Wananchi wampa umaarufu Zitto Kabwe

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
10/5/2007

*Mgodi wa Buzwagi waitwa Kabwe Gold Mine

Na Shija Felician, Kahama
Mwananchi


WAKAZI wanaoishi kuzunguka eneo la Mgodi wa Buzwagi, wamelibadili jina la Mgodi huo na kuuita Kabwe Gold Mine.

Hali hiyo ilibainika baada ya waandishi wa Habari kutembelea eneo hilo na kukuta mabango yakionyesha maandishi jina hilo.

Kuitwa kwa jina hilo, kunatokana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zito Kabwe kupinga kusainiwa kwa mkataba wa mgodi huo nchini Uingereza na kusababisha kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya bunge.

Baadhi ya wakazi waliohojiwa kuhusu jina hilo, walidai wameamua kuuita hivyo, kwa sababu mbunge huyo anajali maslahi ya wakazi wa Buzwagi.

Tumeamua kuuita Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi kuwa Mgodi wa Kabwe tukiwa na maana ya kwamba huo ndio uliosababisha Mbunge huyo akafukuzwa bungeni, " walisema kwa nyakati tofauti.

Kumekuwa na malumbano ya kisiasa takribani miezi mitatu kuhusu utata wa ufungaji wa mkataba huo wa Buzwagi uliofanywa baina ya Kampuni ya Barrick na Serikali ya Tanzania hali iliyosababisha baadhi ya wanasiasa kuchukua nafasi hiyo kujipatia umaarufu wa kisiasa.

Baadhi ya Wabunge wa Kanda ya Ziwa wamekuwa wakizomewa mara kwa mara na wananchi wao pindi wanapozungumzia mgogoro huo kwenye mikutano ya hadhara.

Wanachi hao wanauzunguka Mgodi huo wamekuwa wakimsifia Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwani kwa sasa wanamuona kama mkombozi wao.
 
Kwenye gazeti la Mwananchi jana kulikuwa na nakala inayozungumzia ziara wa waandishi wa habari mgodini Buzwagi,Ulinzi ni wahali ya juu camera haziruhusiwi!! kuna kaguzi lukuki. cha ajabu waandishi hawakuweza ona dhahabu zaidi ya mchanga. Chakuvutia waliweza piga picha moja ya magreda yale likiwa limeandikwa ZITO KABWE... kwa kweli Mh Kabwe yupo matawi ya juu..asikubali kushushwa ama kujishusha.
 
kweli hiyo picha licha ya kuvutia inakufanya mtu ukae chini na kufikiria sana.kama mtu aliyeko humo ndani mgodini anafikia kuupa jina "Zitto Kabwe" mtambo huo inaleta maswali mengi,kwamba kwa nini wasiubatize "Jakaya Kikwete" (ambaye anadaiwa kuwa "mtu wa watu" au "ametumwa na Mungu")?je ni kwa sababu Zitto kagusa kilio cha watu wengi hapa Tanzania?maswali nimengi ila kinachotia matumaini ni kuwa ukombozi wa kifikra kwa watanzania dhidi ya ufisadi wa CCM umeanza kuingia kwa kasi kuliko tulivyotegemea.Maana zamani CCM walitegemea nguvu na ngome yao kubwa huko kunakoitwa "vijijini/mikoani" (ambako mafisadi wengi wa CCM wanatoka),sasa kwa kuwa huko nako msingi unayeyuka kwa kasi naamini come 2010 tutakuwa na wabunge wa kutosha tu tuka Upinzani...
 
Hakuna kosa la kiufundi ccm walilofanya kama kumfukuza mh. Zitto. Naamini babu ya Malechela ambaye aliinjia zoezi lile akitafakari yanayoendelea anajutia ushauri wake kwa kiasi kikubwa.Nasi tunawashukuru kwa kutusaidia kufumbua macho wananchi amabo wengi wanahitaji n=mifano ya dhahiri "ushahidi" kama walivyofundishwa na utawala uliopita ili wakubali. Sasa ushahidi umepatikana kupitia 'Buzwagi'
 
Back
Top Bottom