Wananchi wampuuza Zitto na ACT Wazalendo, wajitokeza kujiunga na bima ya afya

blix22

Senior Member
Joined
Jun 23, 2013
Messages
157
Points
500

blix22

Senior Member
Joined Jun 23, 2013
157 500
Leo nilipita katika ofisi ya Kurasini kushughulikia issue yangu ya bima kwenye mida ya saa tano hivi, nilichokikuta ni foleni ya Watanzania na kila uliyemuuliza alisema amekuja kujiunga na vifurushi.

Cha kushangaza wapo niliowakuta ambao wanasema wameanza kufuatilia tangu jana na kikubwa ni kukamilisha mahitaji ili waweze kujiunga na kufurahia huduma.

Watanzania wameanza kufuata uhalisia na kuachana na Siasa, nadhani Zitto ambaye yeye na familia yake wana bima tena labda za private ambazo gharama zake ni kubwa, aache kuwahadaa wananchi, awaache wajiunge na wajikomboe kwa bima ya Tsh 192,000.

Zitto mshahara wake kama Mbunge tu ni mamilioni, hapo usihesabu zile pesa anazopewa na wadau wake, kwake yeye huduma ya afya sio tatizo hata kama ikibidi atibiwe kwa milioni 2 kwa siku anaweza kumudu, vipi jamani tunawadanganya Watanzania.

Ifike mahali tumuache mwananchi aamue kutibiwa kwa 192,000 kwa mwaka, kwa hesabu za haraka haraka ni kama Shilingi 600 hivi kwa siku, tena hapa niliona hadi ma CT Scan sijui ma MRI yamo mule.

Siasa za maendeleo nadhani ni muhimu kuliko siasa za kuwadanganya Watanzania, ili upate madaraka.
 
Vangigula

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2015
Messages
388
Points
1,000

Vangigula

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2015
388 1,000
Hiyo 192,000 inalipwa kwa mafungu au ndo mara moja? Maana kama tulimhurumia Mtanzania mnyonge kwamba atashindwa kumlipia mtoto ada ya 20,000, tukaona tumbebee huu mzigo kwa elimu bure, je huyu huyu mnyonge leo amekuwa na nguvu ya kufanya foleni kulipa 192,000?
 
ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Messages
4,000
Points
2,000

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined May 23, 2017
4,000 2,000
Hiyo 192,000 inalipwa kwa mafungu au ndo mara moja? Maana kama tulimhurumia Mtanzania mnyonge kwamba atashindwa kumlipia mtoto ada ya 20,000, tukaona tumbebee huu mzigo kwa elimu bure, je huyu huyu mnyonge leo amekuwa na nguvu ya kufanya foleni kulipa 192,000?
Bora iwe kinyume chake ndio mnyonge angepata unafuu
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Messages
3,652
Points
2,000

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2011
3,652 2,000
Soma vifurushi vizuri..

Kwanza hakuna hata kimoja kinachotibu magonjwa makubwa..

Hivi kuna m Tanzania anaweza jitibia kansa, moyo , au figo akiumwa ghafla?

Why bima ya taifa..inakataa kumtibu mlipa kodi akiumwa ugonjwa mkubwa.. huku nhif imeanzishwa kwa kodi za huyo huyo mlipa kodi
 
blix22

Senior Member
Joined
Jun 23, 2013
Messages
157
Points
500

blix22

Senior Member
Joined Jun 23, 2013
157 500
Soma vifurushi vizuri..

Kwanza hakuna hata kimoja kinachotibu magonjwa makubwa..

Hivi kuna m Tanzania anaweza jitibia kansa, moyo , au figo akiumwa ghafla?

