Wananchi wanabomolewa nyumba zao kwa usimamizi wa serikali. Nani mtetezi wao


Gurudumu

Gurudumu

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2008
Messages
2,351
Likes
11
Points
135
Gurudumu

Gurudumu

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2008
2,351 11 135
Vitendo vya kuboa nyumba za wananchi ili kupisha miradi ya wawekezaji vinaongezeka hapa Tanzania. Takribani kila wiki kuna taarifa za wananchi au mwananchi kubomolewa nyumba bila hata mali zake kuhifadhiwa. Kisha wanatelekezwa bila kupatiwa hifadhi yoyote.

Hata wakilalamika, vyombo vya habari huripoti lakini hakuna usaidizi wowote kutoka serikalini. Serikali huwa upande wa mwekezaji na ikibidi humpatia mwekezaji ulinzi wa polisi ili aweze kuwabomolea wananchi. Sababu nyingi za migogoro hii huwa ni dhuluma kwa wananchi, kwa maana ya kupewa fidia kidogo kuliko thamani halisi ya ardhi na mali zao

Nani mtetezi wa wananchi? Wananchi watapata haki yao wapi? Kisa hiki hapa chini ni mojawapo tu
[TABLE]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
[TR]
[TD]
Wakazi Kigamboni walilia nyumba zaona Hellen Ngoromera[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] [TABLE]
[TR="bgcolor: #ffffff"]
[TD="bgcolor: #ffffff"] WANANCHI 105 wa Mtaa wa Minondo, Kata ya Somangila, Kigamboni jijini Dar es Salaam hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa kupisha mradi wa nyumba za maofisa ulinzi na usalama unaotekelezwa na Kampuni ya Avic Coastal Land.

Ujenzi wa nyumba hizo katika eneo la Amani Gomvu, ambapo kwa sasa mradi huo upo katika awamu yake ya kwanza ya utekelezaji, unalenga kujenga nyumba kwa ajili ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na vyombo vingine vya usalama.
Wakizungumza na Tanzania Daima, wakazi hao walisema hali hiyo inawafanya waishi kwa tabu na wengi wao wanasaidiwa na majirani sehemu za kulala.
Yusuph Hamidu, alisema kubomolewa kwa nyumba zao kumetokana na wao kukataa fidia iliyotolewa kuwa ndogo, hivyo kusababisha mgogoro wa ardhi kati yao na kampuni hiyo ya uwekezaji.
“Sisi tupo hapa kihalali, iweje mwekezaji aje na kuchukua ardhi bila ridhaa yetu? Je, uko wapi utawala wa sheria?... Tathmini juu ya ardhi, nyumba na mazao ulifanyika mwaka 2007 na tuliambiwa kuwa tutalipwa sh 700,000 kila heka na ulipwaji ulifanywa kuanzia mwaka 2011.
“Aprili 24 mwaka huu wakati tumelala tulishtuka kuona nyumba zetu zikibomolewa kwa kutumia tingatinga huku vitu vyetu vikiharibiwa na baadhi ya askari polisi wa jiji kupora mali hizo,” alisema mkazi huyo.
Naye Hadija Said (41) aliosema yeye na watoto wake 11 wanaishi jikoni kwa msamaria mwema ambaye aliwapatia hifadhi na kwamba nyumba yake iliyovunjwa ilikuwa na vyumba vinane.
Hata hivyo, Diwani wa Kata ya Somangila, Aisha Mpanjila, alikataa kuzungumzia suala hilo na kusema kuwa mkuu wa wilaya ndie mwenye taarifa za kina juu ya suala hilo.
Barua kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke yenye kumbukumbu namba TMK/MD/K.II/31/20 ya mwaka jana, ambayo nakala yake ilipatikana, ilimtaarifu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Somangila juu ya utekelezaji wa zoezi zima la kuwaondoa wakazi hao na kupisha mwekezaji wa Avic Coast Land Development Co. Ltd.
Mradi huu wa nyumba za majeshi ya ulinzi na usalama ulipitishwa na Kituo cha Uwekezaji na kupewa hati namba 061021 ya Novemba 2011 kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Goodluck ole Medeye alisema hana taarifa kuhusu uvunjaji huo.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 

Forum statistics

Threads 1,273,088
Members 490,268
Posts 30,470,878