Leo nilipita katika ofisi ya Kurasini kushughulikia issue yangu ya bima kwenye mida ya saa tano hivi, nilichokikuta ni foleni ya Watanzania na kila uliyemuuliza alisema amekuja kujiunga na vifurushi.
Cha kushangaza wapo niliowakuta ambao wanasema wameanza kufuatilia tangu jana na kikubwa ni kukamilisha mahitaji ili waweze kujiunga na kufurahia huduma.
Watanzania wameanza kufuata uhalisia na kuachana na Siasa, nadhani Zitto ambaye yeye na familia yake wana bima tena labda za private ambazo gharama zake ni kubwa, aache kuwahadaa wananchi, awaache wajiunge na wajikomboe kwa bima ya Tsh 192,000.
Zitto mshahara wake kama Mbunge tu ni mamilioni, hapo usihesabu zile pesa anazopewa na wadau wake, kwake yeye huduma ya afya sio tatizo hata kama ikibidi atibiwe kwa milioni 2 kwa siku anaweza kumudu, vipi jamani tunawadanganya Watanzania.
Ifike mahali tumuache mwananchi aamue kutibiwa kwa 192,000 kwa mwaka, kwa hesabu za haraka haraka ni kama Shilingi 600 hivi kwa siku, tena hapa niliona hadi ma CT Scan sijui ma MRI yamo mule.
Siasa za maendeleo nadhani ni muhimu kuliko siasa za kuwadanganya Watanzania, ili upate madaraka.