Why bima ya taifa..inakataa kumtibu mlipa kodi akiumwa ugonjwa mkubwa.. huku nhif imeanzishwa kwa kodi za huyo huyo mlipa kodi
Nadhani kaka wewe ndio ukasome, sipigi wala sitaki siasa... nimevisoma nimevielewa vizuri yaani kwa 192k nipate hadi huduma za kibingwa, upasuaji mkubwa na mdogo sijui vipimo zaidi ya 160, halaf uje useme kitu gani... siku moja jarb kwenda hospitali na hiyo laki moja na tisini uone kama itabaki au utarudi nayo... Ukifika tu kumuona daktari 10000 au 5000 wakati kama ungekuwa na Hii kitu kwa 192k ni sawa na Shilingi 500 tu... jamani tuacheni siasa... hao wabunge wanastahili zao kubwa za kumudu kila kitu... tusiwadanganye watanzania...
 
blix22

Senior Member
Joined
Jun 23, 2013
Messages
157
Points
500

blix22

Senior Member
Joined Jun 23, 2013
157 500
Hiyo 192,000 inalipwa kwa mafungu au ndo mara moja? Maana kama tulimhurumia Mtanzania mnyonge kwamba atashindwa kumlipia mtoto ada ya 20,000, tukaona tumbebee huu mzigo kwa elimu bure, je huyu huyu mnyonge leo amekuwa na nguvu ya kufanya foleni kulipa 192,000?
Nakumbuka wakati naanza kutafuta huduma za afya nilianza na CHF kitu cha 30000 tu, juzi nimesikia hii, nimeenda kukata na wala sio kwamba mim ni tajiri nimejiuliza tu hiyo 192k kwa mtu mmoja ambayo last week nilitumia 250000 kumtibia mtu mmoja tena kwa siku moja tu... yaan kwa hili siwezi kukubali kugeuka jiwe... tuwashauri wenzetu wakakate...kaka ukija kuumwa utakumbuka na kujidharau kwa kushindwa kutoa 192k
 
Root

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
34,789
Points
2,000

Root

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
34,789 2,000
Soma vifurushi vizuri..

Kwanza hakuna hata kimoja kinachotibu magonjwa makubwa..

Hivi kuna m Tanzania anaweza jitibia kansa, moyo , au figo akiumwa ghafla?

Why bima ya taifa..inakataa kumtibu mlipa kodi akiumwa ugonjwa mkubwa.. huku nhif imeanzishwa kwa kodi za huyo huyo mlipa kodi
Kama figo NHIF iliwasaidia wengi. Leo ukiipata zile 250K za kila siku sijui zatoka wapi
 
Keynes

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
517
Points
225

Keynes

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
517 225
zito kaumbuka sana....miminilikua namfuatiliaga sana lakini kwa hili ameniangusha. Vifurushi ni njia bora ya kuelekea bima ya afya kwa wote.
 
Vangigula

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2015
Messages
388
Points
1,000

Vangigula

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2015
388 1,000
Nakumbuka wakati naanza kutafuta huduma za afya nilianza na CHF kitu cha 30000 tu, juzi nimesikia hii, nimeenda kukata na wala sio kwamba mim ni tajiri nimejiuliza tu hiyo 192k kwa mtu mmoja ambayo last week nilitumia 250000 kumtibia mtu mmoja tena kwa siku moja tu... yaan kwa hili siwezi kukubali kugeuka jiwe... tuwashauri wenzetu wakakate...kaka ukija kuumwa utakumbuka na kujidharau kwa kushindwa kutoa 192k
Sina haja ya kukupinga wala kubishia mtazamo wako, lakini mkuu, uko out of touch with reality. Usijiangalie wewe kwa vile unaweza afford hizo 50,000 au 100,000. Wafikirie vijijini huko ambao sometimes mtu akiugua dawa za shilingi 5000 zinakosekana mpaka mgonjwa anakufa. Wafikirie ambao mgonjwa akipewa rufaa tokea hospital ya kijiji kwenda kwenye kituo cha afya, ukoo unapitisha mchango ipatikañe angalau 20,000 ya nauli. Hizo cases ni common sana huko vijijini, je hao ndo unategemea walipe 192,000 per head kila mwaka?
 
macson3

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2017
Messages
748
Points
1,000

macson3

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2017
748 1,000
Sina haja ya kukupinga wala kubishia mtazamo wako, lakini mkuu, uko out of touch with reality. Usijiangalie wewe kwa vile unaweza afford hizo 50,000 au 100,000. Wafikirie vijijini huko ambao sometimes mtu akiugua dawa za shilingi 5000 zinakosekana mpaka mgonjwa anakufa. Wafikirie ambao mgonjwa akipewa rufaa tokea hospital ya kijiji kwenda kwenye kituo cha afya, ukoo unapitisha mchango ipatikañe angalau 20,000 ya nauli. Hizo cases ni common sana huko vijijini, je hao ndo unategemea walipe 192,000 per head kila mwaka?
Mkuu mimi kuna kipindi nilifanya kazi hospital idara ya malipo,kiukweli watu ni masikini sana,buku tu ya cheti mtu hana na hata ukimuangalia alivyo vaa unakubali kweli hana pesa. Inatia huruma sana vijijini. Bei ni kubwa sana hiyo bora ICHF ingawa ina mipaka sana.
 
