata ni maji kusambaa katika makazi ya watu.

Sasa hoja yako nini?
 
Kuna kimstari kinasema, wamewaambia Tanesco waongeze uzalishaji wa Umeme ili maji yapungue. Sijui nimeelewa sawa sawa!!?
 
TAHADHARI INATOLEWA KIENYEJI NAMNA HII HAKUNA HATA MSISITIZO
Wapare wabishi mnatisha Sasa waweke msisitizo gani? Lo nchi hi haya makabila mawili waha na wapare kwa ubishi hatari halafu wote wafupi sio babu yao alikuwa mmoja
 
BONDE la Maji la Mto Pangani limewatahadharisha wananchi wanaoishi jirani na Bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, kuondoka haraka kutokana na kujaa maji na kufikia mita 688.91 kutoka usawa wa bahari.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Moshi, Mkurugenzi wa Bonde la Maji la Mto Pangani, Segule Segule, alisema kuwa bwawa hilo kwa sasa tayari limeshafikia kiwango cha ujazo unaotakiwa ambapo kwa kawaida likifikia lazima litoroshe maji.

Segule alisema kuwa maji hayo yasipotoroshwa mapema athari yake ni kubwa kuliko, kwani yanaweza kuvunja bwawa na kusambaa kwenye makazi ya watu.

“Lengo likishafika tunaruhusu maji yatoroke kwani tusipoyaruhusu yaweza kuvunja bwawa na kusambaa kwenye vijiji vinavyolizunguka na kuleta maafa kwani maji hayazuiliki,” alisema Segule.

Alisema kuwa mvua zilizoanza kunyesha mwishoni mwa mwaka jana na kuunganisha hadi mwaka 2020, zilijaza bwawa na kuna dalili ya kunyesha mvua nyingi zaidi.

Segule alisema kuwa wametoa taarifa kwa wenzao wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuongeza uzalishaji wa umeme ili maji yaendelee kupungua katika bwawa hilo.

Alisema kuwa mvua bado zinaendelea kunyesha huenda zikawa nyingi zaidi kuliko mvua za masika.

“Kwa hali ya kawaida mvua zilizonyesha mwaka jana zimetosheleza kabisa, na kwamba zaidi ya miaka 10 mfululizo bwawa hilo halijawahi kujaa,” alisema Segule.

Alisema kuwa Bwawa la Nyumba ya Mungu kuanzia Januari 1, mwaka huu tayari limeshafikia kiwango kinachotakiwa.

“Tulipoona mwelekeo wa bwawa hilo kujaa tulitoa taarifa kwa wakuu wa wilaya ambazo zinazunguka bwawa hilo ili kutoa tahadhari kwa wananchi kuondoka mapema kabla ya madhara hayajatokea,” alisema Segule.

Alisema kuwa mwelekeo wa bwawa mwaka huu hautabiriki kutokana na kwamba bado mvua za vuli hazijaanza.

Alisema kuwa timu ya wataalamu wa bonde hilo wako katika maeneo ya bwawa kufanya utafiti kama mvua zitaendelea wanaweza kudhibiti vipi bwawa hilo lisiathiriwe.
Likipasuka
ccm lazima wabebe lawama zote
 
Iwapo bwawa lilisanifiwa vema hakutakiwa kuwa na uwezekano wa kupasuka. Mfumo wa kuachilia maji unatakiwa kuweza kulisalimisja.

Ila uwezekano wa mafuriko downstream haukwepeki mvua zikizidi. Ni mafuriko ambayo yangetokea hata bila bwawa kuwepo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom