Wananchi wamuomba Rais Magufuli kuingilia kati vitendo vya udhalilishaji vinavyofanya na Jeshi la polisi

bhokesa

Senior Member
Feb 23, 2018
138
116
Wananchi wamuomba Rais Magufuli kuingilia kati vitendo vya udhalilishaji vinavyofanya na Jeshi la polisi.

Jeshi letu la polisi limekosa dira. Vitendo hivi wanavyowafanyia wananchi ni hatari kwa mahusiano kati ya polisi na raia.

------------
Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Kambarage Kata ya Buhalahala wilayani Geita katika Mkoa wa Geita wanaomba msaada kutoka kwa Rais Dk. John Magufuli kutokana na vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji vinavyofanywa na askari wa Jeshi la Polisi.

Wakizungumza katika mahojiano maalum na Muungwana Blog, walieleza Mwaka 2003, wananchi kushirikiana na wafadhili Mradi wa Plan walifanikisha kujenga kisima cha maji kwa ajili ya matumizi ya wakazi hao, ambapo kila Kaya ilichangia kiasi cha shilingi 1000/= , jambo lililopelekea kupungua kwa kero ya maji.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kambarage Bw. Mfaume Habali, alifafanua kuwa uongozi wa Shule binafsi ya sekondari ya Waja uliunganisha mabomba kutoka shuleni hadi kisimani kwa ajili ya kuvuta bila kutoa taarifa kwenye uongozi wa serikali, jambo lililopelekea wananchi kugomea zoezi hilo.

Habali, alisema baada ya kuibuka mgogoro kati ya Shule ya Waja na wananchi taarifa zilimfikia Mkuu wa Wilaya na kuitisha ambapo aliitisha Mkutano wa Hadhara wakawa wamemaliza tofauti, lakini baada siku kadhaa wakandarasi wa mabomba walifika tena kuendeleza zoezi la kuvuta maji kutoka kisimani hapo, jambo lililopelekea wananchi kupiga mwano bila msaada.

"Mnamo Februari 22, mwaka huu polisi walivamia hapa mtaani na kuanza kuwapiga wananchi ovyo huku baadhi ya wakina mama walijikuta walinyanyaswa kudhalilishwa, ambapo wengine waliacha miji yao na kukimbia kutafuta sehemu yenye usalama zaidi," alisema.

Mwenyekiti huyo alimpigia simu Mkuu wa Wilaya kumueleza juu ya vitendo vinavyofanywa na askari hao, ambapo mkuu wa wilaya alimpa jibu kwa njia ya ujumbe mfupi katika simu yake uliosomeka "Hakuna Hati Miliki ya Mitaa, nimewatuma mimi mwenyewe na yeyote atakayepinga hata kama ni wewe watakukamata. Agizo la Halmashauri haliwezi kupingwa na mtaa na wewe ni chanzo cha kuvuruga zoezi hilo".

Bw. Habali aliwataja baadhi ya wahanga katika tukio hilo, kwa wanawake ni Justa Fungameza na Fidelina Petro, baada ya kupigwa kuvulishwa nguo kisha kushikwa kifuani wakiwa hawana mavazi, huku kwa upande wa wanaume ni Msika Stima aliyepigwa na kitako cha bunduki kichwani kisha kuzimia, Reonard Lutama, Daud Stephano, Ephraim Odelo wao walipigwa na kushikiliwa kisha kupangiwa siku ya kuripoti mpaka Ijumaa iliopita waliambiwa warudi kituoni mpaka watakapowapatia sababu huku anaye washtaki hafiki na kutojulikana.

Chanzo: Muungwana
 
Wananchi mbumbumbu, malofa, wasiojifahamu, wajinga, can't think, hawajui lolote duniani , Tanzania ! Hao wana baraka zake... elfu tano ya brush, nyofoa matairi, piga wapinzani.... indication kuwa huyo wanayemuomba ndiye anawatuma!
 
Alie watuma na kuwabariki tena ndio mnataka aingilie kati?
Mmeshakoswa vya kumuomba Malaika mkuu.
 
Back
Top Bottom