Wananchi wamwomba Kikwete amtimue DC Biharamulo

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Umoja wa wakulima na wafugaji wa kata ya Bisibo, wilayani Biharamulo mkoani Kagera, wamemuomba Rais Jakaya Kikwete kumtimue Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Richard Mbeo, kwa madai ya kushiriki kuchochea mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Nyalwambu na Kiruruma.

Akizungumza na NIPASHE, Mwenyekiti wa Umoja huo, Dotto Mchelemchele, alisema mkuu huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa CCM, walishirikiana kuwatapeli wakazi hao kwa kuwachangisha fedha nyingi kwa maelezo kuwa ni za kuwapatia maeneo ya kuishi na kuendeleza shughuli za kibinadamu.

Alisema walichangishwa zaidi ya shilingi milioni mbili kwa ajili ya kuwamilikisha eneo ambalo kwa sasa linasemekana kuwa ni hifadhi.

Alisema Desemba 17, mwaka jana, mkuu huyo pamoja na viongozi mbalimbali akiwa ameambatana nao, walienda kijijini Nyalwambu kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wa eneo hilo baada ya kuachwa na wahamiaji haramu kutoka nchi ya jirani ya Rwanda.

Alisema wakulima na wafugaji kutoka maeneo mbalimbali walihamia Nyalwambu ambapo uongozi wa mkoa pamoja na uongozi wa CCM waliwataka wananchi hao kuchangia fedha kwa ajili ya kumilikishwa maeneo.

Mchelemchele alisema Machi 12, mwaka huu walipata mwaliko wa mkutano wa kijiji cha Nyalwambu na ndipo uongozi wa serikali ya kijiji na viongozi wa CCM, walifika kama mashahidi katika makabidhiano ya ardhi kwa wananchi hao.

Alisema mwenyekiti wa serikali ya kijiji alitoa agizo la kuwaruhusu wananchi wa Nyalwambu walipe viingilio katika serikali ya kijiji ya Sh. 40,000 na Sh. 50,000 kila mtu kwa ajili ya eneo alilokatiwa.

Alisema katika hali ya kushangaza, Mkuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya viongozi wa CCM, wamewataka kuondoka eneo hilo kwa madai kuwa ni hifadhi ya wanyama pori.

Alipotafutwa na NIPASHE, Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Mbeo ili azungumzie mgogoro huo, alisema kuwa apigiwe simu baadaye kwa madai kuwa yuko kwenye kikao.

Alipopigiwa tena alisema kuna jambo analishughulikia hivyo hayupo tayari kuzungumzia jambo lolote na kukata simu.

Kwa upande wake, mbunge wa Biharamulo, Dk. Antony Mbassa (Chadema), alisema mgogoro huo ni mkubwa na unakuzwa na uongozi wa Wilaya na baadhi ya viongozi wa CCM.

Alisema viongozi hao kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya wamewatapeli wananchi kwa kuwachangisha fedha nyingi kwa madai ya kuwapa maeneo ya kuishi lakini bila kuwapa risiti jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Diwani wa kata ya Bisibo, Josephat Kayamba, alikiri wananchi hao kuchangishwa, hata hivyo alisema wanatakiwa kuondoka kwa nguvu.

Alisema uongozi wa wilaya ndiyo chanzo cha mgogoro huo kwa kudai eneo hilo ni la hifadhi ya wanyama pori wakati hapo nyuma lilikuwa eneo la kuishi watu tena wahamiaji haramu kutoka Rwanda.

Chanzo: Nipashe
 
Mwanzo » Habari

NA MWANDISHI WETU

7th December 2014

email.png

B-pepe
printer.png

Chapa

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Sasa eneo walikuwa wanaishi wahamiaji 'haramu' wameondolewa bado watu wanataka walikalie kinguvu. Ni lazima maeneo ya hifadhi yalindwe kwa manufaa ya vizazi vilivyopo na vijavyo
 
Usitumie masaburi kufikiri.
 
biharamulo mmezidi uchawi na majungu,mnarogana kila siku na hiyo wilaya mmeshindwa kuiendeleza japo ilianzishwa na mkoloni,mna majungu
 
Kila siku liwe jema liwe baya kwako ni baya tu,hebu twambie wewe umeendeleza wapi?
 
Hawa wananchi wa Bihalamuro wanamwombaje mwajiriwa wao badala ya kumpa maagizo
 
Back
Top Bottom