ManchoG

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Messages
1,346
Points
2,000

ManchoG

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2017
1,346 2,000
Mnajua maisha halisi ya watanzania_au mnakodiwa kuandika ujinga

Nina ndugu yupo kijijini alipata dharura ya kiafya nikamtumia 30K Tsh alinishukuru kwa sms nyingi nahisi ningekuwa karibu siku hiyo angelamba miguu yangu

Kuna siku yupo sawa nikamchana nikamwambia kwanini anakaa bila akiba tena mwanaume hajui ni hatari

Akaniambia "ndugu yangu tema mate chini na shukuru mwezi unaweza katika hata elfu kumi siijui rangi yake" Nikaamua kumpotezea

Sasa ndio nawaza hiyo bima kwa mtu kama huyu na nalinganisha na kauli zenu, naona kama watu mnaoishi dunia mbili tofauti
 
Cherenganya

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2018
Messages
1,112
Points
2,000

Cherenganya

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2018
1,112 2,000
Hiyo 192,000 inalipwa kwa mafungu au ndo mara moja? Maana kama tulimhurumia Mtanzania mnyonge kwamba atashindwa kumlipia mtoto ada ya 20,000, tukaona tumbebee huu mzigo kwa elimu bure, je huyu huyu mnyonge leo amekuwa na nguvu ya kufanya foleni kulipa 192,000?
Nyie hata mngeambiwa 20,000/- mngesema kwanini isiwe 10,000/-.

Hii hulka sijui tunaiondoje kwenye vichwa vya watanzania?
 
Keynes

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
517
Points
225

Keynes

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
517 225
maswala ya bima ya afya nimekuwa nikifuatilia sana mara kwa mara na ninashukuru angalau nina uelewa kidogo wa maswala haya.

Tunachotaka kuelewa wananchi ni kwamba Mfumo wa Bima ya Afya duniani kote unaenda kwa mfumo wa uchangiaji....Unachangia kabla hujaugua. Sasa katika uchangiaji huu makampuni au taasisi za Bima ni lazima ziweke garama za uchangiaji zenye uhalisia na kulingana na huduma atakazopata mchangiaji. Yaani uchangiaji lazima uendane na kitita cha mafao.

Sasa majadiliano ninayo yaona huku kwa Great thinker wanazungumzia hali ya mtanzania mnyonge ambayo kipimo cha unyonge hakipo lakini NHIF tayari wana kipimo cha garama halisi ya huduma na uchangiaji. HIVYO HUWEZI KUWALAZIMISHA WENZETU WA NHIF Washushe garama mpaka huduma zishindwe kulipika. Garama ya Kipimo cha MRI tu kwa cash ni TZS 500,000 MARA MOJA.

Hivyo watanzania kwanza tunatakiwa kuwashukuru wenzetu kwa kutengeneza hii fursa na kuwezesha watanzania wengi KUJIPIMIA...........JIPIMIENI NDUGU ZANGU achaneni na siasa.
 
Oii

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2017
Messages
3,181
Points
2,000

Oii

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2017
3,181 2,000
Soma vifurushi vizuri..

Kwanza hakuna hata kimoja kinachotibu magonjwa makubwa..

Hivi kuna m Tanzania anaweza jitibia kansa, moyo , au figo akiumwa ghafla?

Why bima ya taifa..inakataa kumtibu mlipa kodi akiumwa ugonjwa mkubwa.. huku nhif imeanzishwa kwa kodi za huyo huyo mlipa kodi
Kansa inatibiwa ocean road, bure.
 
Forum statistics

Threads 1,379,949
Members 525,639
Posts 33,761,999
Top