Wananchi, Wanafunzi na Zimamoto washirikiana kuzima moto Mlima Kilimanjaro

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka (CAWMSO) amewaomba wanafunzi waliopo chuoni kushiriki kikamilifu katika kuzima moto katika hifadhi ya Kilimanjaro.

Mamlaka za Hifadhi za Taifa ilisema sehemu ya msitu wa mlima Kilimanjaro ilianza kuungua tangu jana mchana na waliendelea juhudi za kuuzima.

Kwa kuwa moto bado unaendelea Mkuu ametaka kuongeza nguvu kwa kuwaomba wanafunzi hao kushiriki kuanzia leo ili kuudhibiti moto huo kwa haraka.

Wanafunzi wametakiwa kuvaa suruali ya kombati ya kijani na buti na tisheti za chuo.

1602477289411.png
 
Moto unazimwa na wataalamu sio wanafunzi kati ya ajali mbaya za Moto ni pamoja na Moto wa msituni msipojua kitu mtazungukwa na kuteketea moto wa California wiki iliyopita uliwazunguka fire fighter kadhaa mlima unaingiza pesa nyingi kuweni na vifaa thabiti vya kuzimia Moto wa maporini na mlimani acheni ujanja ujanja kwenye Mambo ya msingi, watu wa Moto mkoa KLM na Arusha wahusike kuzima Moto sio hao wanafunzi.
 
Mlima unaingiza pesa nyingi sana.

Kulitakiwa kuwe na fire department special kwa ajili ya mlima na wawe na vifaa special vinavyofika kokote wakati wa janga la moto.

Wanafunzi hawataweza hiyo kazi kwasababu hawajawa-trained kwa hiyo kazi.

Fire department ndo wajibu wao huo.
 
ndio tujiulize sasa hizo "pesa nyingi sana" zipo wapi ?
 
Their lunch/dinner package will contain variety of meat from various animal species found around the mountain including kitimoto poriii (aka Ngiri) ....hahaaa... just joking

all the best to the fire fighters, as this is tourism season
 
Mamlaka husika zihusike kikamilifu.. asubuhi Mr Allan Kijazi anahojiwa na Azam TV wala haoneshi kushitushwa na hali inayoendelea... wajitolee na wakawajibike
 
Moto unazimwa na wataalamu sio wanafunzi kati ya ajali mbaya za Moto ni pamoja na Moto wa msituni msipojua kitu mtazungukwa na kuteketea moto wa California wiki iliyopita uliwazunguka fire fighter kadhaa mlima unaingiza pesa nyingi kuweni na vifaa thabiti vya kuzimia Moto wa maporini na mlimani acheni ujanja ujanja kwenye Mambo ya msingi, watu wa Moto mkoa KLM na Arusha wahusike kuzima Moto sio hao wanafunzi.
Umeongea point kila kitu ni utalaamu aisee niliona kwenye muvi moja aliyocheza jamaa wa THE GODS MUST BE CRAZY walifungwa miguu na mikono wakatupwa porini halafu Moto ukawashwa Moto ulikuwa na speed hatari huku wakijaribu kukimbia lakini Moto ulizidi kuwakaribia jamaa akaona isiwe tabu akakata kamba akaenda kuchukua kipande Cha kuni akakimbia mbele akaenda kuchoma kule mbele Moto wa mbele ukaendelea kuwaka kwenda mbele Moto wa nyuma ukaishia pale Moto wa mbele ulipoanzia huku washikaji wameingia kule mbele Moto umeshazima tayari.​
 
Mlima unaingiza pesa nyingi sana.

Kulitakiwa kuwe na fire department special kwa ajili ya mlima na wawe na vifaa special vinavyofika kokote wakati wa janga la moto.

Wanafunzi hawataweza hiyo kazi kwasababu hawajawa-trained kwa hiyo kazi.

Fire department ndo wajibu wao huo.
Nyie nyie ndio mlioshangilia Mhe. KANGI LUGOLA kutumbuliwa maaana alikuwa na maono kama yako anunue Ndege ya kuzima moto hata Dronne za Kisasa za kuzima moto kama huo juu ya Milima, leo mnarudi Rivasi kulilia Vifaaa vya Kisasa! Kwakweli aliyeturoga alikufa kifudifudi.

Pumzika salama mtaani brother Afande Kangi Lugola, naaamini zile Drone zako na Videge vya kuzima moto Leo vingeonyesha kazi yake lkn mbadala wake tumetuma Wanafunzi wakiwa kwenye fulana za Chuo!

Mungu wasimamie watoto wetu huko Msituni huku tukisubiri magari ya Zimamoto yakweeee Mlimani kwenye msitu kutoa msaada!
 
Moto unazimwa na wataalamu sio wanafunzi kati ya ajali mbaya za Moto ni pamoja na Moto wa msituni msipojua kitu mtazungukwa na kuteketea moto wa California wiki iliyopita uliwazunguka fire fighter kadhaa mlima unaingiza pesa nyingi kuweni na vifaa thabiti vya kuzimia Moto wa maporini na mlimani acheni ujanja ujanja kwenye Mambo ya msingi, watu wa Moto mkoa KLM na Arusha wahusike kuzima Moto sio hao wanafunzi.
Asante Mkuu ahawa MWEKA wanataka kutuletea Majanga Mengine
 
Nimekumbuka huko huko mlima Kilimanjaro mkuu, askari wa KINAPA na PT walikuwa wanasaidiana kusomba watu na kuwapeleka juu huko kuzima moto... bhas ikifika time hiyo vijiweni kunakuwa kweupee watu hawakai.
Watu Wanajificha Ndani Kuepuka Hiyo Kadhia Kusombwa Wakati Huna Ratiba Ya Kwenda Kuzima Moto 😅😄😃
 
Umeongea point kila kitu ni utalaamu aisee niliona kwenye muvi moja aliyocheza jamaa wa THE GODS MUST BE CRAZY walifungwa miguu na mikono wakatupwa porini halafu Moto ukawashwa Moto ulikuwa na speed hatari huku wakijaribu kukimbia lakini Moto ulizidi kuwakaribia jamaa akaona isiwe tabu akakata kamba akaenda kuchukua kipande Cha kuni akakimbia mbele akaenda kuchoma kule mbele Moto wa mbele ukaendelea kuwaka kwenda mbele Moto wa nyuma ukaishia pale Moto wa mbele ulipoanzia huku washikaji wameingia kule mbele Moto umeshazima tayari.​
Watu wengi tuliokua tunafanya kazi za Moto hasa wa meli,oil lig au majumbani wataalamu walitusihi kwenda kuzima Moto wa msituni ni hatari kuliko maelezo inatakiwa upate Elimu ya kuanzisha Moto ili ubadili uelekeo na jinsi upepo ilivyo sio umewashinda hamuwezi hata hii mbinu ndogo sema huku wanachukulia poa tuu kila kitu tunawaangalia maana maamuzi ya kitaalamu yanategemea wanasiasa..
 
Back
Top Bottom